Huu ulinzi balaa!!!

Abbasfarudume

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,625
1,324
Wakuu habari za kutwa matumaini yangu mmeshinda salama, twende moja kwa moja kwenye mada. Hii leo asubuhi saa nne na nusu nipo petrol station pale banana, ukapita msafara mkubwa wa askari ukiongozwa na pikipiki ya traffic police, nyuma ya pikipiki ya traffic police kulikuwa na gari kama 40 au 50 mchanganyiko wa askari niliowaona makachero TISS magereza na bus kubwa la kubebea mahabusu na land cruiser za police na za magereza na TISS wakiwa na silaha nzito nzito, wakiwa wamezishika na kuzielekeza juu angani na wengine kuzielekeza kwenye lile gari la mahabusu, sasa sijajua kama ni magaidi au la? Maana na huo mwendo waliopita nao kwenye riffs matuta yale ya banana karibu na shule ya msingi minazi mirefu bus la mwendo kasi kutoka kimara kwenda kivukoni mara 4 yake Nb ulinzi sio wa mchezo mchezo!
 
Hayo huku kwetu Mkuranga na Kibiti tumeyazoea wala sio story ya kushangaza.
 
Gari 40 ni nyingi!!!! Kwa hiyo kama waliachana at least meter 3 mpaka 5 watakuwa walicover 200+ metres zakukutosha kutukamatia walau kapicha ungetuwekea hata picha maana nahisi banana pali banwa kwelikweli!
 
Niloziona gari zilikua nane si arobaini chumvi uliyo ongeza ni kiboko.
Yani ndo nimetoka kujiuliza sasahivi huyu gari 40 mpaka 50 alizozitaja nikipiga hesabu ya haraka naona walicover let's say banana shely mpaka majumba sita hivi wao peke yao maana gari zao hazifuatwi!
 
2a51da03c28286923e96b289d974890d.jpg
hadi hao waliovaa mabaka mabaka walikuwepo pia na silaha zilishikwa hivyo hivyo asubuhi ya leo
 
Wakuu habari za kutwa matumaini yangu mmeshinda salama, twende moja kwa moja kwenye mada. Hii leo asubuhi saa nne na nusu nipo petrol station pale banana, ukapita msafara mkubwa wa askari ukiongozwa na pikipiki ya traffic police, nyuma ya pikipiki ya traffic police kulikuwa na gari kama 40 au 50 mchanganyiko wa askari niliowaona makachero TISS magereza na bus kubwa la kubebea mahabusu na land cruiser za police na za magereza na TISS wakiwa na silaha nzito nzito, wakiwa wamezishika na kuzielekeza juu angani na wengine kuzielekeza kwenye lile gari la mahabusu, sasa sijajua kama ni magaidi au la? Maana na huo mwendo waliopita nao kwenye riffs matuta yale ya banana karibu na shule ya msingi minazi mirefu bus la mwendo kasi kutoka kimara kwenda kivukoni mara 4 yake Nb ulinzi sio wa mchezo mchezo!
Ulinzi wa namna hiyo mara nyingi nauonaga kwa wahalifu hatari (magaidi, wahaini, majambazi sugu na nk)
 
Back
Top Bottom