Huwa mnamsoma Ulimwengu?

Huyu mzee ni fisadi tu hana jipya. Kwanza ni mdini. Pili yupo bitter baada ya kuwekwa benchi na kuondolewa kwenye lineage ya wala nchi..thats the motives msiwe naive mazee.

Majinga utayajua tu,huwa yanajibu bila fact,kipi cha ajabu hapo.hata mpagani ni mdini,kama aliondolewa kwenye lineage ya wala nchi baada ya yeye kukataa ku collaborate anageuka kuwa fisadieee.kaazi kwerikweri
 
Huyu mzee ni fisadi tu hana jipya. Kwanza ni mdini. Pili yupo bitter baada ya kuwekwa benchi na kuondolewa kwenye lineage ya wala nchi..thats the motives msiwe naive mazee.

Huo ni mtizamo wako, besides hakuna binadamu (aliye hai ama mfu) ambaye hana/hakuwa na upungufu duniani.

Wanachosema wadau ni kwamba Ulimwengu ana maandishi yaliyoenda shule kikwelikweli na kiukweli watanzinia wachache sana sasa hivi wanaweza kum-match jamaa katika kuandika makala za kiuchambuzi. Tunaobahatika kumsikiliza akihojiwa ama akiwa kwenye mijadala mbali mbali tunatambua hili.

Yeye kutopatana na Mkapa hakuathiri tathmini yetu juu ya maandishi yake!!

Ulimwengu is one of the very few true intellectuals that we currently have in Tanzania!!!!
 
Mkuu kumbe hujamsoma jenerali ktk maoni ya mhariri-raia mwema? Waulize wasomaji wengine wa gazeti hili kama mimi ninasingizia mtu hapa.

Alitoa ktk maoni ya mhariri then akaandika makala nzito ya kumuomba radhi alhaj mwinyi na awamu yake.

Kwa sababu raia mwema haijafikisha mwaka tafuta marejeo utapata hilo gazeti.
 
namkubali sana ulimwengu, lakini huwa natatizwa naye anapokuwa kigeugeu. kwa waliomsoma kipindi kile katika rai, baada ya kikwete kuingia madarakani, wataona kama nyoka anayefahamu mambo mengi sana, lakini asiyejua ashikilie lipi moja. yafuteni makala ya jina la BARUA KWA KIKWETE. HATA HIVYO NINGEPENDA KUMSIKIA ULIMWENGU AKICHAGUA NJIA NYINGINE YA KUFIKISHA UJUMBE KWA WANACHI WENGI ZAIDI, HATA KWA KUTOA MIHADHARA SEHEMU MABALIMBALI AMBAPO NAAMINI UDHAMINI WA KUFANYA SHUGHULI HIUO UPO WA KUTOSHA ,KULIKO GAZETI AMBAZO RICH YAKE SIYO KUBWA SANA.
 
Mkuu Mziwanda,

Huwa sikosi gazeti la Raia Mwema kila alhamisi, lengo kuu ni kumsoma huyu bwana. Kwa kweli ni mmoja kati ya watu wachache ambao nawapa heshima kuu nchini kwetu. Tumuombe mungu ampe maisha marefu kwani anachokifanya ni faida kubwa kwa wengi wengi

KIla JUMATANO
 
yap , makala za jamaa zimeenda shule, ni mtu ambaye anaelimisha jamii, lakini kama alivosema bwana mziwanda kuwa Wabongo wengi hawana full access ya magazeti au internet, then comes a problem, kwa sababu mtu wa kijijini anasoma gazeti la leo labda baada ya mwaka mmoja na ndo maana elimu ya uraia inakuwa ngumu na inawafikia wachache, lakini kama Tanzania miundo mbinu iingeimarishwa basi nafikiri Tanzania ya sasa CCM wangelia sana, make tungekuwa tumewaerase kwenye History kama KANU ya Kenya.

Bravo Ulimwengu, keep it on.

Rom
 
Mkuu ulimwengu anasomeka ila bado anaendelea na kaugomvi kak na mkapa na kidogo sasa anadiriki kupingana na utakatifu wa kambarage ktk maono yake ya kitawala, maana haishi kuwahukumu hawa wakuu wawili ktk kila makala zake, ni vizuri tunamsoma na kumtafakari maana mzee wetu ulimwengu kwakweli ana nyanga za mbivu kwelikweli.

Taratibu namuona anajiandaa kuanza kuishughulikia awamu ya nne baada ya kuiomba radhi awamu ya pili ambayo kwake yeye sasa anathubutu kutuaminisha kuwa ilikuwa bora zaidi kwa nchi yetu.

Pamoja na mapungufu yote, suala la awamu ya pili kuombwa radhi sina kumbukumbu sahihi kama Jenerali mwenyewe ndiye aliyeomba radhi, lakini naamni watu wengi makini ninaowafahamu katika media wanakiri hadharani hata katika maandishi yao kwamba Watanzania wakiongozwa na media wanapaswa kumuomba radhi huyu mzee wa watu, na hiyo ni baada ya kuona kwamba viongozi wote walioshika madaraka ya nchi hii wamefanya madudu mengi kiasi cha kumuona Mwinyi kama MALAIKA. Hayo sasa yanaelekea kuonekana kwa baadhi ya viongozi waliowahi kushika uongozi wakatai wa Mkapa na wao kuonekana wachafu, kumbe Mkapa alikuwa mchafu zaidi na sasa wanaanza kuonekana nao ni watu wema.

Pia nadhani ondoa hayo mawazo hasi (-ve) kusema, "kuanza kuishughulikia awamu ya nne", maana waandishi, wachambuzi na wanaharakati na hata viongozi wa dini wanachofanya si kushambulia bali ni kutimiza wajibu wao kwa jamii wa kusimamia watawala kwa maslahi ya Umma na Taifa letu. Ama kwa baadhi kuteleza hilo si tatizo maana lipo duniani kote na ni ubinadamu.
 
Wako watu watatu kwa sasa katika NCHI hi ambao wakiandika lazima niwasome. Jenerali, Mzee Mwanakijiji na Johnson Mbwambo. Sina la kufanya na maandishi yao haya ambayo kama watawala/Viongozi wangeyaelewa pengine hali ingekuwa tofauti na tuliomo kama Nchi.
 
Personality cult in making...
 
Huo ni mtizamo wako, besides hakuna binadamu (aliye hai ama mfu) ambaye hana/hakuwa na upungufu duniani.

Wanachosema wadau ni kwamba Ulimwengu ana maandishi yaliyoenda shule kikwelikweli na kiukweli watanzinia wachache sana sasa hivi wanaweza kum-match jamaa katika kuandika makala za kiuchambuzi. Tunaobahatika kumsikiliza akihojiwa ama akiwa kwenye mijadala mbali mbali tunatambua hili.

Yeye kutopatana na Mkapa hakuathiri tathmini yetu juu ya maandishi yake!!

Ulimwengu is one of the very few true intellectuals that we currently have in Tanzania!!!!

Hayo uliyoyanukuu unasema ni mtazamo wangu ..yes! una tatizo na hilo?

Ninachoona ni kuwa ameandika kile kinachokufurahisha ..au ulichotaka kukisikia. Sina tatizo na waandishi na maandishi yao, bali naangalia larger picture na motives zao, mimi sio naive au mwenye kuamini haraka kama wengi wenu.

Ukitaka data zaidi tafuta kuna thread nyingine ya Ulimwengu uone upande wa pili wa shilingi.
 
Majinga utayajua tu,huwa yanajibu bila fact,kipi cha ajabu hapo.hata mpagani ni mdini,kama aliondolewa kwenye lineage ya wala nchi baada ya yeye kukataa ku collaborate anageuka kuwa fisadieee.kaazi kwerikweri

Wewe choko kama huna la kuongea kaa kimya.
 
wako watu watatu kwa sasa katika nchi hi ambao wakiandika lazima niwasome. Jenerali, mzee mwanakijiji na johnson mbwambo. Sina la kufanya na maandishi yao haya ambayo kama watawala/viongozi wangeyaelewa pengine hali ingekuwa tofauti na tuliomo kama nchi.

ndugu ukisoma maandishi ya mwanakijiji ni sawa na unavyosoma jf tu kwahiyo usifananishe mwanakijiji , mwambo na jenerali hivyo ni vitu tofauti kabisa yaaani umeonyesha jinsi ulivyobutu mkuu
 
Hawa ndio wanaodeserve kupewa doctorate za heshima kutoka vyuo vikuu, na sio akina JK na karume,

To be honest huyu J.Ulimwengu amewaacha mprofessor wengi mno katika kuleta maendeleo ya nchi hii!

T
 
Wako watu watatu kwa sasa katika NCHI hi ambao wakiandika lazima niwasome. Jenerali, Mzee Mwanakijiji na Johnson Mbwambo. Sina la kufanya na maandishi yao haya ambayo kama watawala/Viongozi wangeyaelewa pengine hali ingekuwa tofauti na tuliomo kama Nchi.

You are right add Lusekelo mtambo mwingine wa kuvutia hajali yuko kwenye magazeti yao!
 
Huyu mzee ni fisadi tu hana jipya. Kwanza ni mdini. Pili yupo bitter baada ya kuwekwa benchi na kuondolewa kwenye lineage ya wala nchi..thats the motives msiwe naive mazee.

Hata kama unachosema ni kweli basi ujue ni mipango ya nature (kama huamini katika Mungu). waweza kuita coincidence ukitaka, yaani itokee kutokuelewana ili ukweli uwekwe wazi. tunahitaji mchango wako ambao ni chanya
 
Kwa kifupi ni kama nilivyoeleza, kuwa huyu mzee baada ya kutoswa baharini na nahodha mwenye meli na mabaharia wenzake, akaamua kufanya kila lililo kwenye uweza wake kuipindua meli..this is exactly what has been happening..need i say more?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom