Huyu ndio Faru Fausta wa Ngorongoro,atimiza miaka 54,aishi chini ya ulinzi wa kijeshi masaa 24

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
image.png


========================================
Wakuu huyu ndio Faru Fausta ambaye ni kipofu,usahihi wa habari hii umeletwa na na mkuu cDNA na Sakasaka Mao
Jf kisima cha maarifa

barafu


FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni
Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi

FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.

Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona.

Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.

Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.

Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua hatua juu ya Faru Fausta.
 
Hata Mimi nashangaa. ...hawa wanyama ni baraka kutoka kwa MWENYE ENZI MUNGU inabidi tuwalinde na kuwa tunza. ..pamoja na misitu yetu lazima tuithamini kwa kiwango cha juu sana. ...
Hiyo picha ni fotoshop, ama ni ya maktaba kutoka maeneo mengine katika Afrika.
Hakuna hapa Tz jeshi la taifa kulinda kitu kiitwacho faru. Kazi hiyo hufanywa na askari wa wanyama pori na sikuhizi wanapewa mafunzo maalumu ya kijeshi-usu(para military).
Huyo askari alivyokaakaa ni kama askari wa Kenya kutokana na mavazi aliyovaa pamoja na aina ya bunduki aliyoshikilia mikononi mwake.
 
Back
Top Bottom