harakat
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 2,887
- 1,350
Huwezi kupqmbana na wauza madawa ha kulevya ukiwa na wewe ni mchafu yaani una madhaifu tena yanayoonekana waziwazi ndio maana hata Mh. Rais alijitahidi sana kuhakikisha anakua na timu ya watu ambayo ni wasafi kwa kiasi kikubwa.
Suala la kuwa na mafisadi pia ni la kupigwa vita ndio maana kuna mahakama ya mafisadi Mh.Rais ameianzisha kwenye ufisadi huu sijui kama ufisadi dhidi ya Elimu yetu unaingia maana unapokua na vyeti feki maana yake tayari ni ufisadi kwa masuala ya Elimu.
Tuhuma ni kitu kimoja na kuzithibitisha ni kitu kingine ni ngumu sana kwa mazingira kama haya kudhibitisha tuhuma ambazo zinaonekana kuwa na mkanganyiko bila pia kuchafua majina ya watu ni ishu ya kusikitisha isihokuwa ya kiuungwana hata kidogo.
Inahitajika kjfanyika uchunguzi Wa kina ili kufikia kwenye hitimisho la kumuita MTU kwamba ni muuza unga au ni fisadi.
Tuangalie tuhuma ya MTU kukosa vyeti wakati ukiwa na wadhifa mkubwa serikalini .Hili si suala la lelemama hata kidogo ni suala zitu kwani linaleta aibu Kubwa kwa taifa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutokuwa makini kwenye vetting.
Aibu hii inaenda mbali mno na kjtuonyesha kwamba tuna kiongozi ambayo si waadilifu kwa maana ya kufanya ufisadi kwenye Elimu .watu Wa aina hii ni hatari kwa mustakabali Wa taifa kwani wako tayari kuvunja sheria za Nchi kwa manufaa na maslahi hao binafsi na hivyo wanaweza sababisha uvunjifu Wa Amani ya Nchi.
Katika mazingira haya hutaweza kuwa na uwezo Wa kugagua vyeti vya wafanyakazi Wa serikali vilivyohalali wakati cha kwako ni feki au huwezi kuwanhooshea vidole wenzako waliofoji ilihali kumbe na wewe ulifoji.
Katika mazingira hayo utakapoanza kunyoosha vidole kwa wenzio nao watarudisha tu vidole kwako hamna jinsi watakavyokuacha salama .
Katika mazingira haya yatupasa kuwa na uvumilivu na kutoa muda ili mambo kama haya yafanyiwe kazi naamini kwamba kila kitu hudhihirishwa na muda .
Muda ndio hutoa tofauti za mtoto Wa Simba na mtoto Wa Mbwa bila mwanzo hufanana.
Muda muda muda nawasilisha.