Huyu ni Lugumi tena? Kwanini asitajwe hadharani?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,514
2,000
678989988.jpg

Magufuli afichua ufisadi wa bil. 60/- Jeshi la Polisi
WAKATI sakata la mkataba wa Sh. bilioni 37 kati ya polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises wa zabuni ya kufunga vifaa vya kutambua alama za vidole likiwa limeanza kupoa, Rais John Magufuli, amenusa ufisadi mwingine kwenye jeshi hilo wa takriban Sh. bilioni 60.

Rais Magufuli alianika kashfa hiyo mbele ya viongozi wakuu wa polisi nchini waliohudhuria shughuli iliyohusisha Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) ambao aliwapandisha vyeo hivi karibuni walipokuwa wakila kiapo cha uadilifu wa utumishi wa umma.

Alisema ana taarifa kuwa mwishoni mwa mwaka jana, kuna mtu alipewa kazi ya kununua sare za polisi na kupewa fedha zinazotakiwa ndani ya wiki moja, lakini mpaka sasa bado hakuna nguo zilizoletwa.

Kufuatia hali hiyo, Rais Magufuli ameagiza viongozi wa polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kufanya uchunguzi juu ya suala hilo na wakigundua taarifa hizo zina ukweli, basi watu waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

Alisema wakati kukiwa na ubadhirifu huo wa mabilioni ya fedha za umma, polisi imeshindwa kukomboa magari yake 77 iliyoyaagiza na sasa yameshikiliwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

“Kwa hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wewe ni mwanasheria na Meja Jenerali, waliohusika wapelekwe mbele ya haki,” alisema na kuongeza:

“Kuna watu wanasema fedha zilizotolewa ni Sh. bilioni 40, wengine Sh. bilioni 60, wengine Sh. bilioni 20, na fedha zote zilitolewa ndani ya wiki moja,” alisema Rais Magufuli.

“Naomba suala hili lifuatiliwe, kama ni kweli, fedha hizi zikombolewe hata zikakomboe magari yenu.”

Kashfa hiyo ya sare za polisi imekuja wakati sakata la ufungaji wa mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi lilichunguzwa na Bunge hivi karubuni.

Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliunda kamati ndogo kulichunguza suala hilo na Bunge kuagiza serikali kushughulikia kasoro hizo ndani ya miezi mitatu bila ya kuzitaja.

Rais Magufuli aliwahi kuzungumzia anavyokerwa na mikataba mibovu ya polisi na taasisi nyingine wakati alipofungua mkutano wa makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa na vikosi, kilichofanyika Aprili 29, mwaka huu mjini Dodoma..

“Oysterbay (jijini Dar es Salaam) pale ni eneo ambalo ni very `prime’ (lenye thamani kubwa), kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua ninyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa,” alikaririwa Rais Magufuli akizungumzia suala hilo.

Katika hatua nyingine jana, Rais Magufuli jana alilitaka jeshi hilo na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.

Chanzo:Nipashe
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Nilisikia jana mkuu mwenyewe analalamika nikasema kweli hii nchi kuna watu wana nguvu. Ila ndio mtaji wa kuanzia kwenye ile Mahakama ya mafisadi majaji wako Lushoto wanajifua
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,905
2,000
BAK huyo Lugumi akiguswa itakuwa shida ndo maana hilo swala limeshafunikwa tayari
 

interlacs

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
211
250
Hapo Raisi wetu alitumia hekima. Kwa mtu mzima lazima ajiongeze. Kama ni jipu lilipasuliwa mchana kweupee!
 

kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,340
1,500
Hizo ni senema tu kama kawaida. Lengo kuwa-keep busy watanzania ili siku zisogee. Hapa na pale tayari 2020. Rais hakumaanisha hivyo. Yeye amemaanisha trafiki waachwe wachukue 5,000/= ili kubrash viatu. Nimekumbuka enzi za Mobutu Seseseko, askari walikuwa hawalipwi mshahara kwa hoja kwamb watumie bunduki zao kujilipa. Mobutu alikuwa dikteta aliyekubuu. Hizi tunazoona ni mawingu ambayo ni dalili za mvua.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,924
2,000
Hizo ni senema tu kama kawaida. Lengo kuwa-keep busy watanzania ili siku zisogee. Hapa na pale tayari 2020. Rais hakumaanisha hivyo. Yeye amemaanisha trafiki waachwe wachukue 5,000/= ili kubrash viatu. Nimekumbuka enzi za Mobutu Seseseko, askari walikuwa hawalipwi mshahara kwa hoja kwamb watumie bunduki zao kujilipa. Mobutu alikuwa dikteta aliyekubuu. Hizi tunazoona ni mawingu ambayo ni dalili za mvua.
Maelezo yako yamejaa chuki zako zilizo moyoni dhidi ya Raisi,hujachangia wala kujibu hoja ya mtoa mada,huo mfano wako wa Mobutu hauhusiani na chochote kwenye huu Uzi,mbona hujacoment raisi alipomlalamikia bosi wa polisi aliyekuwa akiombwa mafuta ya gari,anawajibu askari watumie vyeo vyao kupata mafuta??,au hujaangalie speech yote?,ulichoambulia ni kuhusu Trafic tu?,acheni unafiki.Mnaboa sana
 

kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,340
1,500
Ukiona rais analalamika ujue kuna tatizo katika utendaji wake. Na hasa anapomlalamikia mtu mdogo ambaye ni mhasibu wala hana madhara yeyote. Mobutu ni mfano mzuri shida yako ni uelewa mdogo wa association and synthesis of distant related issues.@Jmc06
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,331
2,000
“Kuna watu wanasema fedha zilizotolewa ni Sh. bilioni 40, wengine Sh. bilioni 60, wengine Sh. bilioni 20, na fedha zote zilitolewa ndani ya wiki moja,” alisema Rais Magufuli.
Hivi ni nani anakaa na Rais na kumpa hizi taarifa zisizo na uhakika .... mara 20, mara 40 mara 60 ......!!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,514
2,000
Huyu ni mtu wa majanga Mkuu. Madudu mbali mbali aliyoyafanya katika nyadhifa mbali mbali alizowahi kushika na madudu katika familia yake ni ushahidi tosha kwamba hana sifa ya uongozi hata chembe.

Mkapa na Kikwete kwa kuweka mbele maslahi yao ya kulindwa kwenye maovu waliyoyatenda walipokuwa madarakani nchi inapitia wakati mgumu kuliko kipindi chochote kile kutokana na kuwa na mtu ambaye hakustahili kupewa uongozi wa nchi.

Hivi ni nani anakaa na Rais na kumpa hizi taarifa zisizo na uhakika .... mara 20, mara 40 mara 60 ......!!
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,905
2,000
Naona limeshazimwa rasmi na huyu aliyejitoa kafara kupambana na mafisadi.
alikuwa anaongea hakuna nia ya dhati kweli kutokana moyo sijawahi kuamini kauli zake wala sitawahi kuamini kauli zake
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom