Zacharia Kifyasi
Senior Member
- Dec 23, 2012
- 135
- 24
Nina mpenzi wangu (mjita) ambae nimedumu nae kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa, tunapendana sana kwenye shida raha kwani ameridhika na hali yangu ya kimaisha! Alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi hapa dar, lakini miezi miwili hivi iliyopita aliamua kuacha kazi kwa madai kuwa haina maslahi hivyo akaniambia anaenda kwa wazazi wake Morogoro, anaenda kutulia nyumbani.
Hapa ninapo kaa niko karibu na dada yake ambae amepanga jirani na nyumba ninayo kaa,. Huyu dada yake ana house girl. Tatizo ni kwamba huyu house girl akipita nyumbani nikapiga nae story mbili tatu huyu dada mtu ana mpigia mdogowake simu kuwa naongea na house girl wake, baada ya hapo mpenzi wangu anacharuka na kutishia kwamba tuachane. Hapa nimechoka nikiangalia hapa nyumbani ndio njia ya huyu house girl kupita, sasa nisioongee nae jamani kisa ntamtongoza? Wadau huyu dada mtu mwenyewe ana mimba kubwa yani nashindwa hata kumfuata kumweleza upuuzi wake!