Huyu dada amekwama wapi au ndio anataka kuniibia?

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Habarini wanajamvi.

Ishu ipo hivi, kuna mdada mrembo. Nilitana nae mara kadhaa sehemu flani hivi last year mwezi wa 7 tukazoeana kimtindo.

Katika mazoea hayo, day moja baada ya kupiga zangu gambe akaja hapo Bar, tukajumuika mwisho tukaishia kuzoana na kwenda kumaliza shida zetu.

Huyu binti baada ya siku hiyo sikuwahi kuonana nae tena na sina kumbukumbu kwamba katika mazoea yangu mimi na yeye kama nlishawahi kumpa namba zangu.

Juzi ananitext kwamba ana mimba yangu ya miezi nane na yupo mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini na anatarajia kujifungua mwezi ujao.

Nimemuuliza maswali kadhaa anaonekana anajikanyaga kanyaga na mimi simkumbuki kabisa licha ya kunitajia jina lake. Nimemuomba anitumie picha anadai yupo kijijini sana na hakuna WhtasApp.

Nimeenda bar nilipotana naye mara hizo kadhaa kuulizia kwa mdada wa kaunta na meneja wote wanasema hakuna mfanyakazi aliyetumia jina hilo (alilonitajia kwamba ndio jina lake).

Swali langu inawezekanaje mtu ana namba yanga all this time asinitafute siku zote hadi "mimba" ifikie umri huu ndio anitafuta?? Nikimuuliza hana majibu zaidi ya kuniambia atanibwagia mtoto.

Mi nshahama mkoa tuliokutana japo hajui hilo.

Huyu bibie sio kwamba anataka kunipiga hela, maana ameniomba hela za kujifungulia nikimbipigia simu anadai mike ya simu yake mbovu.

Ushauri wenu wadau. Sio nataka kuingizwa chaka hapa??
 
Back
Top Bottom