DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 6,190
- 12,109
Nimepata kumfahamu Mwalimu huyu shujaa mwenye hulka yenye kusisimua. Toka anasoma shule ya msingi mpaka Sekondari alionyesha uwezo mkubwa sana darasani, mbali ya kuwa bright pia alikuwa na talanta ya uongozi.
Alipokuwa shule ya msingi alipata kuwa kaka mkuu toka darasa la tano kwa sababu ya weledi wake ndipo akapendwa sana na walimu pamoja na wanafunzi wenzake. Alikuwa na uwezo mkubwa katika masomo yake yote yaani masomo ya sayansi na yale ya sanaa. Kuna kipindi alipata kualikwa kwenye midahalo ya kiingereza(debate) kwenye shule ya jirani ya sekondari ingali bado akisoma primary st kayumba. Alijariwa uwezo mkubwa wa kujieleza pamoja na ushawishi.
Kidato cha kwanza alijiunga na moja ya shule maarufu sana za vipaji maalumu hapa Tanzania. Sekondari pia alijidhihirisha kwa uwezo mkubwa sana wa kimasomo darasani. Alikuwa kiongozi wa taaluma toka kidato cha pili mpaka kidato cha nne. Alikua ni active member kwenye clubs za kimasomo shuleni kwake. Alimaliza elimu yake ya kidato cha nne kwa ufaulu wa DIVISION ONE
Kidato cha tano amepata kusoma katika shule moja ya private maarufu sana Tanzania, shule iliyojijengea jina kwa kuwa king'ang'anizi kwenye top ten ya matokeo ya kidato cha tano kwa miaka kadhaa. Alipata kuwa kinara kwenye hizi programu za "young scientists" kama nimekosea jina, nitaomba nirekebishwe. Japokuwa alikuwa akisoma mchepuo wa sayansi lakini alipata kuiwakilisha shule ktk mshindano ya ESSAY WRITING na DEBATE COMPETITION ndani na nje ya nchi. Pia alikuwa ndiye Head Prefect wa shule. Alimaliza na ufaulu wa DIVISION ONE nzuri.
Alijiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam tawi la Main Campus akisomea shahada ya ualimu wa sayansi. Kwenye maisha yake UDSM alipata kuwa waziri wa mikopo, alipambania sana wanafunzi ili waweze kupata stahiki zao za mikopo. Wengi walimwona kama mwanaharakati na si kiongozi kwa alivyojiwekea heshima pale REVOLUTION SQUARE mahali pa harakati kwa wenyeji wa UDSM tawi la Main Campus. Alimaliza elimu ya chuo kikuu kwa heshima kubwa. Mpaka sasa ni mwajiriwa wa shule moja ya serikali jijini DSM.
TUNAPOSEMA KWA UJUMLA KWAMBA WALIMU NI WAOGA NA WALIOFELI SASA SIJUI HUYU MWALIMU TUNAMUWEKAJE KWENYE HILI KUNDI.