Mwingira amlaani mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:32
Elizabeth Suleyman
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.
Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. "Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.
"Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,"alisema Mwingira.
Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. "Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.
Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka," alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.
Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.
"Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,"alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.
"Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira. Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion' na baade ikaleta madhara."
Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.
Pengo alisema: "Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion' na baadae watu wakapata madhara makubwa.
"Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,"alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.
Comments
123
0
#44 jojas brand 2011-03-16 10:01 Nabi na Mtume.Ninaomba sana kwa maana hujuwi ulitendalo.Hiyo ni hofu yako,je?hizo of Money unazozipata na kuzila hizo hela unamhubiria shetani?Ni heri aliekubali kuchukua mia kuliko wewe.
Hifi ni hofu ya kukimbiwa na waumini wako baada ya kupona
Quote
0
#43 Neema Linke 2011-03-16 10:00 Mimi ninamuunga mkono Mwingira kuhusu huyo Babu ninapinga tiba zake na nunabii wake mungu ajamwelekeza wala hajamuotesha
lolote kuhusu kutibu watu,kinacho fanyika
kwa Baba ni Shetani ana mtumia anamutumia
Baba kuteka roho za watu ktk ulimwengu roho.ktkt Bibulia imeandikwa yakwamba Shetani ujigeuza anakujifanya kuwa kama malaika wa Nuru,mimi ninamkemea Baba kwa
jina la Yesu Kristo wa Anazaret ashindwe
Baba kadanganywa na Shetani.Hapo ktk dawa
zake hakuna nguvu za Mungu.Mtu akitaka kuponywa magonjwa yake ansome Bibulia
kuna ahadi ya uponyaji Isaya 53:3-5
Quote
0
#42 Mhifadhi 2011-03-16 09:58 Quoting Jesus is Lord God:
simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?
Please hata kama Mwingira ana mapungufu (kitu ambacho sio suala la msingi hapa), tujadili alichosema. Hata mlevi akikuonya, utakuwa makini kuchambua anachosema na si aliyesema, kwa kuwa main issue hapa ni kama Mungu wa Biblia ndiye anayetenda kazi na Babu Mwasapile.
Shalom!
Kili[NENO BAYA] mezani ni lile lililo zito. Swala la mtumishi mkuu mwema nabii mtume kuanza kuro po ka na kumwaga laana ni kubwa zaidi ya unayotetea ya kutokuwepo biblia n.k. Swala la hivyo vingine hakutupa uthibitisho ila ktk laana tumeona akituthibitishi a anavyojua kulaanai. Katika vitabu vitukufu watu hawa wamekuwepo tangu hapo kale na walikuwa wakijipendekeza kwa wafalme ili waonekane wao ndio basi. Wafalme wa siku hizi ni watu walio na hela na utaona manabii hawa wa uongo wakijipendekeza kwao. Mwache babu atumie anachotaka kutumia ili mradi waendao kule wanaimani wanaponywa. Mbona hatumsikii huyu nabii akiwalaani waganga? kama angekuwa anakemea ya ukweli miaka yote anapowalaghai watu basi leo kungekuwa hakuna uchawi wala mganga bongo na kila mtu anagekuwa akiishi maisha safi. THis is actually a downfall of mr. nabii mkuu mtumishi mtume na ukishaanza kuelekea kwenye downfall huwa hakuna turning back. Umewaonea sana waumini wako na kusababisha vifo bila sababu kwa kuwadanganyia maombezi bila dawa
Quote
0
#41 Ankali 2011-03-16 09:52 Kama unabii ni kutoa mapepo sielewi. Kakobe amelaani,laana haijafika, Kama Mwingira ni nabii wa kweli mbona hakuliona suala la mchungaji kabla halijatokea? Paulo (Saulo) alipoi[NENO BAYA] utume hakuwa mfuasi bali mtesi wa mitume wakati huo. Wasifikiri tunategemea uponyaji utoke kwa hao manabii uchwara. Mungu ana njia yake ya ajabu kuteua watu wake.
Quote
0
#40 The Matokeoism 2011-03-16 09:50
NGASTUKAA! KUMBE DINI NI SIASAA?
wengine wanabariki, wengine wanalaani,
jamani mbona mwatuchanganya, au kuna nini?
jamani viongoz w Mungu kaeni chini mtafakari ukweli kisha muangalie namna ya kumtangaza Kristu la mtaganyika, wakatoliki kwa waliteri, wpentekoste kw waaswmbly.
JAMANI MAMBO YA DINI ME SIMOOOOOOOOOOOO !
Quote
0
#39 Bernard 2011-03-16 09:47 Mwingira hacha unafiki wewe ukihubiri hautaji sadaka?kwanini unauza neno la Bwana?huyu babu kasimamisha shuguli zake zote ambazo zingemuingizia mapato kwa ajili ya kutibu watu.Nini mia tano anayotoza!!!
Quote
0
#38 Ruakia 2011-03-16 09:39 Huyu mtuu anaye jiita nabii anawaza nini? huyu mzee anayetoa tiba ni kama bure kulinganisha na bei yenyewe, na pia watu wanao kwenda kuchimba dawa na bili ya maji na kuni vyote hivyo anapewa bureeeeee! tuwaze kabla yakusema
Quote
0
#37 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:32 Jamani NGIWIRA asifuatwe ni mshenzi tu huyo sio nabii
Quote
0
#36 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:30 Mitume yote na Manabii wote wametajwa katika Vitabu vitukufu.
Hivi hawa mitume na manabii Josephat Mwingira anatokea wapi.
Huyu ni muongo na watu wasimsikilize bali waende kutafuta tiba.
Quote
+1
#35 paulsen shijah 2011-03-16 09:30 Haya sasa ni Majungu, Wewe mwingira kama kweli we ni mtumishi wa Mungu huwez kumuombea mabaya babu wa loliondo, kinachokusumbua wewe ni hiyo sh. 500 anayotoza? Au ni wasiwasi wa kukimbiwa na wumin!, hayo unayoyaomba yampate babu sio mazuri na hayana tofauti na arbadri, Wkristo tumeagizwa kuwapenda adui zetu na kuwaombea wale wote wa
naotuudhi, wewe umefanya lipi?, na ndio unajiita Mtume na Nabii, je!?, Kazi ya Mtume na Nabii ni Kulaani na Kuombea mabaya?, huduma zenu wenyewe haziaminiki, zimekuwa za kinafiki, kwenu mtu akipata uponyaji nilazima abaki kanisani kwenu lakin hatujasikia babu akilazimisha mtu abaki KKKT, unaponywa unaenda zako, sasa tatizo liko wapi?, lakin kwenu mnaponya na kuwaomba Pesa nyingi tu!, eti kwa Kisingizio cha Kumtolea Bwana Shukrani, mie nawomba kabla hamjatoa maoni au kupinga kitu ni vyema kuchunguza kwanza kuliko kuropoka ukaonekana kituko mbele ya jamii, kauli hiyo ya kulaani iko tofauti sana na Mafundisho ya Kiongozi wa Ukristo, YESU KRISTO mwenyewe, ni bora ungemuomba mungu akakufunulia kujua kama huduma hiyo inatoka kwake na sio kutoa maneno ya kukashifu na kulaan.
Kaka Mwingira wewe unaejiita Mtume na Nabii, Toa Kwanza Boriti lilomo ndani ya Jicho lako kabla hujatoa kibanzi ndani ya Jicho la Mwenzako.
Tuache unafiki tuseme kweli nayo kweli itatuweka huru,
Am Out.
Quote
0
#34 Jesus is Lord God 2011-03-16 09:25 simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?
Please hata kama Mwingira ana mapungufu (kitu ambacho sio suala la msingi hapa), tujadili alichosema. Hata mlevi akikuonya, utakuwa makini kuchambua anachosema na si aliyesema, kwa kuwa main issue hapa ni kama Mungu wa Biblia ndiye anayetenda kazi na Babu Mwasapile.
Shalom!
Quote
+1
#33 miriam 2011-03-16 09:21 wewe mtumishi nasikitisikitik a sana kwani mbona huduma yako pia inasikika haitoki kwa mungu unakwenda kupokea kwa mfalme wa giza mnapigana vikumbo na watu wa ulimwengu wa giza unafikiri ni kila mtu anakuamini?????? WEWE WATU WANAJUA VITU UNAVYOTUMIA KUVUTA WATU HUNA CHA INJILI ILA BIASHARA TU HAPO.
Quote
+1
#32 Kabigi 2011-03-16 09:18 Mwingira, Hivi wewe ni mtume kweli???Umepewa wapi mamlaka ya kulaani?Anayelaani ni Mungu si wewe.Ninamashaka na unabii wako.Mungu amesema tuombeane mema mbona wewe unayejiita nabii humuombei mema mtumishi mwenzako?Au kwasababu anatoa tiba sawa na bure?Au kwasababu Mungu amemuinue yeye na si wewe?Acha wivu bwana.Acha Mungu aliyemuumba amtumie kama apendavyo yeye na si wewe.Au ulitaka aje kanisani kwako ndo uamini Mungu amempa maono?Umetuboa na Si kuamini tena kama mtume kweli
Quote
0
#31 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:16 Jamani MWINGIRA anaonekana kama mtu asiye na busara hata kidogo na anaonekana kama mtu mwenye choyo kikubwa kwa sababu anaona kwa nini miujiza hii amepewa Mchungaji Mwasapile na hakupewa yeye.
Hivyo jamani Mwingire ni mtu mbaya na hafai katika jamii yetu kufuatwa kwani watu wanaonekana kupona.
Quote
0
#30 JOHN 2011-03-16 09:14 Jamani ninawaomba katu msipotoshe na matapeli wanaojiita ati ni Manabii, huo ni u[NENO BAYA]. Kwani yeye na familia yake anakula nini kama si kuwatapeli waumini wenye IMANI na dini yao. [NENO BAYA]IIIIIII.
Quote
123