Huyu Mfugaji anatoa wapi jeuri hii?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,606
2,000
Nimekuwa nafuatilia ugomvi wa wakulima na wafugaji kwa muda mrefu nimegundua yafuatayo;
1. Wafugaji vinara wa kupiga wakulima ni wamasai wa manyara ambao wanaranda randa kati ya Tanga Morogoro na Lindi, huo ugomvi wao wala hawaufanyii Manyara Kilimanjaro wala Arusha.

2. Kila wanapogombana ITV wapo na wanachukua tukio live, sasa huwa wanataarifiwa au wanamawakala wanaozunguka na hao wafugaji?

3. Ni masai yule yule anayeshambulia watu na baada ya ugomvi lazima ahojiwe na ITV sasa sijui huwa anawaandaa kabisa ITV au ni coincidence tu!

4. Sura zilezile za wamasai ndio zinagombana na wakulima kuanzia morogoro Lindi Pwani Handeni sasa najiuliza ni special project au ni kundi hilohilo likienda huku linafukuzwa linahamia sehemu nyingine?

Hebu vyombo vya usalama mfuatilieni huyu Mmasai anayehamahama na ng'ombe huku akifuatwa na camera za ITV kwa nyumba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom