Huwa nawaza, hivi ile vuta nikuvute ya Kikwete na Kagame ingekuwa ni Magufuli ingekuwaje?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,733
26,867
Kama mnavyokumbuka kipindi cha nyuma awamu ya 4 chini ya Jakaya Kikwete iliwahi tokea sintofahamu kati ya Rais Kikwete wa Tanzania na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Na wakati huo yale malumbano yalimalizwa kidiplomasia/kimazungumzo mambo yakaisha, lakini kuna baadhi hadi walimuona JK kipindi hicho kwa nini anakuwa mpole, wakati jeshi na nguvu na uwezo anao, kwanini anakubali kudharauliwa kiasi hicho.

Hivi kwa dharau zile za Kagame kipindi hicho Kikwete angelikuwa na maamuzi magumu kama ya Magufuli, mpaka sasa hii nchi ingekuwa kwenye wakati gani? Je, Magufuli angepeleka jeshi msituni au angekuwa mkimya kukubali yaishe kama Kikwete?

Karibuni kwa hoja.
 
Kwa huyu mwamba Magu, nadhani mida hii Kagame angekuwa nyampara gereza la Karanga - Moshi au gereza LA Uyui- Tabora, au amesharest in pisi.

Halafu bora ukumbane na Pirate kuliko magu maana yy naonaga siyo wa sayari hii; hana msalie Mtume wala nini.
 
Umemsifia utadhani anaweza hata kurusha ngumi. Wakati kiuhalisia yeye atajificha tu kwenye handaki akisubiri ripoti za Vijana walioko field...
 
Back
Top Bottom