thread hii imeletwa hapa kimkakati,
kwa kuwa walioleta wanawajua waliowatuma, na kwa kuwa wao kwa ufupi wao wa kufikiri wanaamini kuwa hii ndio silaha yao kwangu, leo nasema ukweli kuhusu hili humu jamvini, tena nasema ukweli bila hata kumung'unya neno hata moja, na wakati nasema ukweli najua kuna watu watasema nilikuwa wapi siku zote.
ndugu zangu, mimi ni muumini mzuri sana wa siasa za kweli na haki, mimininaamini katika mtu kuwa awarded kulingana na nafasi na ushiriki wake, lakini kikubwa mimi ni muumini mzuri wa kuhakikisha chama changu kinaendelea kuwa imara.
NASEMA HIVI.
1. sijakatwa na kuenguliwa BAVICHA kwa sababu ya rushwa, nimekatwa kwa sababu za siasa zenu hizi cha chuki, unafiki na majungu majungu ziizotawaliwa na WOGA...msimamo wangu wa kutokubali kumezeshwa ujinga kichwani mwangu ndio kinachoniponza zaidi.
2. waliokuwepo kwenye kikao wakati nakatwa wanaweza kuthibitisha. alitafutwa hadi GIRLFRIEND wangu aandike mashtaka kuwa mimi sio mstaarabu ili nienguliwe lakini akakataa...wakatafutwa hadi watu wa VCOBA wakasema nimewadhurumu wakatafutwa hadi viongozi wanafiki wakasema nimewatukana..nafahamu moyoni kwanini nilienguliwa BAVICHA na hata HECHE anafahamu kwanini ALIPEWA KITI cha dezo''...hakuna kesi ya rushwa duniani kote yenye adhabu ya kumuengua mtu kwenye uchaguzi na kesi kuishia hapo hapo.. mwanahalisi wao walijikuta wakinitumia kutimiza malengo yao kumshambulia Zitto, in any how kama niliyekatwa ni mimi kulikuwa na haja gani ya kumuhusisha zitto kwenye ukatwaji wangu?.
3. hakuna kesi ya rushwa duniani kote ambayo mwendesha mashtaka ndio huyo huyo mshitaki, ndio huyo huyo shahidi na ndio huyo huyo hakimu....na kama mimi nilienguliwa kwa rushwa MWAMPAMBA alienguliwa kwa kosa gani?...NYAKARUNGU alienguliwa kwa sababu ipi?.
sisi tunaokipenda chama tuliamua kukaa kimya tuendelee kukuza chama, kukaa kwetu kimya hakukumaanisha kuwa ni wajinga. ukwatwaji wangu unahusika moja kwa moja mikakati ya baadhi ya viongozi wa kichama kuhakikisha sishindi, mwanzo walizani nacheza walipoona nguvu yangu wakaungana na kuamua kunikata. nasisitiza tena rushwa ilikuwa ni shitaka moja kati ya mashitaka zaidi ya nane niliyosomewa kwenye hicho kikao.
katika kuwathibitishia kuwa mwanahalisi ilifanya kazi ya kuhalalisha ukatwaji wangu ili kujihami kuwa nilitoa rushwa kwa madai eti chama chetu ni mpiganaji mkuu wa rushwa, naomba nisisitize yafuatayo.
1. Mwanahalisi ambalo ndio linatumiwa kama kielelezo kikuu cha mashtaka yangu imeongopa kama alivyofanya ndugu ben saa nane hii leo.
A. ukijumlisha jumla ya pesa ambazo wanadai nilizituma haziwezi kufika hata laki tano wao wamesema nimetuma jumla ya shilingi milioni 2.5 huu ni uwongo nilioudharau kuupinga lakini sasa lazima niweke kumbukumbu sawa.
B. Mtitiriko wa mashtaka hayo umekaa kiujanja ujanja kiasi kwamba hakukuwa hata na namba moja ya kweli niliyoirushia pesa, leo nitazielezea namba zote zilizoorodheshwa hapo kwenye gazeti hilo.
(i) mwanahalisi wanasema '' Alianza kutapakanya fedha kwa wajumbe 11 Mei 2011 saa 10:44.58 ambapo kiasi cha Sh. 28,500 zilitumwa kwa mmoja wa wajumbe wenye simu Na. 0659 374206''. ukweli ni kwamba mwenye namba 0659374206 hajawahi wala sio mjumbe wa BAVICHA..mwenye namba hiyo kipindi hicho ni mzee hamis lichonyo ambaye umri wake unazidi miaka 63 kwa sasa, huyu ni mzee wangu katika siasa na ni mwenyeji wa mkoa wa lindi, tumefundishwa vijana kuishi vizuri na wazee wetu, hivyo mzee wako anapokuomba msaada si vibaya kumsaidia, nilimsaidia mzee wangu..
(ii) mwanahalisi waliendelea kuongopa ''Mchange alituma Sh. 50,000 kwenda kwa mwenye Na. 0713 867745'' ukweli ni kwamba mmiliki wa namba hii ni ndugu fikirini rajabu, huyu wakati namtumia pesa alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo kikuu cha dodoma akisoma project planning and community development-hajawahi hata kuwa kiongozi wa kata wa chadema wala BAVICHA.
(iii). wakaendelea kudanganya kuwa mchange ''alituma Sh. 19,000 kwa mwenye Na. 0713 866650''. ukweli ni kwamba mmiliki wa namba hii ni NDUGU NKYA ambaye ni mfanya kazi wa kampuni ya simu ya tigo tawi la mlimani city nilipompigia simu baada ya gazeti hili kuchapishwa akacheka sana na kuahidi kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.
(iv) mwanahalisi likaendelea kudanganya watanzania kuwa Wengine waliotumiwa fedha na Mchange; ni wenye Na. 0712 511508 aliyetumiwa Sh. 26,000.....oooh my God MWANAHALISI WALIENDELEA kudanganya, mmiliki wa namba hii anaitwa ALLY MCHANGE, ni kaka yangu wa kuzaliwa, yeye ni mtaalamu wa hotelians na mechanical engineer, hajui lolote kuhusu siasa na wala hana kadi ya chama chochote cha siasa, tukio pekee la kisiasa alilowahi kushiriki ni kunisaidia kwenye kampeni zangu za ubunge wa kibaha. mwanahalisi ni WANAFIKI NA WAONGO KAMA BEN SAA NANE.
(iv) mwanahalisi waliendelea kubwabwaja kuwa saa 12:41.48 alituma Sh. 81,000 kwa mwenue Na. 0714 038536. hapa waliendelea kudanganya sana, mwenye namba hii anaitwa NYEMBO M. TEMBA huyu hajawahi kuwa mjumbe waBAVICHA HATA SIKU MOJA, yeye ni msaidizi wa mweshimiwa zitto kabwe tena jimboni kigoma kaskazini tena wa kijijini mwandiga.
(V) Uwongo mwingine wa MWANAHALISI NI HUU kuwa niliendelea kutuma pesa kwenda kwa mjumbe mwenye mwenye Na. 0713 606169 aliyetumiwa Sh. 10,000 ambaye alitumiwa fedha hizo, saa 22:24.31. --hapa pia walidanganya kikamilifu, mmiliki wa namba hii anaitwa EDWARD KINABO (naye ni mwana JF), na kipindi hicho naye alikuwa anagombea ujumbe wa BARAZA KUU KUPITIA BAVICHA huku akiwa ni mwandishi wa habari wa GAZETI LA TANZANIA DAIMA na makala zake maarufu za WARAKA WA KINABO, ni rafiki yangu sana sana siku hiyo nilikutana naye sinza, WHITE INN BAR akaniambia ndugu yangu nataka kwenda sehemu lakini sina pesa, mimi nikamwambia sina CASH naweza kukurushia kwenye TIGO PESA tukakubaliana nikamrushia tukaachana akaenda na zake. gazeti lilipotoka hakuwa ameiona namba yake, akanipigia simu kunipa pole, nikamwambia sijawahi kutoa rushwa kwenye maisha yangu, na sitakuja kutoa rushwa mpaka naingia kaburini, akabisha nikamwonyesha namba yake, nikamuuliza nawewe nilikupa rushwa?. akasikitika tukaendelea na mishe nyingine...
namba pekee ya mjumbe wa bavicha bwana liberatus dotto ambaye nilimtumia jumla ya shilingi 40 elf (mwanahalisi wao wamedanganya kuwa nilimrushia laki moja na nusu-150,000/=) ambazo yeye mwenyewe aliniomba mara nne tofauti, mara ni 0717 268576 AMBAYE KUMBE ALITUMWA NA WAPINZANI WANGU ASEME NIMEMPA RUSHWA, Mungu ni mkubwa kwani wakati anatoa ushuhuda wa mimi kumrushia yeye rushwa ya nauli tayari nilishapata nakala ya ticket yake ya ndege ya shirika la precision air yenye namba E-TICKET NUMBER 03144109725678 ya ndege aina PW411 ya kwenda Dar tarehe 25.05.2012 na kurudi mwanza tarehe 02.07.2012 AMBAPO ALIWASILI JKN AIRPORT SAA 10:00AM na kurudi mwanza kwa ndege ya saa 18:00 jioni kwa tarehe hisika. ticketi hizi zililipiwa na kiongozi mmoja wa chama ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mbunge na taarifa zinasema alirudishiwa pesa zake na chama baada ya kutimiza kazi zake ipasavyo---hapa walidhihirisha ujinga wao na nikazidi kuwadharau..maana wamenishtaki kwa kutoa rushwa ya kutengeneza huku wao wakitoa rushwa ya zaidi ya laki 3.7 kwa ticket....
MWANAHALISI walishindwa kuthibitisha kuonyesha Transactions za watu waliowataja kama Wlfred kitundu wa singida na mwengine yeyote, badala yake wakachukua print out zangu za tigo na mpesa na kuzihusianisha na rushwa, hii ni lugha ile ile aliyoionyesha saa nane humu jamvini..
siku katibu mkuu ananisomea haya mashtaka sikuamini macho na masikio yamgu, sikuamini kama kiongozi niliyekuwa nataraji angekuwa rais miezi sita nyuma angeweza kushiriki kwenye uwongo wa namna ile..
narudia sikutaka kuweka hadharani haya kwa sababu yanawahusu moja kwa moja viongozi wangu wa chama..
nasema tena kwa msisitizo, SIJAENGULIWA BAVICHA KWA SABABU YA RUSHWA, NIMEENGULIWA KWA SABABU YA SIASA ZA WOGA DHIDI YA MAHUSIANO YANGU NA ZITTO.
nitaendelea kufichua kila unafiki dhidi yangu mpaka hapo jamii itakapoelewa na kuziona true colours za baadhi ya wiongozi wetu.