Habari zenu?
Kila napoangalia wanawake wengine wanapendwa na waume zao roho huwa inaniuma sana ,sio kwasababu naona wivu ila kwasababu nawaza kwanini isiwe mimi.
Nimeolewa mwaka wa kumi na moja huu sasa tuna watoto watatu .mume wangu ana kimada nje ambae amezaa nae na ndio anaemthamini zaidi yangu na wanawe.kuna wakati hawalipii watoto ada ya shule hadi wanarudishwa nyumbani, mwaka jana mtoto wetu wa mwisho ndio alizaliwa pale katika hospitali ya tmj,mikocheni.nilijifungua kwa operesheni na nilikaa hospitali siki 3 bila mume wangu kufika hospitali na nikawa nashindwa kurudi nyumbani kwasababu sikuwa na pesa ya kulipia kila akipigiwa simu hapokei,mpaka siku ya tano ndio alinifata na kunipeleka nyumbani.
Ni visa vingi na mateso mengi nimeyapata kwa huyu baba.huwa anatuacha nyumbani hata wiki nne bila pesa ya chakula inabidi niende kuomba chakula kwa majirani,akirudi nikimuuliza ananipiga sana mpaka kuna siku alinivunja taya.sijui nifanye nini,sina pa kwenda,sina pa kuwapeleka wanangu.nifanye nini?je kuna sehemu yoyote nayoweza kwenda nikapata msaada

uslilie F.L utakuja kuliza jukwaa zima hapa...hata mimi hapa machozi yananitoka...oooh jamani hii habari imeniumiza sana moyoni..machozi yamenitoka
kwanini mnakuwa hivi jamani? Mbona hamtuhurumii ?
Tunajua mnayafanya huko nje ..naona huyu kavuka mipaka natamani nimfate nikamtafune mzima kwani huyu dada hana ndugu jamaa na marafiki wanaoweza kumpa msaada wa karibu haya ni mateso .
siku yangu imevurugika kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.naomba mungu unisaidie usinipokonye kipato changu hiki kidogo kinachonisaidia kujikimu maisha ....
oooh eeeh kumbe ni hivi???????
uslilie F.L utakuja kiuliza jukwaa zima hapa...hata mimi hapa machozi yananitoka...
daaaah mi nahuzunika sana kwa nini jamni inakua hivi wababa kwa nini hamna huruma....jana nusu jirani yetu afekule mtaani mume wake ameoa anapitisha miezi haji home mama wa watu anauza mkaa apate hela ya kula na wanae sita yule baba amewaacha akija hapo home ni matusi kwenda mbele mtu mbaba mzima miaka 60 halafu BOSI WA DOWUTA BANDARI....Inatia kinyaa..hela mpaka akatwe kwenye mshahara kutoka oFisini ndo ipelekwe home daaah wanaume mnatutisha sisi ambao bado hatujaolewa jamani itakueje...huyu jirani yetu jan apresha nusu afe.....dada pole sana mungu akusaidie NENDA TAMWA WAMKOMESHE HUYO MBABA ASO HAYA....yani na hasira kama ntukane...lakini naheshimu kijiwe....ila kina baba mmezidi jamani....MBONA ZAFANANA TU KWANINI HAMTULIII.....
Wanaume mbona hamchangii jamani hii topic!! Mkimaliza kusoma tu..mnakula kona..kwa nini???
Mhh Fidel!Duhh kuna mianaume mingine mikatili kweli sijui kalishwa libwata!!
Mhh Fidel!
Kulishwa limbwata siyo hoja..!