Huu si upupuu jamani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu si upupuu jamani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,031
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  HUU NI UPPUZI MTUPU;WAZIRI S.SIMBA ANADAI SERIKALI AWAWEZI KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA WA RADA MH CHENGE SABABU AWAJALETEWA TAARIFA ZA KAMA KUNA DENI WANADAI

  SIKIA HUYU MWINGINE NA VERSE YAKE;HAYA SI MAKANDE MATUPU INAAMAANA WAKATI HUYU AANATOA HOJA YAKE AKUWASILIANA NA FISADI SIMBA AMA!!!HII SERIKALI INASIKITISHA KILA WAZIRI ANAKUJA NA LAKE BADO MASHA WA MAMBO YA NDANI;SIJUI ATAKUJA NA LIPI;  SERIKALI jana imetoa msimamo wake kuhusiana na ‘chenji ya Pauni milioni 28’ ambazo zinatarajiwa kurejeshwa nchini na serikali ya Uingereza baada ya kubainika kwamba Kampuni ya British Aerospace Engineering (BAE System) ilifanya udanganyifu katika kuiuzia Tanzania rada.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha hizo zikirejeshwa zisipelekwe kwenye asasi zozote bali zirudi serikalini kwani zilikuwa ni za walipa kodi.

  Ingawa Waziri Membe alisema hadi sasa serikali haifahamu kiasi cha fedha zilizotajwa na Serikali ya Uingereza kwamba zitarudishwa nchini zipo taarifa kuwa Tanzania itarudishiwa Pauni milioni 28.

  Uchunguzi uliofanyika Uingereza kuhusu kashfa hiyo ya rada ulionesha kuwa Kampuni ya BAE Systems ilimlipa dalali zaidi ya Sh bilioni 12 kwa kufanikisha Serikali ya Tanzania kununua rada ya kijeshi kwa Sh bilioni 40.

  Kampuni hiyo ilikiri kosa na kuahidi kurudisha fedha Tanzania. Katika mazungumzo na waandishi wa habari Waziri Membe alisema ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada, inatarajiwa kufikishwa nchini wakati wowote kwa lengo la kutumiwa na serikali kuchukua hatua zinazostahili.

  Membe ambaye alikutana na mabalozi wa nje waliopo nchini na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo suala la rada na kuhusu uamuzi wa Bunge kufunga mjadala wa mkataba tata baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Richmond Development LLC kabla ya kuzungumza na waandishi, Membe alisema ripoti ya Serikali ya Uingereza kupitia Makachero wa Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ndiyo itakayoiongoza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukamilisha uchunguzi wake. Mkutano huo uliombwa na mabalozi hao.

  Alisema taarifa hiyo ndiyo itakayosaidia serikali namna ya kuhitimisha suala hilo katika utaratibu unaokubalika. “Tunasubiri ripoti. Tutatoa uamuzi kulingana na ripoti ya Uingereza,” Membe aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano na mabalozi hao na akasema ripoti hiyo ambayo serikali ndiyo imeifuatilia kufahamu yaliyomo, italetwa wiki hii inayomalizika kesho.

  Kwa upande wa Tanzania, Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah hivi karibuni aliwaambia waandishi wa Dar es Salaam kwamba uchunguzi unaendelea na akasema kwamba ofisi yake inasubiri taarifa rasmi na nyaraka kutoka SFO ambayo ilikiri kuwapo rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.

  Miongoni mwa wanaotuhumiwa katika suala hilo ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa wakati huo, Andrew Chenge na dalali, Saileth Vithlani. Katika hatua nyingine, Waziri Membe akizungumzia suala la Richmond, aliwaeleza mabalozi mchakato wote na namna ambavyo Bunge liliridhia kufunga mjadala kutokana na kuridhishwa na hatua za serikali katika kutekeleza maazimio ya Bunge.

  Mjadala ulifungwa katika Mkutano wa 18 wa Bunge ulioahirishwa wiki iliyopita. Aliwaambia kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikugawanyika nchi nzima isipokuwa waliokuwa wamegawanyika ni wabunge juu ya suala hilo la Richmond.

  Alisema hata hivyo suala lenyewe pia limekwisha na kilichobaki ni serikali kukubali changamoto ya kutekeleza mambo yaliyobaki kulingana na maazimio ya Bunge. Kuhusu rushwa, Membe aliwaambia mabalozi hao kwamba vita dhidi ya ufisadi inafanyika nchini kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

  Alisema katika kuonesha kuwa serikali iko makini katika hilo, zipo kesi mahakamani na nyingine uchunguzi wake unaendelea. Katika hatua nyingine, Membe amewafahamisha rasmi mabalozi wa nje kwa kuwataka wenye nia ya kufadhili vyama au wagombea binafsi katika Uchaguzi Mkuu ujao, wawe tayari kutangaza fedha watakazotoa na malengo yake ni nini kwa kuzingatia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2009 ambayo inasubiriwa kusainiwa na Rais baada ya Muswada wake kupitishwa bungeni hivi karibuni.

  Vilevile aliwaeleza mabalozi uamuzi uliofikiwa wa kuwepo Serikali Shirikishi Zanzibar. Alisema kwa kuzingatia uamuzi wa Butiama, kutakuwa na makamu wawili wa Rais; mmoja akiwa ni wa chama kilichoshinda na mwingine kutoka chama cha upinzani.

  Aliwafafanulia pia suala la mgombea binafsi kwa kuwaambia Serikali haina pingamizi kuwepo isipokuwa suala hilo haliwezi kutekelezwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa kuwa linahitaji mabadiliko ya Katiba.

  Kwa upande wake, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ((DRC), Juma Mpango ambaye ni Mkuu wa Mabalozi Nchini, alishauri Waziri Membe aweke utaratibu wa kukutana nao kila mwezi kwa lengo la kufahamishwa mambo mbalimbali yanayojiri kuliko kuegemea taarifa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...