Huu uoga umeanza lini CHADEMA?

Huu uoga umeanza lini CHADEMA?

Maramla

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
588
Reaction score
648
HUU UOGA UMEANZA LINI CHADEMA?

Na Mwal. NICHOLAS, SOMBETINI

Nimekuwa muumini wa siasa za hoja kwa muda mrefu sasa kwangu CHADEMA imekuwa shule na wakati mwingine kama nyumba ya mawazo mbadala. Vijana wengi tulioanza siasa katika Viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam tulivutiwa na muktadha huo. Lakini kwa hili la CLOUDS360 leo naona aibu kujiita mwanachadema.

Kwa wenye kumbukumbu mtakubaliana na mimi kuwa ilifika wakati vijana wa CCM wakawa hawana ubavu wa kusimama katika majukwaa ya ushindani wa hoja. Leo DC wa Hai na Kijana wa CCM kushiriki kipindi cha Clouds kila mtu anatoka POVU eti Clouds inaiua CHADEMA, seriously??? Yaani tumekosa hoja kiasi hiki?

Nani asiyejua juzi hapa Zitto Kabwe alikuwa pale Clouds360 ? Alienda kuisifia serikali ya CCM? Nani asiyejua wanaharakati wetu kama Bob Wangwe wamepata airtime Clouds360 ? Je ni kwasababu ya uana CCM wao? AU Uwezo wa kujenga hoja ndio unaowapa airtime pale ? AU kwa kuwa Nyalandu nae alipata airtime? Kwani Boniface umezuiwa kwenda? Pambalu umezuiwa kwenda?

CHADEMA kama itakufa msingi wa kifo chake ni sisi wanachama tusiofikiri na badala yake tunacheza ngoma zisizo na msaada kwa chama. Hivi CHADEMA kazi yetu kuandika Tweet siku nzima? Kazi yetu kupiga soga na watu walio ughaibuni mtandaoni ? Hivi kazi yetu kupiga majungu siku nzima kumfuata mtu anayeogopa hata kutumia jina lake twitter na badala yake anatumia parody na kujiita "Kigogo". CHADEMA tuamke, tujibu hoja na kujijenga kama chama badala ya kundi la wahuni mtandaoni.
 
Back
Top Bottom