Huyu ndiyo Zitto ninayemjua

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
4,305
Reaction score
2,564
Zitto Zubery Kabwe amepangua hoja dhaifu za CCM kuhusu gharama za uendeshaji wa serikali ya shirikisho kwa kuwaambia kuwa Tanzania inao uwezo wa kuendesha serikali ya idadi yoyote ile ikiwa serikali itaongeza umakini kwenye kukusanya kodi kutoka kwa makampuni makubwa.

Anasema kuwa Taifa linapoteza zaidi ya shilingi trilioni 2 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi.Anasema kama kodi zitakusanywa barabara haoni ni kwanini tushindwe kuendesha serikali tatu.Aidha anaongeza kwa kusema kuwa anawashangaa baadhi ya wajumbe wanaowatisha Watanzania kwa kusema kwamba tukiwa na mfumo wa serikali tatu kwasababu ya gharama za kuiendesha itawaongezea mzigo wa kodi wananchi

Akasema hiyo siyo kweli, Kiasi kikubwa cha kodi kinachosamehewa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi kinatosha kabisa kuendesha mfumo wa serikali tatu.

Akamalizia kwa kuonya kwamba,Gharama za kuvunjika kwa muungano ni kubwa kuliko kuendesha serikali tatu kwasababu kila upande utaingia gharama ya kuilinda mipaka yake mara baada ya muungano kuvunjika.

Akatolea mfano suala la eneo la gesi na mafuta baharini ambalo nusu Zanzibar na nusu Bara kwamba hili linaweza kuzaa mgogoro mkubwa kuhusu nani ana uhalali wa kumiliki mafuta na gesi baharini.

 
Zitto akikua akaacha kutokueleweka, atakuja kuwa mwanasiasa mzuri atakayeaminiwa. Anauwezo mkubwa sana wa kujenga hoja vizuri kimantiki, na pia anauwezo mzuri wa kusaliti.
 
He is not an ideological fanatic like many of you would expect him to be,He is an independent and free thinker something which many of you are not familiar with but it's a normal thing in the advanced and civilized world.

what did u mean?
 
Haaminiki huyo...sawa na kumkabidhi fisi bucha
NB.huwezi jua kesho atasemaje km atajaziwa mzigo CRDB
 
Zitto ashasema serikali 3 zenye rais moja na mawaziri wakuu watendaji wawili Znz na Tanganyika....lakini hili la gharama za Muungano via tax exception was briefly mentioned na Mbowe jana....

Huyu anadhani uwepo wa Executive Premiers ndiyo salama ya Muungano....hapo amepotoka....hoja ya Membe ina uzito sana....ni vema tukaiga shirikisho la wakoloni wetu wapenda maendeleo ya ukweli wa Kijerumani....

Acheni ushabiki wa personalities baadala ya ISSUES.

Nini tofauti yetu kama great thinkers na Bunge la wahuni.....
 
Hebu niangalie briefcase yangu nyekundu
 
ziito hana shida sema ana ugonjwa unaitwa kigomaphobiapoliticks,na hiyo hataweza kuiacha kwani ni wa kurithi kutokana na eneo analotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…