Huu ni wizi au ufisadi?

kiboksi manyoya

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
377
311
Unapoamua kumsaidia mtu, msaidie kwa moyo wote sio unajifanya unasaidia kumbe ndani ya msaada kuna maslahi binafsi.

Shemeji yenu ni mwajiriwa katika haya majeshi yetu ya ulinzi, juzi amekuja na tracksuit fulani ambayo ni miongoni mwa mzigo niliowauzia jamaa fulani kwa bei ya jumla tshs 30,000/=. Nilipoiona tu nikashangaa na kumuuliza hii tracksuit umetoa wapi? Jibu lake ni kwamba wamelazimishwa kazini kwao kuchukua hizo tracksuit kwa malipo ya tshs 69,000/=.

Toka tshs 30,000/= hadi tshs 69,000/=, hii ni halali kweli?
5c01bf8d0c65b10573bade63995f3c46.jpg
c9d2c4cf5ac57eb81ecd423802c77736.jpg
07d86baff2633bd90b15b868548bc529.jpg


Je jeshini kuna utaratibu wa kumlazimisha askari kununua kitu anachouza bosi wake? Naomba mhe mkuu wa majeshi iangalie pale Kigamboni nahisi kuna jambo linaendelea.
 
mbona mwanzoni umetoa rai kuhusu msaada, halafu mkasa wa shemeji wako wa kuuziwa kwa bei ya juu?
anyways, mkuu wa majeshi naamini atasikia rai yako!
Yule wa magereza alishajiuzuru mra baada ya makorokocho kama haya..
 
Yule wa magereza alishajiuzuru mra baada ya makorokocho kama haya..

yule alikuwa amepitiliza umri wa kustaafu kama ilivyokuwa kwa afande kova....
alifanya jambo zuri maana madaraka yangemponza na mafao ya kustaafu asingepata kisa sare..
 
Back
Top Bottom