Mwigulu Nchemba kwa anayofanya yupo sahihi, soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu Nchemba kwa anayofanya yupo sahihi, soma hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by frema120, Jul 21, 2012.

 1. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  NIMEJITAIDI NIWEKE KWENYE FILE LAKE ORIGINAL IKAGOMA BUT SOMA SASA (tafakari chukua hatua... ngeengeee .. haki ya elimu...)


  CHAMA CHA MAPINDUZI

  KUHUISHA MTANDAO WA WANA CCM KATIKA VYUO NA MASHINA YA WAKEREKETWA
  Kumetokea na sura tofauti katika hali ya kisiasa nchini hivi karibunikufuatia propaganda za CHADEMA kutaka kujipatia umaarufu na kujitafutia uhalalikwa njia ya kuichonganisha serikali na wananchi na kupandikiza chuki dhidi yaChama cha Mapinduzi. Hali hii imedhihirishwa na juhudi za makusudi zilizofanywana chama hicho za kupotosha ukweli, kutokuona ukweli na kung'ang'ania uzushikuwa ndio mtaji wao wa kisiasa bila hata kujali masilahi ya Taifa na misingi yautu iliojengwa kwa wananchi wake. Kwa mfano kumekwepo na upotoshaji wa kuwahakuna uthubutu wa serikali ya awamu ya nne, ubunifu, kubeza mafanikio nawakati mwingine kuropoka kuwa hakuna mafanikio yaliofikiwa tangia uhuru. Piakumekwepo na lawama kuhusu kupanda kwa gharama za maisha bila hata kuzingatiachanzo cha gharama hizo kinatokana na nini badala yake lawama zinatolewa kamavile bei zimepandishwa na Chama na Serikali na viongozi wake.Hii imesababisha baadhi ya wananchi kwa kutokujua ukweli kupotoka nawengine kushabikia nadharia bila kutaka ukweli na bila kujali madhara yaushabikiaji wa vitu vya kizushi kuwa una athiri umoja, aman, utulivu nahata shughuli za uzalishaji . matokeoyake tumekuwa tukishuhudia vitendo vya uvunjifu wa taratibu maeneotofautitofauti.Baadhi ya vitu vilivyochangia kukua kwa wimbi hili katika vyuo vikuu na maeneo mengine kamailivyoelezwa katika kikao cha baadhi ya wabunge vijana na viongozi na wanachamawa vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma ni
  • Kudhofika kwa UVCCM na vitengo cha propaganda vya CCM kwa ngazi zote kiasi cha kupungua kwa watu wa kukitetea chama na kuelezea mafanikio yaliopatikana kutokana na jitihada za serikali yake.
  • Kupungua kwa moyo kujitolea kufanya kazi za chama kwa wa CCM wakati usio wa uchaguzi na kuyaacha baadhi ya makundi kama vijana bila mawasiliano mpaka wakati wa Uchaguzi. Kukosekana kwa mikutano na wanachama kwa viongozi wa vijana Taifa hata ile isio rasmi kiasi cha kuwafanya wafuasi wa CCM vyuoni kuwa wapweke.
  • Kutokufanyika kwa semina za mara kwa mara kwa wanafunzi zinazohusu fursa hivyo kuwafanya wakate tama na kupotoshwa kirahisi kwa kauli za vitisho za wapinzani.
  • Kutokuwafanyia semina za mara kwa mara kwa wakereketwa wa CCM walioko vyuoni ili kuimarisha uhusioano na chama na serikali na kujua undani wa chama, sera na mafanikio yaliofikiwa na serikali ili kuwa na mwelekeo wa pamoja na kauli ya pamoja wanapoitetea serikali
  • Wanafunzi walio wana CCM kukosa mawasiliano hata ya kufikisha taarifa za siri punde kunapokuwepo na vuguvugu vyuoni na pia hakuna mtandao wa kuwafikishia taarifa hata wafuasi wa CCM kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuhusu malalamiko ya wanachuo.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa kauli za wahadhiri wanapoibeza serikali wanapofundisha na wakati mwingine kufanya kampeni za wazi wazi darasani kinyume na sheria za utumishi wa uma za kutokufanya siasa mahali pa kazi.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa vurugu wanazofanyiwa wafuasi wa CCM na wanafunzi wasiounga mkono migomo. Wakati mwingine wanafunzi wanafanyiwa fujo kwa kuvaa sare za CCM na kuzuiwa kutoka maeneo ya vyuo kwenda katika mikutano.
  Kwa upande wa Mashina ya wakereketwa kumetokea malalamiko ya vijanakutotumika kwenye shughuli za kisiasa mpaka wakati wa uchaguzi. Pia kumekwepona malalamiko ya kukosekana kwa ufafanuzi punde chama au viongozi wakuu wanapokuwawamepakwa matope hivyo kuwafanya wafuasi wa CCM kuanza kuzomewa mitaaniwanakoishi kuwa wameshindwa kujibu.
  • Hii inawavunja nguvu wakereketwa wanapoambiwa kutokujibiwa malalamiko au matope yaliorushwa ni ishara ya ukweli.
  • Pia kimekosekana kitengo cha propaganda na kutawala vyombo vya habari hata vilivyo vya serikali kiasi kwamba hata panapokuwa pameandikwa habari ya CCM, wapinzani ndio wanakuwa wameiandika hivyo kuwa na madhara kwa Chama.
  Mapendekezo
  • Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu na ofisi ya mnadhimu mkuu ziongezewe nguvu ili zifanye shughuli ya kwenda hatua zaidi ya wapinzani kwa kuwa na watu wanaoshughulikia mambo haya. Vinatakiwa viwepo vitengo vya propaganda kwa kila ngazi viwezeshwe na kuratibiwa ili viende sambamba na matukio makuu katika kalenda. Kwa mfano maadhimisho ya CCM yawe na midahalo ya wana CCM, wanavyuo wetu na wananchi kwa ujumla, siku ya akina mama iwe na midahalo, sikukuu ya mungano iwe na midahalo na yafanyike maandalizi na fursa hizo zitumike kukosoa wale ambao wamekuwa wakileta lugha zenye madhara kwa hatima ya mungano nk.

  • Kuwepo na kikundi maalum katika ofisi ya umoja wa vijana na wabunge vijana kushirikiana na ofisi ya Chama taifa, ofisi ya waziri anayehusika na mahusioano na uratibu na mnadhimu mkuu kushughulikia kupangua hoja za kizushi za upinzani na kutoa mapendekezo staiki kuhusu kutengeneza mtaji wa kisiasa kwa makundi mbalimbali ya jamii.
  • Kikosi hicho kiimarishe mtandao kwa wanavyuo wanaomaliza masomo wajulikane walipo na ikibidi wawezeshwe ili wafanye kazi ya kukisemea vizuri chama popote walipo na wawe chachu pale mahali pa kazi walipo.
  • Kitengo hicho kiratibu midahalo na kutafuta wana CCM wanaoweza kuwa na majibu mazuri zaidi kulingana na uhusiano wa maada husika na utalaam na uzoefu wa msemaji anaestahili kushiriki
  • Kuhamasisha wana CCM kushiriki midahalo kwa njia za simu na wakati mwingine kuwaweka wana CCM kimkakati kushiriki mjadala hiyo tokea sehemu mbalimbali maada inapokuwa na mvuto wa kisiasa, masilahi ya kitaifa na chama chetu
  • Kupitia mwavuli wa Ofisi ya mahusiano na uratibu kitengo kiwe na uwezo wa kujibu kila hoja kwa kupata ushauri, majibu stahiki na makubaliano tokea kwa wataalam na wakuu wa wizara husika inayoguswa na agenda.
  • Kikundi kihusike na kutembelea wanavyuo na kufanya mawasiliano ya uamzi wa chama na makusudio ya serikali kutengeneza wasemaji wa agenda za serikali ndani ya jamii.

  • Kikosi hicho kishirikiane na wabunge wa kila jimbo kutembelea shule za sekondari kwani hao ndio wanavyuo wajao na wapiga kura wa uchaguzi ujao. Ni vyema pia ifanye mikutano ya hadhara nchini kote punde zinapotokea kauli za kukishambulia chama chetu. Wahusike wanachama, viongozi wa wilaya, mikoa na wabunge kukanusha na kulaani kauli za uongo. Hili liratibiwe na ofisi ya chama makao makuu, mikoa, wilaya, kata na matawi.

  • Kitengeneze utumiwaji wa wataalamu wa fani mbalimbali kufanya mawasilianao kwa njia ya SIMU NA INTERNET kueneza sera za chama na kazi za serikali.
  • Kuwepo muda maalumu na kikundi maalumu cha wabunge wa kuandaliwa kupeleka hoja au kujibu hoja watakaoweza kufanya hivyo kwa hisia za juu kuleta msisimko wa kisiasa na kuwapa moyo wana CCM pote walipowasiwe wanyonge.
  • Kutengeneza mtandao wahadhiri watakaokuwa wanakisemea vizuri chama mahali pakazi
  • Kufanya tafiti za siri kuhusu misimamo ya wateule wa nafasi mbalimbali kwa chama ili kuepuka hujuma na usaliti wakati wa uchaguzi.
  • Kukutana na viongozi wa kidini kuwaweka sawa na kutambua kuwa chama kinawajali na kujua umhimu wao katika amani ya nchi
  • Kukosi pia kitakuwa kinahusika kutengeneza mtazamo wa pamoja kuhusu jambo linalohusu nchi na kutafuta watu maeneo tofauti kulisemea jambo hilo, mfano mambo ya kuzingatiwa katika katiba mpya.
  • Kuanzisha ofisi, matawi na kuratibu upatikanaji wa wana CCM kushika uongozi kwenye serikali za wanafunzi.
  • Kuhusu vijana wa kwenye majiji na mijini na miji midogo wasio na ajira, wizara ya inayohusika na biashara na wizara inayohusika na vijana iangalie namna ya kutekeleza mpango maalumu wa kuwarudisha vijana walioasi chama kwa madai ya hali ngumu ya maisha.
  • Kwa mfano wizara husika zinaweza kufanya sensa na kupata idadi ya vijana wanaoweza kutambulika na kukopesheka halafu watafutiwe supplier maalumu aagize kwa jumla pikipiki na bajaji halafu zikopeshwe kwa vijana badala ya utaratibu wa sasa wanaoajiriwa na kupeleka hesabu kwa matajiri wao, wapeleke hesabu kwa supplier na punde deni likiisha pikipiki zinakuwa za kwao. Lakini mpango huo ufanyike kimkakati ili uweze kuleta manufaa kwa chama.
  • Mfano wa mkakati ni kwanza kufanyika kampeni ya kukaa vikao vya ndani na vijana kila miji watakao pata kwa kila awamu watakuwa chachu.
  • Mfano wa pili ni kuwakusanya vijana ambao wana ufundi wowote wawezeshwe halafu wafanye kazi na serikali. Kwa mfano wanaoweza kutengeneza madawati wajulikane watengeneze madawati ya shule zote za misingi, sekondari na vyuo kwa ushirikiano na serikali.
  • Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi uwahusishe wananchi ili waone vinavyofanyika pamoja na wabunge kutumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa kinachotekelezwa kilikuwepo kwenye ahadi. Kwa mfano vitabu visigawiwe kimyakimya kwa kuwatumia watendaji wa sekta ya elimu kuwakabidhi waratibu na waratibu kuvifikishia ofisini bali kuwe kunafanyika mikutano inayohusisha wanafunzi na wananchi ili wajue hatua zinazochukuliwa. Ifanyike hivyo kwa huduma za afya, kwa maabara, umeme n.k kwa kadri itakavyowezekana.
  • Hii itapunguza wananchi kudanganywa mathalani walikuwa wanaambiwa wao ndio wamejenga shule za sekondari za kata sio serikali ya CCM lakini ukweli ni kwamba mchango wa wananchi kwenye ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, zahanati na vituo vya afya ni maboma peke yake na mambo yote yanayosalia ni fadha za serikali. Utaona kuwa fedha ya serikali ni kubwa lakini kwa kuwa zinatoka kimya kimya kwa njia ya akaunti wananchi wakiambiwa wamejenga wanadhani ni michango yao imefanya kila kitu.
  "WE STILL HAVE THE CONTROL OF THE MATCH"
  MUNGUIBARIKI CCM
  MUNGUIBARIKI TANZANIA
  MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB)

  JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  kauli moja ya nchemba inafukuza wapiga kura 1000 wa ccm wenye akili timamu.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi mavi ukiya pulizia pafyumu nini hutokea...ccm tumewachoka mmetuibia vya kutosha na hatuoni wa kuibadilisha mavi kuwa mandazi..
   
 4. K

  Konya JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  "we still have the control of the match" bado hawajajua wananchi wanataka nini na sidhani kama huu mkakati utatekelezwa kama ambavyo wameshindwa kutekeleza ilani zao walizotuahidi kipindi cha uchaguzi
   
 5. r

  richone Senior Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  utapata mwingulu lameck Nchemba
   
 6. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...pole sana magamba huo ujinga wenu mnaofikiria kuufanya hauna nafasi hata kidogo kwenye kizazi hiki...hiki ni kizazi cha "DIGITAL" ambacho kinaji-set chenyewe sio kama kile cha wazazi wetu cha ANALOGY ambacho mlikuwa mnaki-set kadri mlivyokuwa mkipenda...kwa tahari tumekwisha wasoma,tunasubiri tu muda(2015) ufike tuwapotezee na tuwasahau kabisaaaaaaaaaaaaa!!!...
   
 7. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,570
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  RUBBISH!It culd ev bin pocbo zoz days bt NEVA NOW, 2meamka!CCM mme2pumbaza vya ktosha, mmeiba vya ktosha, mme2buruza vya ktosha!CC KA PUNDA 2nasema IT'S OVA, u must die ccm, u ev 2 go 2 ze hell ccm!KWISHNEI Nchemba + ccm yko nyau ww!
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wamekumbuka Shuka kukiwa tayari kumekucha, na hakuna mwana ccm alienauthubutu wa kufanya hayo
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kweli huyu Mwigulu naamini usomi wake una mashaka au asili ni mgomvi maana kuna vitu vya kuacha kabisa kuvitoa km nilivyoanza kumsikia huko Igunga na Arusha Masahariki inanitia wasiwasi,
  Huwezi kuiendesha nchi kutumia mitandao ya kijamii.
  issue nyingi za humu JF akishazitoa yeye (burn karudi) kesho yake lazima uisikie magazetini, au mtu kakamatwa na kupelekwa mahakamani na hili sms fake limeanzia humuhumu JF jana Usiku yeye na Nape wanautangazia umma.
  kweli atawaingiza wengi mkenge maana sasa anafuatia Nape kumwamini
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mtu mwerevu hawezi pingana na mageuzi ama kushindana na wakati. Enzi ya CCM kukaa madarakani imefika mwisho. Lazima wawepo watu kama Nchemba ambao watagoma kuuona ukweli,wana msongo wa mawazo!
   
 11. b

  beyanga Senior Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​kuna makaburu waliapa kuwa kamwe mtu mweusi hataongoza sa sasa ni haya ya ccm lakini hawana watu makini mwigulu,nape wasira komba maji marefu na mzee dhaifu kikwete
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Invisible
  Tafadhali nipe ruhusa nivunje moja ya kanuni za jf ili nipunguze ma-stress, na wala haitakuwa ajabu, tumemuona ndugai juzi kitalani,

  kumbe ndio maaaaana mikutano yake ya kirushwa rushwa anifanyia pale kanisani kkkt kyengeeege? Ni mkakati maalum eeeeh!

  Mkuu, uniwekee ruhusa kwenye inbox nimpopoe kwa matusi huyu alias mwigulu nchemba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. M

  Mohamed Ngwasu JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 304
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na ule utumbo wake wa safari hii bungeni amejimaliza na kukimaliza chama chake kabisa
   
 14. b

  bid2015 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu jogi yatapike tuu tuta'solve mbele kwa mbele.
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kesho watakuja kukanusha kuwa huu waraka umeandaliwa na chadema
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hapa mwigulu anachemka mno mfano;
  1. bado hajabaini kinacho waua kuwa ni , rushwa, ufisadi, utendaji mbaya wa viongozi wa chama chake amuulize Nape ili amupe story ya muuzaduka na mwenye duka - huwa sisahau!
  2. viongozi wa dini wakijiingiza kwenye siasa watafukuza waumini jambo ambalo hakuna hata kiongozi mmoja aliye tayari kulishudia
  3. mradi wa pikipiki utaleta lawama kubwa mno kama ilivyo kwa ruzuku ya mbolea
  4. vijana wa shule ndiyo wanao jiandaa kuwa maliza hasa wa shule za kata maana wamelundikwa ili wakue kwenye majengo hayo bila walimu, vitabu na hata maktaba au maabara - rejea kauli ya Mzindakaya alipo kuwa akiliaga bunge la 9
  5. hoja ya mwisho ukiitamtamka tuu basi utawafukuza hata wanaishi kwa matumaini ya 30% ndani ya chama - kumbuka watu wanachangia si chini ya tsh 10000/= per head
  6. waziri wa uhusiano akitumia tu mali ya serikali raia hawata mwelewa - kumbuka yaliyo mpata waziri huko Tunduma baada kutumia gari la serikali ktk kuzindua matawi ya chama
  7. hoja zako zote zina prove failure sijui kwa nini ??? hata ile ya kitengo cha propaganda ndiyo bomu kabisa ndiyo maana walifutilia mbali
   
 18. B

  Bubona JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Yes Nchemba, you still have control to those with suppressed thinking whose number is now tending to zero!!
   
 19. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama kuna fani inayomfaa Nchemba si nyingine bali upiga debe au hata ukora ukiachia mbali uzin... malizia.
   
 20. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  anasema wananchi wamechangia hela kidogo kwenye ujenzi wa sekondari za kata nyingi zimechangiwa na serikali!hajui kuwa hela za serikali zinatoka kwa wananchi kwa njia ya kodi!halafu anajiita mchumi daraja la kwanza!lameck mkumbo
   
Loading...