Huyu mwanaume jamani!

Huyu mwanaume jamani!

jack 1

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
61
Reaction score
63
Kanipa mimba hataki kueleweka, katoa mahali nyumbani harusi ilikua mwezi wa 5 tangu nimemwambia ninamimba anarusha miezi mara wa 7 mara wa 10 sasa kasema mwaka kesho, wazazi wa pande mbili hataki wajue kama ninamimba mimi naishi kwangu wanza nlikua nafanya kazi sasa nimeachishwa sababu ya kuumwa umwa kutokana na ujauzito ananiambia nikae hukuhuku nyumbani wasijue chochote mpaka nijifungue ndo mipango ya harusi iendelee,sasa nishaurini nitakaaje huku sina ndugu sina kazi nitaishije na huu ujauzito kumbuka ni mimba ya kwanza nikipata matatizo hakuna wa kunisaidia na yeye yupo arusha,nifanyeje?
 
Aisee hivi wanaume tunaweza kuwa wakatili namna hii,mfate Arusha na uonane na wazazi wake full stop.Pole sana wangu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama kwao wanajua uansubirir nin tena nenda ukawajulishe, maana ukija kujifungua alafu ndio mfunge ndoa atakuja kuzusha jengine
 
Mfuate huko huko Arusha kila kitu kitafahamika.wewe unazani ukipata matatizo mwanza nani atakusaidia?tafakari chukua hatua
 
kanipa mimba hataki kueleweka, katoa mahali nyumban harusi ilikua mwez wa 5tangu nimemwambia ninamimba anarusha miez mara wa 7 mara wa 10 sasa kasema mwaka kesho...., wazazi wa pande mbili hataki wajue kama ninamimba mm naishi kwangu mwanza nlikua nafanya kazi sasa nimeachishwa sababu ya kuumwa umwa kutokana na ujauzito ananiambia nikae hukuhuku nyumbani wasijue chochote mpaka nijifungue ndo mipango ya harusi iendelee... sasa nishaulini nitakaaje huku sina ndugu sina kazi nitaishije na huu ujauzito kumbuka ni mimba ya kwanza nikipata matatizo hakuna wa kunisaidia na yeye yupo arusha...nifanyeje?

pole sana Jacky.
U knw what..haya ni maisha yako na ni afya yako,,wewe ndio unafeel kila kitu na sio that idiot..sory but yes he is.
Me nngekuwa wewe..
Ningeenda kwetu niwashhirikishe ndugu zangu wenye akili,then ndugu zake wajue pia. .i mean ninge either force or shawishi hadi kieleweke.
Come on girl we ungekuwa ndo yeye ungemfanyia hivyo yeye?
Then hizo tarehe za ndoa em weka tag , cos nmemsoma kama mtu ambaye hayupo tayari kukuoa ama anakitu anaficha.
Even if he is a nice and perfect for you but honey u gotta raise ur eyebrows and think HARD with ur brain.
Kwa situation kama yako na reactions zake hmmmm. Pliiizz
 
pole chagua moja kwenda arusha au kwa wazaz wako kuliko kuish mwanza!!!!
 
Mbona unasema harusi ilikuwa mwezi wa tano? Mnafunga harusi nyingine? But all in all the guy is not serious.
 
Mamaa changamka. Utapigwa chini muda si mrefu.....funga safari nenda Arusha. Lakini pia waambie ndugu/wazazi wako na wake pia wajue una mimba. Ukichelewa kidogo tu utashaa.
Ukikuta manyoya ujue keshaliwa
 
kama kweli...kuna wanaume irresponsible...mm umri ulivyoenda hivi...nlitewe alafu iwe yangu...dah
 
Mrembo hiyo mutu iko vile nacheza sebene ndani ya kichwa yako acha pigia yeye sebene tapata jibu...
 
Fanya yako bibie huyo ni katili hiyo ni afya yako nenda kwa wazazi upate msaada.
 
Duu pole sana.umesema jamaa kwao ni arusha?atakua mtumiaji mzuri wa kitu cha arusha.
 
Nenda kwenu ukifika weka kila kitu wazi.inavyoonekana huyu hata akikuoa ni majangatu.
 
Huyo si mume wewe ni janga tu hilo!! Mfate ama urudi kwenu ! Isitoshe mwenzio keshaoa huyo huko! Loh!
 
Back
Top Bottom