Tandu huyo ni hatari sanaHabari wakuu,
Hapa nnapo ishi nimekutana na hawa wadudu mmoja ni mkubwa balaa na mwingine ni mdogo kama uyuView attachment 696000 sasa nauliza hawa wadudu wanaitwaje je wanauma na akikuuma dawa yake ni nini na njia ya kuwazuia ni ipi.Nimewakuta wawili wapo karibu na shimo la maji machafu wanakula mende.
Kuna mwenzao mmoja aliwahi kuuwa kicheche.... Basi akakuja humu jf na boonge la heading eti "Wana jamvi, leo nimepambana kiume na mpambano haukua wa nchi hii" alafu mwisho akaweka na picha ya marehem....Hahahahaaaaa,,,,,,,,,heshima kwako mkuu
angeua nyoka si ndo angeenda tangaza tbc ukweli na uhakikaKuna mwenzao mmoja aliwahi kuuwa kicheche.... Basi akakuja humu jf na boonge la heading eti "Wana jamvi, leo nimepambana kiume na mpambano haukua wa nchi hii" alafu mwisho akaweka na picha ya marehem....
Sasa huduma ya kwanza ukiumwa unafanyaje au ni kama kwenye nyoka tuMtoto wangu ali umwa na huyo mdudu kisha kambeba kaja nae hahaha ilikua shughuli maana alikua bado hajaanza kuongea vzr baada ya mda kidogo joto lake la mwili lilipanda sana kiasi tuliingiwa uoga sana, shida ikawa hosp za kiTz hawajui dharula kabisa ya mtu anae umwa magonjwa ya kawaida na alie umwa na mdudu ama kupata ajali wakataka tukae foleni tuliyo ikuta na foleni kwenye hosp za watoto zilivyo mh! Mtoto hali ili change kabsaaa sikuamini kama mdudu huyo akiamua kufanya yake anaweza kubadili hali ya hewa, mwisho alipata matibabu na hata ivyo tuliambiwa anabahati alie mng'ata alikua mdogo hivyo sumu si kubwa sana mana alikua kama ana rangi ya kijani kidogo, kwa madai ya dr anasema wale wekundu na wengine wanakua kama wana mbawa mbili mwishoni mwa mikia yao ndio noma zaidi
Kwa kifupi sio mdudu rafiki sana huyo kama nnge