Huyu binti anataka nizae nae mtoto

Huyu binti anataka nizae nae mtoto

Habari wadau..
Nimeona niweke hapa labda kuna mwenye uzoefu na hawa mabinti basi atatoa maoni yake.
Huyu Binti nilikutana nae kupitia binamu yake, kweli alikuwa ni mzuri hasa na rangi yake ya kahawia basi ilimfanya aonekane mrembo zaidi bila hata kufanya makeup na umbo lake zuri wanaliita na nane..
Nilijitahidi kupata namba zake na ndipo nikaanza kumfuatilia kwa karibu na kuanzisha kaurafiki lakini nahisi alikuwa na mahusiano na aliniambia yeye ni mke wa mtu nisimtumie text mida ya usiku basi nikawa muelewa nikatulia nikaona sio riziki...
Baada ya miezi kama sita kupita nikapita kwenye chart history zangu nikaona charting nikaona ngoja nimsalimu na hapo tukaanza urafiki na yeye akiwa kwenye mood hasa na mda huo nilikuwa nimepata kiajira mahali na ukizingati mshahara ni mzuri kwa kweli na kulingana naka Bsc kangu nikawa nimetendewa haki.
Siku zikaenda lakini nikawa sichat mchana maana nakuwa kazini ila usiku tunachat na Bnt akaanza kunitreat like ni mm ni Mpenzi wake lkn ikumbukwe hapo hakujua kuwa alishanizingua....Nikawa kinifanya shopping ya vitu vya ndani basi namuuliza maana alikuwa mtu wa karibu kwangu.
Baada ya wiki mbili Binti akaniambia ananipenda, Nilishtuka sana ila nikajikaza maana nilishindwa nimjibu nn kwa dkk kama tano nikamuambia Ahsante Nakupenda pia...ila nkamuambia ni urafiki wa kaka na dada
Basi Bnt ndio ikaanza kuitana Hubby mara Mpenzi mara Baba fulani...Siku zikaenda akaanza sasa kuniambia nataka nipate mimba yako but nikamuambia kwa sasa itakuwa ngumu isitoshe ndio naanza maisha na nina malengo mengi ukizingatia mm familia duni...akasema nakuja unipe mimba then narudi kwetu so sitakusumbua.
Ikumbukwe mda huo nina Girlfrnd tayari mbali na huyu na ni Bnt anayejiheshimu japo kwa muonekano niwa kawaida.
Nafsi ikawa inanituma kweli sijtembea na Bnt mrembo kama huyu ktk historia yangu lkn pia nikitembea nae ntakuwa nimemkosea yule Girlfrnd wangu tena bado Bikira na amejitoa kuwa wangu...Basi nikamueleza kuwa mm nina mchumba, kweli alipata shida akaniambia tuachane basi tukaagana ila baadae aksema hawezi kuniacha huku akiwa analia kwa uchungu na yuko tayari kushare penzi na huyu Bi dada mchumba wangu so nizae nae then niwe nawajali wote..
Jaman hii imekaaje maana mpk now huyu mrembo kila nikiongea nae ni yeye kutaka mimba yangu wala hanitoi upepo kivile hela anazoomba niza vocha tena 500 akizidiwa sana ni hela ya kusuka ambayo huwa nampa hata mda mwingne bila kuniomba....nilimuuliza kwa nn unipende na uamue kudate na mm akasema namjali sana so anashindwa kujizuia.
mpe hiyo mimba halafu uone jinsi gani huo mshahara wako ni mdogo mno. Kutokuwepo kwa vizinga sasa hivi anawekeza baada ya kitumbo kuingia.

Utarudi hapa hapa kuja kulia lia tena. Tatizo la watoto wa siku hizi wakiwa na shida wanakula na wa kwao wakizipata tu wanawapelekea wakina dada. Ushasema umetoka familia duni basi lipa fadhila kwa familia kwa kukupatia hiyo Bsc. Kuwa na mademu wengi sio ujanja kijana ni kujilimbikizia tu gharama zisizo na umuhimu. All the best
 
Usijaribu kuingia kwenye huo mtego,tulia na huyo mchumba wako...

Ukiendekeza kichwa cha chini tegemea nawe kuchapiwa,sijui utakua tayari?
 
Labda wewe unapungua
Baba watatu tulia. Hivi kwa huu uzi ungelikuwa wewe si tayari una mtoto wa nne. Huyu amekuja kuomba Ushauri wa nini ina maana situation ndogo kama hiyo anashindwa kuikabili. Like serious kabisa. Nasisitiza kwa kusema. WANAUME TUNAPUNGUA KWA KASI MNO. KASI YA LTE
 
usijaribu kumbebesha huyo dada mimba kama haupo tayari kumwoa anakutege ukiingia king ndio hivyo tena kamaliza dili
 
Mkuu utaoa bila kupenda uzoefu wangu huo ni mtego. Nina Rafik angu kaoa kwa hiyo style
 
Huyo mchumba naye anakudanganya bikri Siku hizi hazipo bikri za leo in zalimao kaka mwowaji uko chunguza vizuri hiyo bikri uko mtegoni kaka kimbia
 
Huyo mchumba naye anakudanganya bikri Siku hizi hazipo bikri za leo in zalimao kaka mwowaji uko chunguza vizuri hiyo bikri uko mtegoni kaka kimbia
Ni bikira wa kuzaliwa
 
Kosa kubwa unalolifanya ni kulea bikra.
Hakikisha hulei Hiyo kitu,utakuja ambulia manyoya.

Ukisha kamilisha hilo Huyo mchepuko hatakuwa na nafasi tena.

Tatizo lako ni kukosa sex ndio maaana unakuwa mwepes kushawishika na Huyo mchepuko.

Ila hivi ulipokuwa unachart nae unamtumia hela una mjali... Ulitegemea nn????

Kama humtaki acha mawasiliano nae...futa namba Yake

Unless nawewe unamtaka... Unataka tukupe go hed
mwache alee hyo bikra,siku akija kugonga akakuta n bwawa ndio atafungua akili.
 
Kumbuka kipindi huna kazi uliomba ukanyimwa ila umepata kazi yeye ndo anaomba fikiria chukua hatua
 
Back
Top Bottom