Huyu msichana vipi?

Huyu msichana vipi?

quantumQ

Senior Member
Joined
Dec 11, 2013
Posts
111
Reaction score
84
Ni waiter katika restaurant moja hivi, nilikuwa napenda kwenda pale kupata breakfast kila siku za kazi yaani Jumatatu hadi Ijumaa

Kiukweli tangu mara ya kwanza nilipoenda pale nilikuwa nimevutiwa naye.

Katika kwenda kila siku nikawa nimeshamfahamu jina lake na yeye akalifahamu langu na pia tukabadilishana namba. Kwenye simu story zikaendelea zaidi na kufahamiana zaidi.

Sa issue inakuja nimewahi kumkaribisha kwangu mara nyingi tu aje kunitembelea ila sababu zinakuwa nyingi za kutokuja. Pia kipindi cha mwisho mwisho mawasiliano yakawa sio mazuri maana sms inajibiwa baada ya siku mbili au tatu.

Mwisho wa siku nikaamua kuendelea na mishe zangu na sasa hivi nipo busy sana na madili yangu ya hela hata pale restaurant sipati muda wa kwenda.

Kama wiki iliyopita gari yangu ya kwanza ilifika maana niliagiza ili niwe na usafiri wa kufanya mishe zangu, siku moja nipo town nimetoka bank nikakutana nae nikamsalimia tu kawaida basi sikutaka hata kuanza kumuuliza sijui nini..

Nikamuuliza anaelekea wapi akasema kazini kwake basi nikamwambia twende, nikampeleka then nikaenda zangu ofisini.

Kuanzia siku hiyo jioni ananitafuta sana kuniuliza lini nipo free aje kunitembelea kwangu.

Of course mishe zangu zinaniweka busy sana unakuta kwangu nikiondoka saa moja asubuhi narudi saa nne usiku, na kipindi hicho namuomba tuonane nilikuwa nipo tayari ku sacrifice hata masaa mawili nionane naye ila ndio hivyo akawa amezingua..

Je, mnanishauri vipi wakuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom