Huyu MC wa Mei Mosi ni timamu?

Huyu MC wa Mei Mosi ni timamu?

mkuu cyo hilo tu alisema eti wakati wimbo wataifa unaimbwa watu watulie kama wanafanyiwa tohara/jando
 
"mbona mnatembea mmenuna mbele ya mgeni rasmi, embu chekeni basi"
 
Haya ni maneno aliyoanza nayo rais Kikwete kabla ya hotuba yake ya Mei Mosi. Sijayapenda kwasababu Tanzania tunasifika ndani na nje ya nchi yetu kwa uchawi. Hapa rais kwa mtizamo wangu, alianza kusujudu uchawi kama sio wachawi.

Si mara yake ya kwanza,kuna sherehe kama hizi za mei mosi ilikuwa Morogoro alipoona dalili ya wingu akaomba miungu ya milima ile ya Uluguru isilete mvua,tena alitaja na jina ila sikumbuki,wenyeji wanaweza kuifahamu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
...nilimsikiliza kwa makini sana nikacheka sana,na jinsi alivyokuwa akiyasoma mabango nikajua ni mtu wa aina gani huyu mc...
 
Nipo hapa naangalia sherehe za Mei mosi lakini nashindwa kuelewa huyu mshereheshaji ana matatizo ya kufikiri au ndio kujipendekeza kwa mkuu mpaka anaongea kauli zisizopendeza? Kwanza nilimsikia anawakemea watu kuwa "Tulieni kama mnafanyiwa tohara" nikadhani amepitiwa tu lakini amerudia tena kwa kumwambia mgeni rasmi kuwa "usiwe na wasiwasi hii mvua haitonyesha nina uwezo wa kuizuia" hapa amenishangaza sana, ina maana yeye ni Mungu au ni bingwa wa ushirikina? Sifa nyingine sio nzuri kuzitafuta kwenye halaiki kama hii.

Huyo MC amesema Mkoa wa Mbeya unasifika sana kwa ukarimu wao wa kupokea vizuri wageni wa Kitaifa; najiuliza sijuhi ni Mkoa gani hapa Tanzania unaolalamikiwa kwa kutopokea vizuri wageni wa Kitaifa!
 
anasema uwanja wa ndege songwe inaweza kutua ndege ya obama 747 bila shida, pia anawashauri wachangamkie kilimo cha maua tuwashinde kenya. Kima cha chini cha mishahara ameahidi kitaongezwa kwa kiasi kikubwa kidogo ila hakuta wahusika wataona ongezeko mwezi julai.

hivi ule mpango wa kuita uwanja wa songwe kwa jina la jk umeishia wapi?
 
CCM wanahujumiwa/wanahujumiana kwa mbinu mbalimbali ! MC ni muhujumu pia
 
Kavaa nguo za rangi gani huyo jamaa Msema Chochote!Atakua ni mbunge tarajali!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


lazima zilikuwa za kijani kama mkongo wetu lusinde mtu wa Iringa.
 
Haya ni maneno aliyoanza nayo rais Kikwete kabla ya hotuba yake ya Mei Mosi. Sijayapenda kwasababu Tanzania tunasifika ndani na nje ya nchi yetu kwa uchawi. Hapa rais kwa mtizamo wangu, alianza kusujudu uchawi kama sio wachawi.

Aliyeongea maneno hayo kwa kadiri ya mwanzishaji wa thread hii siyo Rais ni MC. We umeidaka bila kutafakari na inawezekana haupo nchini wewe.
 
Hata mimi sikufurahishwa na mfano ule. Lakini la kushangaza rais alionekana kuufurahia mfano ule na alicheka sana! Mawazo ya MC yule ni kuwa kila mwanaume amefanyiwa tohara za kienyeji zisizo na ganzi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom