ni kweli ndugu zangu, hata mimi niko West Africa jioni hii ilikuwa na wenzangu tukiangalia Al Jazeera, CNN, BBC, SABC, CTVV lakini niliambulia aibu! Unajua leo pia ni uchaguzi mkuu wa Cote d Ivoire huo unatangazwa kila mara na station hizi! Tanzania ziiii umeshindwa kuuza jina la nchi. We angalia hata wanapotangaza hali ya hewa, hutaona jiji la Dar-Es-salaam, Kigali, Bujumbura, Lusaka, Mogadishu, Nairobi, Bamako n.k. wapo! Sisi tupo tupo tu! Haki ya mungu ukitaja TZ wanamkumbuka Julius K.N.! Yaani Tanzania inakumbukwa kwa ajili ya Mwalimu na si kitu kingine chochote!