Huu wimbo bado unaimbika?

kingfish

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
571
Reaction score
159
CHAMA TAWALA WALIKUWA NA WIMBO HUU HAPO ZAMANI.
"Chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi"
SWALI:Wimbo huu bado unaimbika midomoni mwa watanzania?
 
Imba ukisikia unaitikiwa utajua bado unaimbwa. Haya, 1, 2, 3
 
Zomba, ritz na Rejao wanaimba wimbo huo usiku kabla ya kulala na asubuhi baada ya kuamka.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nilishausahau huo wimbo, halafu kina Nnauye Jr anakuja hapa na kusema wapinzani hawana jipya, bila wapinzani tungejua kuna Kagoda, EPA na mengine mengi ambayo wameahindwa kuyafumbua ukianzia na ufisadi unaoitesa serikali na chama twawala!!! Aibu!!
 
Last edited by a moderator:
Unanikumbusha mbaliiii saaana enzi za Mwl, kweli ulikuwa na hamasa ila sasa, ukiwaambia mafisadi waimbe ili kuhamasisha ugawaji wa rushwa kwenye uchaguzi ndani ya CCM huko Dom na Mikoani, haaaa utaeleweka
 
Nashukuru sana kwa kunichekesha!! Kwa mlio changia maana huu wimbo kwa sasa ukianza kuimba unaanza kungalia huku na huku usije tukanwa na huenda ukapigwa!!
Ukitaka kupigwa kaanzishe hata shule ya msingi uone!!
 
Kama wenye nao wameshausahau, wapita njia wataweza hata kusoma herufi kweli? Nafikiri hayo maandishi yamebaki kwenye makabrasha tu.
 
Sasa unaimbwa hivi, chai chapati maharagwe mchuzi vya jenga mwili
 
na mwengine tuliimba hivi;
...." sasa naahidi mbele ya chama ....mapinduzi nitakulinda mpaka kufa"
 
CHAMA TAWALA WALIKUWA NA WIMBO HUU HAPO ZAMANI.
"Chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi"
SWALI:Wimbo huu bado unaimbika midomoni mwa watanzania?
umeshasahaulika hata kwa wanaccm wenyewe na kama bado wanaukumbuka basi wanaona haya kuuimba
 
Huu wimbo uliimbwa enzi hizo kwa sababu kweli ccm chini ya Nyerere angalau kulikuwa kuna alama za kujenga nchi. Viwanda, Makampuni ya umma, Kuwaunganisha watanzania, kuwaelimisha hata kwa bure.
Lakini ccm ile sio hii ya leo. Hii ya leo inajenga majumba ya kifahari ya mafisadi na kugharamia watoto na familia zao masomo nje ya nchi na kuiba rasilimali za taifa. Kwa kifupi huu wimbo hauimbiki kwa sasa.
 
Huu wimbo hauna mvuto tena .............. :confused2:
 
Kama wenye nao wameshausahau, wapita njia wataweza hata kusoma herufi kweli? Nafikiri hayo maandishi yamebaki kwenye makabrasha tu.
Hawajausahau mkuu,hauimbiki kwani chorus itakuwa na maswali mengi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…