Huyu rafiki yangu 'fainali uzeeni' ananitakia mema kweli?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,460
40,451
Katika pita pita zangu, za mtaa kwa mtaa, nikakutana na kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la fainali uzeeni

Huyu kijana akaniomba tuwe marafiki, ili tuwe tunashauriana kuhusu harakati za maisha ya hapa duniani. Nami nikaona ni busara, tuwe marafiki ili tuwe tunabadilishana mawazo.

Kesho yake ilipofika, nikaamua kwenda bar angalau kukata kiu, kutokana na uchovu wa hapa na pale, nilikunywa bia nyingi sana mpaka nikatumia mpaka nauli, nilipotaka kuondoka, kwa mbali nikamuona rafiki yangu fainali uzeeni ananipungia mkono, nami nikampungia mkono kama kawaida yetu.

Baada ya wiki, nikaamua kwenda disko; kule nikatumia sana pesa, nikawanywesha marafiki, warembo wote nikawa nawalipia bili; kuja kushtuka, kuangalia kwenye waleti, nakuta kuna shilingi mia tano tu. Ile nainua kichwa ili nipige mahesabu vizuri, namuona rafiki yangu fainali uzeeni anapita na boda boda.

Majuzi tena, warembo wakali wakawa wananikubali kutokana na pamba zangu; nami nikawa nawaonga pesa ili niweze kuwa nao kwenye mahusiano; nilifanikiwa kuwa na wadada wengi sana, nikawa nawafungulia biashara, nawanunulia viwanja n.k

Nilipoenda kwenye mashine ya ATM ili nitoe pesa nimuonge mrembo Mwajuma akalipie kodi ya nyumba, nikakutana na rafiki yangu fainali uzeeni naye yupo kwenye foleni ya kwenda kwenye ATM mashine.

Sasa najiuliza wakuu, huyu rafiki yangu fainali uzeeni, nakutana naye karibia kila sehemu ninapokwenda; Je, huyu ni rafiki mzuri kweli kwangu? au ni mzimu unaonipeleleza?

Nitumie njia gani, ili asiwe ananifuatilia?​
 
Ulishawahi kujibu swali kwenye mtihani ukahisi umepatia jibu sahihi; baada ya matokeo kutoka ukawa umepata sifuri?
Mada zingine zinatumia 'fasihi', unatakiwa uwe na upeo mkubwa wa kuchanganua mambo.
Pia mada zingine hazina ukweli wowote, 'just for entertainment' ndio maana watu wanapewa 'script' kuigiza 'movie'​
Nimepitia haka ka uzi nimekupata vyema.
Ispokuwa wakurupukaji wengi hasa wanao kaa kwa Mashemeji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom