Huyu Ndio JK Bana!!!!!

Muuza sura aka bishoo aka sharobaro aka kilaza aka zero brain aka hajui lolote la maana la kuisaidia nchi..hivi misheni yake b4 kuukwaa uprzdaaa ilikuwa ipi,

Mission yake ilikuwa ni kuukwaa uprzdaaaaa na marupurupu yanayoendana na nafasi hiyo.
 

Una hoja ya msingi. Unaonaje ukiweka hizo data ili tuweze kuona na upande wa pili wa shilingi - yaani kiasi kilichopatikana kutokana na safari za rais, investment alizofanikiwa kuleta kutokana na safari zake, ajira zilizopatikana, kodi iliyokusanywa na iliyosamehewa kutokana na hizo safari.

Ili kukamilisha zaidi uchambuzi wako utueleze kwa kina ni kwa nini awe ni yeye tu ndiye anaenda badala ya kutumia mabalozi, waziri wa mambo ya nje, Tanzania Investment Center na vyombo vingine vya serikali ambavyo vimeundwa kwa shughuli hizo za kutafuta wawekezaji. Pia utueleze huo muda wote aliotumia nje ya nchi ni nani hasa aliyekuwa akitekeleza majukumu yake ya URAIS wa nchi ambayo ndiyo aliyochaguliwa kuyatekeleza?
 
loh! asante mkuu kwa huu upembuzi yakinifu kwa mwenzetu GB!
Atatuelewa tu tuendelee kumuelewesha iv iv!
 
Nina wasi wasi JK anashikilia nafasi mbili za uongozi at once!!!! yaan Waziri wa mambo ya nje (cheo alichokuwa nacho awali) na Uraisi wa nchi
Ni balozo wa Nchi zaidi ya tatu vilevile!!
 

Mwalimu wako wa hesabu (Calculus) akiona hizi assumption zako! Atakukana kuwa ulisomesha na yeye namba.
 
 
 
Bravo Obsesd! wala haihitaji elimu ya chuo kuona hasara tuipatayo. Hali yetu, kupanda kwa hali ya maisha, uchumi hafifu, kuchupa kwa tofauti ya shilingi na dollar, mfumuko wa bei za bidhaa mbali mbali, wabunge kung'ang'ania posho kubwa kwa mteremko, kuongezeka kwa deni la taifa, kupungua kwa ruzuku toka serikalini kusaidia taasisi mbali mbali. Ni uthibitisho kuwa tuko pabaya na tunakokwenda ndo hakufai zaidi.
Geniusbrain anaonyesha wazi kuwa jina lake alipewa na yule bingwa wa reverse!
 
Dada nashukuru sana,

sasa angalia na ziara zake za ndani ambazo hazina tija, angalia ziara za mawaziri ambazo hazimsaidii mtanzania, angalia ufisadi unaofanyika wizara na idara zote za serikali, piga hesabu halafu niambie ni wapi Dr wa Ukweli Slaa alipokosea kusema Elimu na Afya Bure Tanzania vinawezekana.
 
Huyu ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hana majukumu ya kumbana kwa kuwa nchi hizi mbili (Tanganyika na Zanzibar) zinapaswa kuwa na maraisi wao - Zanzibar wanaye. Ndo maana mambo mengi anadelegate kwa mawazili. Sioni sababu ya kumlaum JK; nawalaum Watanganyia kwa kutodai uchaguzi ili wampate rais wao ambaye atakuwa mwakilishi wao kwenye vikao vya Muungano ambapo JK ndo atakuwa mkuu wa vikao vya Muungano. NISOMEKE HIVYO!
 

Hesabu ni logic, viongozi wengi wa serikali tuliyonayo sina uhakika kama wanajua hesabu; wao wanawaza kukwapua mali ya Umma tu!
 
Nakwambia ndugu yangu huyu Bwana Raisi na chama chake CCM hadi waondoke madarakani sijui nchi hii itakuwa wapi???? Maanake kila kukicha anabuni mbinu mpya ya kufilisi nchi kama sie yeye basi ni watu wake kufilisi nchi kwa kwenda mbele, la maana hatulioni!!!!Makampuni ya mufilisi kibao na umeme wao wa diesel na magenerator IPTL,SYMBION POWER,SONGAS, malipo ya capacity charge Tshs 156,000,000/= kila siku sijui hadi lini??? Dhahabu, Tanzanite wanachukua bila kulipa ushuru kila siku sijui itakuwa hivyo hadi lini???
 
Hiyo haisaidii manake ataendelea kuwa mkubwa wao na mufilisi ni pale pale!!!

 
Ileje!
Wengine hata hata panzi anawazidi akili; ona hii;
Yeye akienda nje anarudi na vyandarua,
Wenzake wakija kwetu wanaondoka na dhahabu!
 
Hiyo haisaidii manake ataendelea kuwa mkubwa wao na mufilisi ni pale pale!!!


Ndg! itasaidia; kuna mambo ambayo hatakuwa na majukumu ya moja kwa moja kuyafanya (Rais wa jamhuri) kama ilivyo kwa Zanzibar ambapo wanafanya mambo mengine mengi tu pasipo kumhusisha JK na serikali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…