Huyu msichana mimi simuelewi

Mhdiwani

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
650
712
Habari zenu ndugu zangu bila shaka mko poa,,
kuna jambo linanisumbua naombeni ushauri wenu kabla sjafanya chochote ,,,ni hivi
kuna binti mmoja nilikua nae kwenye mahusiano kwa muda kidogo ,,nilipanga kumuoa kabisa baadhi ya ndugu zake wanalifahamu hilo
tar 12/2 mwaka huu alipigia simu na kuniomba pesa kidogo anashida nayo pesa ni 200,000 ,,
nikamjibu sina pesa kwa siku hio labda kesho njoo home uchukue,, hakujibu akakata simu
sikua na presha yoyote nilijua kachukia kwa muda tu,,
tangu hapo nikimpigia cm hapokei nikimtumia sms hajibu,,
ilipofika 14/2/ valentine day ,,alitumia siku hio kufanya jambo,, nikiwa nimerudi kwenye shughuli zangu nipo ndani nimepumzika ,,nkaskia mlango unagongwa nikaamka kufika nakutana na mtoto wa jirani wa kiume ameniletea bahasha akaniambia nimepewa kule nikuletee wewe nkasema sawa .
skujua ninani kamtuma yule mtoto ,
Nikafungua na kuanza kusoma
hakika ilikua siku mbaya sana kwangu kwakifupi aliniambia Mimi na yeye basi na tayari anabwana mwingine ,,kibaya zaidi akanitajia na jina la jamaa ambae namfaham,,
basi niliumia sana na mbaya zaidi nilikua nikiwaona wakiwa pamoja nyakati za jioni nikirudi job,
hapo nilimkumbuka mungu wangu niliumia sana lkn ninapokutana nao nawasalimia kwa furaha mpaka wanashangaa
tangu tar moja mwezi huu nimebadilisha njia staki kuumia bure,
lkn wiki iliopita kanipigia cm sijapokea akatulia
kanitumia sms kunisalimu nikamjibu akatulia,,
sasa Jana kanipigia cm kwa namba nyengine akaniambia kuna kitu anataka kuniambia kesho nikamuuliza kitu gani akasema nitakuambia tukionana ,,,jioni ya Leo narudi job nakuta ujumbe kua amekuja kuniulizia
sasa wadau nimfanyaje huyu dem Mimi ninahasira nae yeye hajui tu ,,,nikimtazama nakumbuka upuuzi alionifanyia inauma sana
Nishaurini wadau nimkwepe vp huyu kwasababu nikionnana nae naweza kufanya jambo la ajabu nikapata matatizo
 
Huu ndo uwanuaume ninaoutaka mm kila Siku,kukaa kimya nalo ni jib chief,kufanya vimbweka vyote ili akuone unatetereka but umekaza ukayachukua maumiv yako na kuyaweka mfukon,Bravo's You,we kakikutafta tenha we kasikilize tu then hata usionyeshe chochote,hakuna kitu kinatesa MTU akupigie kimya,mana hapo anajiuliza maswal bila majib
 
Pole mkuu! Wadada sisi!!!!
Kama hutaji kuwaona kabisa, ukiwa na unauwezo wa kuhama sehemu hiyo ningekushauri uhame ila kama huna uwezo huo basi komaa na msimamo wako. Usimpe time ya kujieleza na wala usimjibu msg. Usibadilishe njia, jifunze kuwapotezea.
 
Ma-X wangu wote huwa wanasema mi Nina roho ya kigaidi, sababu mi demu akinizingua nafuta mawasiliano yote na huwa napiga kimya mazima ila nikikutana nao Hi nawapa, washalia wee mi nawacheki tu. Huyo demu we piga kimya kabisa endelea na mishe zako. Watoto wazuri wako wengi sana nowdays.
 
Mimba ya kulazimishwa inakaribia. Usimruhusu kuingia naye sehemu ya faragha, mkaribishe kama rafiki wa kawaida na ongea nae kikawaida tu halafu mtakie heri kwenye mahusiano mapya. Hakuna sababu ya kununa!!
 
Samahan kama wewe ulieish nae kwa kipind fulan humuelew sie wana JF tusiojua hata anafananaje tutamuelewa kwel?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom