Huu ukimya unaashiria nini kwa Wapinzani hapa nchini?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kumkubali mtu kuwa yupo vizuri sio mpaka utamke maneno, uweza kukubali hata kwa kutikisa kichwa au kukaa kimya.

Tujihoji kwa umakini, kama Chama cha Upinzani makini hapa nchini utakaa kimya kama haungi mkono yanayofanywa na chama tawala?

Kwanini uchukue ruzuku na kuitumia ili hali unajua ni haramu? Ndio maana hatusikii viongozi wa Chadema wakitoa matamko? Kwahiyo wameamua kuunga juhudi kimyakimya?

Ok, basi kama mnaunga juhudi tunataka tamko la Chadema kuunga juhudi rasmi kama wenzao ACT Wazalendo. Kulikoni kuunga kimyakimya kama binti aliyetoroshwa na kufunga ndoa ya kimyakimya kisha baada ya miaka 3 mnakuta amezalishwa watoto wanne na kutelekezwa.
 
Vipi mmeanza kujihisi wapweke bila wapinzani? Tulieni dawa iwaingie maana mmeamua muwe wenyewe kijani sasa mnawataka wapinzani wawasaidie nini tena?
Kwahiyo kila mtu ni CCM sasa, kuna watu tupo kusikiliza mawazo ya wengine kazi yetu kubwa ni mpira na hatuulizi chochote ila tunaulizwa Kwa sababu upande huo tunajua vizuri.

Hembu tuache ushamba sasa dawa iwaingie mara ngap dawa kitambo inaingia swali lijibiwe, mdau atoke na mawazo chanya.
 
Mmekosa wa kutafuna sasa mtaanza kutafunana wenyewe
IMG_20210120_161741.jpg
 
Vipi mmeanza kujihisi wapweke bila wapinzani? Tulieni dawa iwaingie maana mmeamua muwe wenyewe kijani sasa mnawataka wapinzani wawasaidie nini tena?
Yaani CDM mnajiona wajanja na kwamba mnaikomoa serikali ya CCM wakati mnaiunga mkono kwa kupokea ruzuku na kupeleka bungeni viti maalu 19 kimyakimya kwa kuogopa kuitwa CCM-C !! Achani siasa za ujanja janja!

Tunachotaka sisi ni kuona uhai wa vyama vya upinzani kwa kujitokeza kukemea uvunjifu wa katiba unaofanywa na CCM. Inawezekanaje kila linalotakiwa na chama tawala linakuwa tena hata kwa kuvunja sheria za nchi alafu pasiwepo wanaharakati wa kuzuia au kulaani.
 
Yaani CDM mnajiona wajanja na kwamba mnaikomoa serikali ya CCM wakati mnaiunga mkono kwa kupokea ruzuku na kupeleka bungeni viti maalu 19 kimyakimya kwa kuogopa kuitwa CCM-C !! Achani siasa za ujanja janja!
Aibu kubwa sana,alafu wamejazana humu Jf wanajifanya wapinzani wa ukweli.
 
Ukimnya unaashiria kwanba wamekubali yaishe, ila kimnya kimnya wafuasi wanapenda longo longo wakisikia itakuwa baraaa.
 
Ukimya ni kwamba hawana cha kusema. Ajenda ya Covid imeanza kidogo kunukanuka msubiri Mbunge (Mstaafu) Heche ataanza kumlaumu Waziri wetu mpya wa Afya (Mbunge mteule). Covid inatoka Kenya, unakumbuka kwenye uchaguzi lilikuja rundo la Washashi wa Kenya kumpigia debe tundulissu?
 
Mnataka Maalim aanze kubishana tena sasa?
Aanze kutaja Uhanithi?
Wakati kilichotafutwa kimepatikana,
Ruzuku imepatikana
Viti maalum vimepatikana,
Makamu kaimu amepatikana,
Sasa ni mwendo wa kula kuku kwa mrija.

"Penye shibe hapana kelele"

RIP Christopher Mtikila
 
Mnataka Maalim aanze kubishana tena sasa?
Aanze kutaja Uhanithi?
Wakati kilichotafutwa kimepatikana
Ruzuku imepatikana,
Viti maalum vimepatikana,
Makamu kaimu amepatikana,
Sasa ni mwendo wa kula kuku kwa mrija.

"Penye shibe hapana kelele"

RIP Christopher Mtikila
Maalim ameunga juhudi hadharani, hajamumunya maneno.
 
Back
Top Bottom