Huyu mpangaji mwenzangu ananitafuta nini?

BradFord93

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
910
2,165
Ni mdada ambaye ana mume wake but tunajuana mda tuu. Alipata tatizo alipokuwa anakaa akahitaji kuhama na akataka msaada wangu kupata chumba

Mahali nilipopanga mimi kulikuwa na nafasi ila hua sipendi kukaa na mtu tunayejuana jirani, nikamkatalia. Akaongea na ndugu zangu akawaeleza knachomhamisha. Wakaja kunielekeza hali halisi ya anayopitia

Nikamkubalia kwa masharti kuwa maisha yake hayatanihusu na maisha yangu hayamhusu, salam saawa ila hakuna taarfa yyte kuvuja. Mambo yangu ayaache kama yalivyo nikaongea na landlord akakubali mtu ahamie

Saasa naona ameanza kukiuka tuliyokubaliana. Anaongelea mambo yangu. Vitu vyangu nkiacha nje anatumia. Unafki wa chini chini

Natamani kuhama lkn kwa mazingira ya hapa ni mazuri na sidhan kama ntapata sehem nyingne

Naomba ushauri mtu kama huyu unamfanyaje yaani?
 
Nyumba za kupanga tabu sana. Mkuu dunduliza ujenge kwako na uzungushe ukuta wa maana.... uishi unavyotaka.
 
Tafuta chura ndani na kitambaa chekundu.Hakikish chura hajafa tafuta naa kitambaa cheusi na mkaa ndani take Fung weka mlangoni mbona atahama kesho
 
Mkumbushe mliyokubaliana kwa mifano wa hayo anayoyaongea, pengine hakuwa na picha halisi ya nini ulichomaanisha.
 
Akishindwa kumkalisha chini amtumie hata ujumbe mfupi wa sms.
Kwa sms sidhan kma ujumbe utaenda serious...nahitaji face to face...!!natafuta mda akiwa peke yake...maana ht makubaliano tuliyafanya peke yetu
 
Back
Top Bottom