Huwa inatokea mwanaume kum-admire mwanaume mwengine, na ni kawaida

Huwa inatokea mwanaume kum-admire mwanaume mwengine, na ni kawaida

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
1,475
Reaction score
3,538
Kuna kitu wanaume huwa hawa admit mana wanaona kukubali hii ni kama sio urijali, ila unaweza ukatokea tu unamkubali jamaa fulani naturally, labda ukimuona au kumsikia, haimaanishi kwamba wewe sio lijali, i upendo tu wa kawaida ad natura one.

Kwa wadada wao hawafichi mana katika jamii hiwezi kuleta picha yoyote tofauti.

Mi niiwahi kumkubali public figure fulaini, vile tu anavyoongea basi, ila kadri nilivyokua nikimsikiliza aadae nikawa naona kawaida tu. waongo watabisha.
 
Kumkubali = kuendana = kuhusiana

Huwezi kuwa na rafiki kama hujamkubali

Huwezi kuwa na mentor kama huja_admire harakati zake na kuamini atakuvusha

Huwezi kuwa na favorite artists au role model bila admiration

Tofauti ni wanawake huziongelea na kuzionesha ila kwa wanaume. Ni kuoneshana zaidi, mtu hawezi kukuambia anakupenda ila utaona jinsi atavyobeba matatizo yako au atakupambania ili utoboe. So tofauti ni communication tu
 
1000007881.jpg
 
Kuna kitu wanaume huwa hawa admit mana wanaona kukubali hii ni kama sio urijali, ila unaweza ukatokea tu unamkubali jamaa fulani naturally, labda ukimuona au kumsikia, haimaanishi kwamba wewe sio lijali, i upendo tu wa kawaida ad natura one.

Kwa wadada wao hawafichi mana katika jamii hiwezi kuleta picha yoyote tofauti.

Mi niiwahi kumkubali public figure fulaini, vile tu anavyoongea basi, ila kadri nilivyokua nikimsikiliza aadae nikawa naona kawaida tu. waongo watabisha.
Kuna kipindi walikuwa wanawagawia watoto wa shule kitabu kama hiki, kwamba usijisikie vibaya ukipata hisia na mwanaume mwenzio ni kawaida kabisa.. hii ni hatari!
 
Wanaume hawako hivyo umeiweka kilaini sana kama rafiki rafiki tu unamkubali kwenye hustle zake na mnapeana support kwenye mishe na kila siku mnaonana na vitu kama hivyo!...ila siyo ku admire the way mshkaji anavyoonge sijui anakuvutia sura sijui nn hapo men hatupo hivyo!...jishikilie mkuu
 
Kuna kitu wanaume huwa hawa admit mana wanaona kukubali hii ni kama sio urijali, ila unaweza ukatokea tu unamkubali jamaa fulani naturally, labda ukimuona au kumsikia, haimaanishi kwamba wewe sio lijali, i upendo tu wa kawaida ad natura one.

Kwa wadada wao hawafichi mana katika jamii hiwezi kuleta picha yoyote tofauti.

Mi niiwahi kumkubali public figure fulaini, vile tu anavyoongea basi, ila kadri nilivyokua nikimsikiliza aadae nikawa naona kawaida tu. waongo watabisha.
Mbona mimi namkubali Arnold Schwarzenegger kiasi kwamba kuna kipindi nikiwa chuo mwaka wa kwanza nilikuwa nafuatilia maisha yake ya miaka ya 70, 80, akiwa Professional Bodybuilder kabla hajazama sana kwenye Uigizaji wa filamu za Kivita, nilikuwa namfahamu toka kitambo toka nikiwa mtoto mdogo lakini kumfuatilia kindakindaki nilianza nikiwa chuo kikuu FIRST YEAR na nilikuwa sifichi, nilikuwa nampostiposti WHATSAPP STATUS mpaka baadhi ya watu wakaanza kuniita jina la utani la "BABA JANE" na huyu mwamba ndiyo alikuwa anani-inspire sana hata kuanza kujenga mwili nikiwa chuo FIRST YEAR. Yani nilikuwa namkubali hatari, muonekaano wake wa kibabe afu handsome na pigo zake kama kutoongea sana vitendo zaidi yani hizo pigo zake zinafanya nimkubali Arnold Schwarzenegger mpaka kesho. Huo ni mfano wa kwanza.

Mfano wa pili, kuna Mtangazaji wa Radio Free Africa (RFA) miaka ya 2016 alikuwa anajiita MBURU ZE BOSS sijui bado yupo hai au la maana tangu niende ADVANCE niliachaga kufuatilia vipindi vyake kutokana na ubize na shule. Sasa huyu MBURU ZE BOSS nilikuwa namkubali kinoma yani jinsi anavyoongea yani nilikuwa namkubali hatari, ile ongea yake tu ya kishikaji afu na sauti yake ile nilikuwa napenda sana kumsikia akiongea. Nilikuwa napenda kipindi chake cha Ijumaa saa nne usiku mbaka sita usiku nadhani japo pia alikuwa na vipindi vingine siku zingine.

Ko nakubaliana na wewe, naunga mkono hoja, mwanaume kumkubali mwanaume mwenzako ipo wala sio kesi.

Yani hicho ni kitu cha kawaida kabisa. Wanaoona ni kitu cha ajabu wana mitazamo hasi tu! Kumkubali mwanaume mwenzako sio dhambi wala sio kesi.
 
Back
Top Bottom