Huyu mama ananifanyia fitna nimfanyaje?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Salamaa wana MMU

Kama mada inavyojieleza

Nipo Mkoani huku nafanya kazi,sasa naishi chumba cha rafiki angu ambaye sasa tumekua kama ndugu

Huyu Jamaa kaoa na yupo Daslama huko na nke wake ,hivyo chumba chake mi ndo naishi

Hapa home kuna ndugu(sio wa damu) na huyu rafiki angu ambaye ameoa na ana binti kama wa miaka 17-19 hivi anasoma,kiukweli tangu nije hapa nlipewa taarifa kuhusu tabia za huyu mama so nikamfahamu kinaga ubaga

Mwezi uliopita nlipata msichana akawa mpenzi wangu so akaanza utaratibu wa kunitembelea pale ghetto Mara kwa Mara ,yule mother alikua anamwona ,Mimi niliona ni jambo la kawaida kumpeleka pale home coz kila mtu anaishi kwenye chumba chake,hii nyumba ni ya ndugu wa mume wa Huyo mmama

Sasa hivi majuzi nikasafiri baada ya kurudi nikakutana kuna matatizo kidogo huduma ya maji imesitishwa so nikampigia yule Jamaa angu kumweleza tukaongea vizuri,ila mwisho akaniambia amepigiwa simu na yule mother analalamika eti Mimi naingiza demu pale home ambaye ni rika la mwanae so haileti picha nzuri

Jamaa nae akaniambia oooh huyo mother mswahili sana Mara hapo home sie wote tumekaribishwa lakini Huyo mama na bwanake wana sauti sana kwa mmiliki wa nyumba so anaweza akanifukuza akisikia nimemwacha mtu halafu analeta msichana,mi nikamjibu poa ntasitisha kuleta huyo msichana

Sasa hapa nawaza nifanyaje je nimfuate yule mother nimchane aache kufuatilia life langu na kutaka kunikosanisha na rafiki angu au nimpuuze tu? Manake huyo binti anamwona ndio anaingia ndani siku moja moja lakini kitendo cha kupiga simu na kuwatangazia baadhi ya ndugu wa mmiliki wa ile nyumba hadi kasababisha rafiki angu akoromewe naona si cha kiuungwana ,Je nimfuate nimchane aache ukuda na fitna au nimpotezee??
 
Sijawahi kufurahia mawasiliano na mama mtoto wangu
Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sigara Kali, Jul 2, 2017.

Watch Thread

  1. Sigara Kali JF-Expert Member
    #1
    Jul 2, 2017

    Joined:May 28, 2017
    Messages:1,414
    Likes Received:2,816
    Trophy Points:280
    Habari wakuu
    Husika na mada tajwa hapo juu
    ni mwaka wa 4 Sasa nipo nae ,tulikutana wakati nasoma chuo kikuu flani hapa TZ
    Nakumbuka mara ya Kwanza nlikutana nae barabarani nkamwomba namba akanipa
    Kama kawaida yetu wanaume atulembi nkamtia vocal binti kajaa
    Tukaingia katika mahusiano maisha yakaendelea.
    Siku za mwanzo za mahusiano yetu binti alikua na juhudi Sana ya kupiga cm na kuchat na mm mawasiliano yakawa mazuri ya kupendeza
    Baada ya muda binti akaenda mbali na mm mawasiliano yakaendelea ,wakati flani akapata kazi mjini kwa Bashite tukawa karibu tena
    Ikafika kupindi binti nikampa ujauzito kazi ikamshinda nkamwambia usijali njoo nikusaidie kulea mimba nkaishi nae kwa amani upendo na furaha
    Mtoto akazaliwa baada ya miezi kadhaa mama mtoto akapata kazi yenye salary nzuri
    Nkauza baadhi ya vitu nkampa hela akaenda mkoani kuanza kazi
    Nligraduate degree yangu salama salmin nkasema niende kwa mama mtoto tukaishi vzr but baada ya muda mawasiliano yakawa nji shida
    Mimi ndo nkageuka mpigaji cm mtumaji msg
    Sometimes simu inapigwa haipokelewe
    Naishi mbali nae nimejaribu kumwelekeza juu ya umuhimu wa mawasiliano mazuri baina yetu lakini Bado tatizo linaendelea
    Nsipopiga cm wala kutuma text nae anakaa kimya
    Na akipiga anaanza kulaumu sijapiga cm kumjulia Hali mtoto kwa maana uwepo wa Mtoto ndo niwe mtumwa
    Sifurahi kabisa mtindo wa mawasiliano yetu
    Imefikia hatua michepuko ndo inanipa furaha kuliko mwandani wangu
    NB: Mimi sina hela wala kazi ya maana ya kuingiza kipato napiga mishe mishe tu za mjini nna kiwango kikubwa cha elimu Ila Bado Mambo hayajanikalia poa naendelea kupambana nijenge heshima
    Mama mtoto wangu ni mwajiriwa kanizidi kipato
    Nimeamini wanawake ndo chanzo cha kuvurugika kwa mahusiano na ndoa mwanamke akijua unampenda anataka akutawale,mwanamke akiona huna pesa heshima inashuka Hana muda na wewe,wanawake chonde chonde mtuheshimu na kutujali waume zenu hata kama hatuna pesa wala kazi za maana .

    Report
    Like - 3 people likes + Quote Reply
 
Kabla hujamchana aache kufuatilia maisha yako, hakikisha umeshapata kodi ya kupanga chumba sehemu nyingine!
 
Kama unafanya kazi kwanini uishi kwa mtu na usitafute nyumba ukapanga??? Hata pangekuwa kwangu ngekuzingua, nyumba nayolala na mke/mume wangu ndo ukaribishe na wapenzi wako??? We mwenyewe hauna aibu wala adabu
 
Mkuu ndo nafanya utaratibu mwezi huu nipange room,sina miezi mingi tangu nianze kazi hapa ninapoishi ni temporary tu
 
Kabla hujamchana aache kufuatilia maisha yako, hakikisha umeshapata kodi ya kupanga chumba sehemu nyingine!
Kwanza jamaa ata akili hatumii, nyumba kakaribishwa, na km ni kwa mtu it means ata kitanda ajanunua, anaendaje kumchana uyo mama ata km hayamhusu????
 
Mkuu ndo nafanya utaratibu mwezi huu nipange room,sina miezi mingi tangu nianze kazi hapa ninapoishi ni temporary tu
Ungevumilia mkaenda kukutana uko ulikopanga sasa na ulichofanya kaa ukijua si cha kingwana
 
Ungekua muugwana ungeanza kwanza na binti wa Huyo mama alafu ukamalizia na yeye ikibidi. Alafu unahama hiyo sehemu maana watakua wanakutamani uendeleee kuishi hapo.
 
Nilichokiona tu ni kwamba Wewe, Rafiki yako na huyo Mama wote kwa ujumla wenu ni ' hamnazo ' kabisa. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
We nae si upange kwako??? yaan ukaribishwe badala uwe na adabu unaanza kuleta wanawake chumba cha mtu??
 
Sio picha nzuri ndio,,,hapo kuna binti,,anaona hujaoa unaleta mwanamke, unafikiri anajifunza nini?? Mama yuko sawa kimaadili. Kama ukimhitaji nendeni huko lodge,, kwanza we Mwenyewe ukijiongeza unaona ni heshima kweli??
 
Salamaa wana MMU

Kama mada inavyojieleza

Nipo Mkoani huku nafanya kazi,sasa naishi chumba cha rafiki angu ambaye sasa tumekua kama ndugu

Huyu Jamaa kaoa na yupo Daslama huko na nke wake ,hivyo chumba chake mi ndo naishi

Hapa home kuna ndugu(sio wa damu) na huyu rafiki angu ambaye ameoa na ana binti kama wa miaka 17-19 hivi anasoma,kiukweli tangu nije hapa nlipewa taarifa kuhusu tabia za huyu mama so nikamfahamu kinaga ubaga

Mwezi uliopita nlipata msichana akawa mpenzi wangu so akaanza utaratibu wa kunitembelea pale ghetto Mara kwa Mara ,yule mother alikua anamwona ,Mimi niliona ni jambo la kawaida kumpeleka pale home coz kila mtu anaishi kwenye chumba chake,hii nyumba ni ya ndugu wa mume wa Huyo mmama

Sasa hivi majuzi nikasafiri baada ya kurudi nikakutana kuna matatizo kidogo huduma ya maji imesitishwa so nikampigia yule Jamaa angu kumweleza tukaongea vizuri,ila mwisho akaniambia amepigiwa simu na yule mother analalamika eti Mimi naingiza demu pale home ambaye ni rika la mwanae so haileti picha nzuri

Jamaa nae akaniambia oooh huyo mother mswahili sana Mara hapo home sie wote tumekaribishwa lakini Huyo mama na bwanake wana sauti sana kwa mmiliki wa nyumba so anaweza akanifukuza akisikia nimemwacha mtu halafu analeta msichana,mi nikamjibu poa ntasitisha kuleta huyo msichana

Sasa hapa nawaza nifanyaje je nimfuate yule mother nimchane aache kufuatilia life langu na kutaka kunikosanisha na rafiki angu au nimpuuze tu? Manake huyo binti anamwona ndio anaingia ndani siku moja moja lakini kitendo cha kupiga simu na kuwatangazia baadhi ya ndugu wa mmiliki wa ile nyumba hadi kasababisha rafiki angu akoromewe naona si cha kiuungwana ,Je nimfuate nimchane aache ukuda na fitna au nimpotezee??
Ndugu, unafanya jazi, ni vyema ukatafuta nyumba yenye mazingira rafiki kulingana na hitaji lako.
 
Back
Top Bottom