Huyu mwalimu ashitakiwe, adhabu hii kwa wanafunzi inadhalilisha utu wao

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,306
Ama kweli ndiyo maana watu wengi hawapeleki watoto wao shule za Kata moja ya sababu ni adhabu kami hii aliyoitoa mwalimu kwa wanafunzi hawa, piga hesabu ukute ni mtoto wako unamkuta anapewa adhabu hii utajisikiaje?



Mama Ndalichako tunakuomba angalia hizi adhabu siyo haki kabisa.
 
Juzi nilimsikia Rais akiwa anawahutubia huko Chato ilifika mahala akasema najiuliza kwa nini viboko viliyolewa mashuleni anasema wakati wake viboko viliwasaidia sana kuwa na utii na heshima...So adhabu ya viboko inaweza rudishwa tu tena maana ni kweli watoto wanazidi kupuputika kimaadili..
 
Kule Chato Magufuli alisema viboko virudi, vinaleta nidhamu na ndiyo maana yeye yuko hapo alipo.
 
Nimeiona hiyo video. Safi tu;

Sisi enzi hizo tulichapwa sana + other corporal punishments tena na wasichana walikula mboko za matako kabla ya baadae kuambiwa wachapwe mikononi.

Ukichapwa shule, mzazi akijua anakuongezea. Nilikuwa nasoma na wadogo zangu wa kike shule moja, siku nikichapwa shule nawanunulia barafu + chipsi dume ili wasiseme home nisije nikaongezewa.

Kama hutaki mwanao achapwe, mlee vyema ili atii sheria za shule. Wazazi wa leo wanaongoza kuwaharibu watoto wao kwa kuwapa malezi mfu. Wanavipa vitoto kiburi cha kujibizana na walimu.

Nimesikia huyo teacher akiwachapa kwa sababu walitoroka shule. Hilo ni kosa kubwa kwa sababu ameenda shule kusoma. Sidhani kama watachapwa bila makosa.

Hiki kizazi ni tatizo zaidi. Bora hata sisi tulikua hata TV hakuna...!

Naunga mkono hoja; Fimbo ziwepo.
 
Ama kweli ndiyo maana watu wengi hawapeleki watoto wao shule za Kata moja ya sababu ni adhabu kami hii aliyoitoa mwalimu kwa wanafunzi hawa, piga hesabu ukute ni mtoto wako unamkuta anapewa adhabu hii utajisikiaje?


Mama Ndalichako tunakuomba angalia hizi adhabu siyo haki kabisa.


Nihakikishie ni bongo na wapi then tuchukue hatua !!
Huu ni uharamia
 
Mwalimu yupo sahihi kabisa kwa sababu enzi zetu zilitusaidia sana kutuongezea uoga na nidhamu wa walimu na walezi wengine.Ila wanafunzi wa kizazi hiki hawana nidhamu hata kwa wakubwa wengine.Yaani hasa hawa wanafunzi wanaosoma shule za kati kati ya mji wa Dar es salaam wana matusi sana kuna siku walimtukana mama wa watu ndani ya daladala kisa tu alimwambia mmoja wao asimame vizuri.Eti wakamjibu kama unataka starehe kapande Tax halafu ukiangalia huyo mama ni umri wa mama yao au zaidi yake.
 
Ama kweli ndiyo maana watu wengi hawapeleki watoto wao shule za Kata moja ya sababu ni adhabu kami hii aliyoitoa mwalimu kwa wanafunzi hawa, piga hesabu ukute ni mtoto wako unamkuta anapewa adhabu hii utajisikiaje?


Mama Ndalichako tunakuomba angalia hizi adhabu siyo haki kabisa.

Jamani serikali ipo wapi? Adhabu kali kama hii ni kosa gani wamefanya hawa wanafunzi? Waziri husika upo wapi? Ndalichako fuatilia kabla hatujachukua hatua raia.
 
Mimi mwalimu hawa watoto wa siku hizi ovyo sana, ukiwachekea tu imekula Kwako. Shule ninayofundisha, mtihani wa midterm ya pasaka mwalimu mwishoni mwa paper kaandika pasaka njema, mwanafunzi kamjibu poa Pendo (Pendo ni Jina la kwanza la mwalimu) sio jina halisi. Mwingine kamjibu haina haja teacher. Mwanafunzi Mwingine aliandika nyimbo tena ya matusi mtihani wa hesabu form four midterm. Sasa ucheke tu na mwanafunzi kama hawa utakuwa unawajenga au unawasaidia. Chapa fimbo 15 kwa kila mmoja. Sijawahi chapa fimbo chini yatano kwa kosa.
 
Tatizo Siku hizi watu wana frustration kibao zinazotokana na ugumu wa maisha na mambo mengine. Sasa waalimu wakiruhusiwa kutumia viboko hizo stress zao zote watataka kuzimalizia kwa watoto shuleni hata kwa makosa madogo tu.

Sipendi kumkumbuka yule mwalimu aliyenichapa zaidi ya viboko 35 kisa kikiwa ni kukosa namba baada ya kuchelewa assembly dakika chache na kukuta wenzangu wameshahesabiwa.
 
Nilipanda daladala nimekaa binti aliyesimama akaniegemea kumwambia akazidisha nikamtazama sikusema tena yakaanza kumtoka kwa lugha ya Malkia akinisema na kunibeza mwenzie alistuka hakujibu, mimi nimenyaza kimya wakati nateremka nikamuuliza binti umemaliza nataka kutemka au bado nishuke kituo cha pili,? Hii ndio mitoto ya.com ambayo hata walimu wanaogopa kuwapiga
 
Ifike mahali tujifunze jambo, tusiweke pamba masikioni.

Kuwachapa Watoto viboko kama unauwa nyoka haisaidii jamii kwani wanakuwa waoga mpaka maisha yao ya baadae.

Beating children can cause trauma, children needs discipline, not punishment.

Ni jukumu la mzazi kumfundisha tabia nzuri mtoto na sio mwalimu.

Mzazi ndio anaemjua mwanao alivyo kwani wengine wana matatizo kiakili na kuwa watundu kupitiliza na mwalimu anapiga tu, wengine wanakuja na njaa na matokeo yake kulala darasani ambapo mwalimu bila kujiuliza huyo mtoto kwanini alale anaamua kupiga tu.

Wengine wazazi wao ni walevi akirudi kalewa ni fujo usiku mzima na kuanza kumpiga mama na huku mtoto akishuhudia.
 
Back
Top Bottom