Huyu ndio Faru Fausta wa Ngorongoro,atimiza miaka 54,aishi chini ya ulinzi wa kijeshi masaa 24

Pamoja na kula majani anakuwa kipofu!!

Nahisi msiba wake utatangazwa soon.
 
View attachment 465022

FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni
.Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi

FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.
Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona.
Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.
Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.
Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua
hatua juu ya Faru Fausta
Hapo mwisho pamenitisha hapo pa gharama na hatua
 
Gharama gani ikiwa ha ma-game wanalipwa mshahara kwa kodi na mapato ya hao wanyama?
 
Sijui kuwa ni kwanini hatutumii akili zetu japo kiduchu...

Wataalamu ingieni maabara tengenezeni genes ambazo zitatoa faru asiye na pembe, vivyohivyo kwa tembo... labda wataongezeka na gharama ya kuwalinda itapungua..

Ikishindikana basi zikateni kama tufanyavyo kwa ng'ombe.
 
Majangiri sio nature mkuu
Sasa jangili atamuua huyo Fausta ili apate nini wakati hata pembe zimebaki kama gunzi?
NB: unafahamu ni kiasi gani kinatumika kumlinda? Na yeye kwa kulindwa kwake anaingiza kiasi gani?
 
Sasa jangili atamuua huyo Fausta ili apate nini wakati hata pembe zimebaki kama gunzi?
Mkuu majangili huwa wanaua faru wasiokuwa na pembe pia kwa sababu wanachukua muda mrefu kumfuatilia faru halaf wanakuta hana pembe wanamuua ili wasije wakapoteza muda kumfuatilia tena siku nyingine
 
Mkuu majangili huwa wanaua faru wasiokuwa na pembe pia kwa sababu wanachukua muda mrefu kumfuatilia faru halaf wanakuta hana pembe wanamuua ili wasije wakapoteza muda kumfuatilia tena siku nyingine
Una ushahidi? Unafikiri majangili wana bahatisha ama kukurupuka? Wana network kubwa mno hadi game rangers, maofisa wa wizara, idara ya wanyamapori, hifadhi na mapori ya akiba. Wanafahamu nini wanakifanya.

Ndiyo maana kuna kipindi South Africa walianza kuwakata faru pembe zao katika kupunguza kasi ya wao kuuliwa. Lakini watu wa haki za wanyama wakipigia kelele hilo, na likasitishwa.
 
Mkuu majangili huwa wanaua faru wasiokuwa na pembe pia kwa sababu wanachukua muda mrefu kumfuatilia faru halaf wanakuta hana pembe wanamuua ili wasije wakapoteza muda kumfuatilia tena siku nyingine
Uliyajuaje hayo yote??
Itabidi ukalisaidia jeshi
 
Back
Top Bottom