Huwa tunasoma ili iweje

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Hivi nia na dhumuni la kwenda shule huwa ni nini, kwa sababu kuna watu wanakwenda shule wanasoma sana mwishowe wanarudi mtaani na kukosa ajira.

Lakini pia wengine husomea biashara na wanaporudi mtaani hawana mtaji licha ya elimu yao wanatafuta ajira aidha kwa wakuu ambao wengine hawakusoma kabisa.

The main aim of going to school ni lipi endapo biashara zinafanywa na wasio na elimu ya biashara ambao baadae huwaajiri walio na elimu hio kuweka mambo yao sawa.

Nini aim ya elimu kwa ujumla?
What is School for?

#Iam Zagarino
 
Shule ni muhimu kuna fani zinahitaji utaalamu mfano
Udaktari
Ualimu
Urubani
Uhandisi nk
 
Hivi nia na dhumuni LA kwenda shule huwa ni nini kwasababu kuna watu wanakwenda shule wanasoma Sana mwishowe wanarudi mtaani na kukosa....

Lakini pia wengine husomea biashara na wanaporudi mtaani hawana mtaji licha ya elimu yao wanatafuta ajira aidha kwa wakuu ambao wengine hawakusoma kabisa...

The main aim of going to school ni lipi endapo biashara zinafanywa na wasio na elimu ya biashara ambao baadae huwaajiri walio na elimu hio kuweka mambo yao sawa

Nini aim ya elimu kwa ujumla?
What is School for?

#Iam Zagarino
Lengo la kwenda shule ni ili kupata ujuzi na maarifa.Ujuzi na maarifa ndo ufunguo wa maisha.bahati mbaya sana chini ya uongozi wa ccm na yesu wa burigi watu wanaenda shule ili wapate cheti.Ujuzi na maarifa si kipaumbele tena
 
Maarifa yanakusaidiaje katika maisha kwa mfano Una elimu ya biashara Ila huna mtaji wa kufanya biashara.

Ila mwingine elimu ya biashara hana ana mtaji na anafanya biashara
Ambayo wewe uliyesoma ni mhasibu wake
 
Maarifa yanakusaidiaje katika maisha kwa mfano Una elimu ya biashara Ila huna mtaji wa kufanya biashara
Ila mwingine elimu ya biashara hana ana mtaji na anafanya biashara
Ambayo wewe uliyesoma ni mhasibu wake
Mkuu maarifa yenyewe ndo mtaji,huwezi ukawa na ujuzi na maarifa ukakosa mtaji,kwenye biashara mtaji haujawahi kuwa issue,labda Kama unataka kufanya biashara ya kimachinja
 
Mkuu maarifa yenyewe ndo mtaji,huwezi ukawa na ujuzi na maarifa ukakosa mtaji,kwenye biashara mtaji haujawahi kuwa issue,labda Kama unataka kufanya biashara ya kimachinja
Wapo watu ambao wamesoma life skills wakiwa shule maarifa wanayo lakini ni wagomvi wa kwanza hao maarifa yao yamewasaidiaje?
 
Ungejua maana ya Elimu ungejua kwa nini unaenda shule kusoma.

Huwezi ishi bila Elimu.

Sasa inategemea na aina ya Elimu.

Moja ya sababu ya kupata Elimu ya darasani ni kurahisisha namna ya kupambana na mazingira.

MTU mwenye Elimu ya shahada labda ya Hotelia. Na yule anayejua mambo ya Hotelia lakini hajasoma, kwenye mshahara utashangaa mwenye shahada anapewa mshahara hata Mara tatu ya yule asiye na shahada. Licha ya kazi wazifanyazo in moja tena ukute asiye na shahada akawa anauwezo zaidi.

Bado hujajua kwa nini unasoma
 
Mkuu maarifa yenyewe ndo mtaji,huwezi ukawa na ujuzi na maarifa ukakosa mtaji,kwenye biashara mtaji haujawahi kuwa issue,labda Kama unataka kufanya biashara ya kimachinja
Maarifa tunayapataje endapo tunafundishwa History of Physics tu kwa nadharia na tunarudia the same experiments done by them
Badala ya kuwa creative na kubuni vyetu!
 
Ungejua maana ya Elimu ungejua kwa nini unaenda shule kusoma.

Huwezi ishi bila Elimu.

Sasa inategemea na aina ya Elimu.

Moja ya sababu ya kupata Elimu ya darasani ni kurahisisha namna ya kupambana na mazingira.

MTU mwenye Elimu ya shahada labda ya Hotelia. Na yule anayejua mambo ya Hotelia lakini hajasoma, kwenye mshahara utashangaa mwenye shahada anapewa mshahara hata Mara tatu ya yule asiye na shahada. Licha ya kazi wazifanyazo in moja tena ukute asiye na shahada akawa anauwezo zaidi.

Bado hujajua kwa nini unasoma
Nawaza ingekuwaje Kama wanachuo wanaohitimu wasingekuwa wanapewa vyeti nahisi wangehisi ni wajinga ?
 
Nawaza ingekuwaje Kama wanachuo wanaohitimu wasingekuwa wanapewa vyeti nahisi wangehisi ni wajinga ?

Huwezi kusoma na kuthibitishwa umesoma,
Cheti ndio uthibitisho kuwa ulisoma, cheti hakina kazi zaidi ya uthibitisho.

Mtu anaweza asiwe na cheti lakini akawa na ujuzi, lakini hawezi kuaminika hata kama anaujuzi bila ya kuwa na cheti.

Elimu sio cheti, ila cheti ni moja ya vithibitisho vya Elimu ya MTU kabla ya kuanza kazi
 
Back
Top Bottom