Huu ujumbe umfikie Kamanda Sirro, NECTA, TCU, Waziri wa elimu na idara zake kuhusu vyeti feki

Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
485
Watu wenye vyeti feki na watumishi hewa sio watu wa kuonewa huruma hata kidogo maana wamewasababishia vijana wasio na makosa kabisa ajira zao kusimamishwa, wailetea serikali hasara kubwa, wataalam feki, lakini pia wanatumia jasho la wenzao kujinufaisha nk.

Natambua kwamba kuna watu waliosoma nje ya nchi na wametoka huko na vyeti halali na pia ni watanzania halali. Hili ni jambo jema pale Mtanzania anapotafuta elimu ya ziada nje ya nchi kwa manufaa ya nchi na jamii kwa ujumla.

Lakini kitu kinachosikitisha ambacho, Kamanda Sirro, TCU, NACTE, Wizara ya Elimu nk wanapaswa pia kulivalia njuga ni vyeti feki na wafanyakazi feki toka nje ya nchi.

KUHUSU VYETI FEKI TOKA NJE IKO HIVI:

Ni muda mrefu Watanzania wengi wamekuwa wakinunua vyeti vya madaraja mbalimbali nje ya nchi hasa Kenya na Uganda nk, na hivi vyeti vikishafika Tanzania wanatumia yale majina kutengenezea vyeti vya kuzaliwa vya hapa Tanzania.

Sasa ili wasome vizuri na kujiunga na elimu ya Tanzania huwa wanapitia shule binafsi. Mfano cheti cha kidato cha nne cha Kenya kuwa wanatumia kujiunga na kidato cha Tano shule binafsi au vyuo mbalimbali na hatimaye wanajiunga na vyuo vikuu halafu kwenye mfumo wa ajira.

Suala hili limefanyika kwa muda mrefu sana na kuna watu kabisa wanahusika kama maajenti/mawakala wa kufata vyeti hivyo nje ya nchi au kuvitengeneza na cha kushangaza vyeti vya Tanzania ndio vinakaguliwa mara nyingi hivyo vinaachwa.

Vyuo binafsi vimekithiri kwa kusajili hawa watu wasiostahili na wanaficha kwasababu ni wateja wao kibiashara. Kitu cha kushangaza mtu hajawahi hata siku moja kwenda nje ya nchi, hajawahi kusoma kwa njia ya mtandao wala hajawahi kujiusisha na masuala hayo lakini ana cheti cha nchi fulani.

Ukimuuliza hata shule aliyosomea inapatikana wapi katika nchi hiyo hajui.
Hawa watu wapo wengi vyuoni, mashuleni na ikiwezekana serikali ianze kukagua shule na vyo binafsi wakati wa usajili wa wanafunzi. Hata shule na vyuo vya serikali wamo japo wanaogopa kwa kiasi ukilinganisha idara binafsi.

KUHUSU WAFANYAKAZI FEKI:

Kuna tabia nyingine pia imekithiri, Watu toka nje yq nchi wanakuja na vyeti vyao feki hapa Tz na kujiunga na mfumo rasmi wa ajira. Hili limekithiri hasa kwenye sekta ya elimu na viwanda. Mfano kwa sasa ukitokea kenya, Uganda, Nigeria nk na unajua kiingereza basi we ni mwalimu wa shule za english medium nk. Shule za binafsi imejaza wafanya kazi feki na wanafunzi feki kwa asilimia kubwa.

Tena hawa watu wanaheshimika sana na cha ajabu vyeti vyao hata kama ni feki huwa vinaonekana ni orijino tu kwasababu unakuta wakati mwingine wanaenda kwenye Taasisi fulani ambapo wanaokwepo hapo hawana uelewa kuhusu elimu na uhalali wa vyeti wa nchi husika.

Rai yangu ni Kuziomba idara husika mtoe tangazo ya kwamba kila mwenye vyeti toka nje ya nchi aviwasilishe vikaguliwe na aje na uthibitisho vinavyoonesha kwamba alisomea huko tofauti na kuonesha vyeti tu. Tunajua kwamba ukienda kusoma nje ya nchi lazima serikali iwe na taarifa, ufike uhamiaji na idara mbalimbali kabla kwenda huko kwa hiyo vitu hivyo vyote vichunguzwe na kuhusu wafanyakazi feki toka nje ya nchi na vyeti vyao, nao pia wakaguliwe wanatubania ajira bure wakati sio watu sahihi.

NB: Inauma sana mtu anapopitia njia zote halali za elimu na amefaulu vizuri lakini ajira yake inashikiliwa na watu feki wenye vyeti feki na ufaulu feki. Tena hawa wenye vitu feki ni wasumbufu sana maofisini na ni wababaishaji hata huko shuleni, vyuoni na kazini.

# TANZANIA NDIO DAMPO LA VITU FEKI DUNIANI
 
Yaani nikitaka kwenda kusoma nje hadi niruhusiwe na uhamiaji+necta?????? duh!! kama naenda mahakami kujibu mashtaka??? haaa haaa
 
Back
Top Bottom