Huwezi kuamini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Huwezi kuamini

ijumaa wikienda
pix.gif
Na mwandishi wetu
Katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya madereva na makondakta wa daladala jijini Dar es Salaam wamefanya pati haramu ya kusherehekea kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri.....

Tukio hilo ambalo liliwakera na kuwaudhi wananchi wengi, lilitokea Jumatatu iliyopita katika Baa ya Minazini iliyopo Mwananyamala, Dar es salaam.

Awali, baada ya taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa zamani kuzagaa kila kona ya nchi, tofauti na matarajio ya wengi, baadhi ya makondakta na madereva jijini walianza kushangilia msiba huo huku wengine wakipiga honi kwa fujo barabarani kana kwamba kulikuwa na tukio la sherehe.

Katika kuthibitisha furaha yao nyuma ya kifo hicho, siku hiyo baadhi ya makondakta na madereva walijikusanya katika baa hiyo na kuanza kunywa pombe kwa fujo pamoja na kucheza muziki (kama wanavyoonekana pichani ukurasa wa nyuma)

Wakiongea na Ijumaa Wikienda katika nyakati tofauti, baadhi ya wananchi waishio maeneo jirani na baa hiyo, walisema kitendo kilichofanywa na watumishi hao wa daladala jijini ni laana kwa Mungu.

“Ni kweli kwamba Dito alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua dereva mwenzao na kila mtu alisikitika kwa tukio lile lakini sasa hii ya kufurahia kifo chake ni sawa na uendawazimu, inamaana hawajui kama nao watakufa?” Alihoji Rajabu Juma.

Naye Joyce John, alisema kuwa amekasirishwa na kitendo hicho na kueleza kwamba hawezi kuongea chochote zaidi ya kumuachia mungu.

“Siwezi kusema kwamba wachukuliwe hatua kwa sababu sijui sheria inasemaje katika hili la watu kuandaa sherehe kama ile, lakini kimsingi siyo ubinadamu, yaani hawa wanaonekana kuwa na roho za kinyama, Mungu atajua adhabu ya kuwapa,” alisema.

Ditopile alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu mjini Morogoro na kuzikwa siku mbili baadaye Kinyerezi, Dar es salaam ambapo kabla ya umauti kumfika, alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa dereva wa daladala, Hassan Mbonde.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Ditopile na Hassan Mbonde mahali pema peponi, amina.

Global Publishers - Tanzania Newspapers
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom