Huu ni wakati mwengine na CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni wakati mwengine na CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 13, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ulikuwa bado unaburuzwa na vyama vingine visivyo na msimamo basi hujachelewa ,Hapa Tanzania kipo Chama kimoja tu ambacho ndicho Chama ambacho kila Mtanzania anatakiwa ajiunge nacho na kuendeleza upinzani wa kweli dhidi ya serikali iliyopo madarakani ,ukweli huu umeonekana huko Pemba na karibu utajitokeza na Unguja ,kuweza kufikia kuzuia uandikishaji wa wapiga kura hewa ,umoja uliopatikana Pemba ndio umoja unaoogopwa na utawala wa CCM kutokea hapa Tanzania,kiasi cha kuifanya serikali ya Kikwete isijue inafanya nini ,ilianza na kupeleka mapolisi kibao ,ikafuatiwa na kupelekwa majeshi na vifaa vya kivita ,kumbuka chaguzi zilizopita walionekana majeshi wakiwa na marocket launcher ,leo mambo yamezidi wameongezea na vifaru ,fikiria hiyo ni Pemba tu peke yake inauhangaisha utawala wa CCM ,je ikiwa upinzani uliopo Pemba utaenea Tanzania nzima ?

  WaTanzania ninawaeleza kuwa hakuna na hatuna haja ya kuwa na misusuru mirefu ya vyama vya upinzani ,ni lazima tuelewe kuwa misururu hii inaletwa na huyu Sultani CCM ili kuwagawa wananchi katika makundi makundi na hivyo kusababisha kuzigawa kura za wananchi walio wengi.

  Ndugu waTanzania ni lazima tuone ukweli na tuukubali kuwa Chama cha kweli cha Upinzani Tanzania ni CUF ,mbinu zinazofanywa na Chama tawala kukidhoofisha Chama hiki ni kubwa sana na CCM inatumia mabilioni ya fedha katika kuhakikisha kuwa kinafanikiwa lakini msimamo ambao unatokana na idadi ndogo ya WaTanzania unasababisha kushindwa kwa mbinu za CCM katika kuimaliza CUF ,msimamo huu bado unahitajia WaTanzania wengine kujiunga nao katika kuelekea safari ya kujikomboa kutoka kwa utawala wa Sultani CCM.

  Tusikubali maneno yanayosemwa kuwa CUF kina nguvu zaidi Pemba,hilo halina ukweli ndani yake ni kutaka kuzidisha hila za kuwafanya WaTanzania waamini kuwa CUF ni chama cha upande mmoja au ni Chama cha watu fulani tu ,waPemba ,kauli hizo ni nonesense na kila Mtanzania mwenye akili timamu inafaa azitupilie mbali.

  Ni Mtanzania gani ambae ana akili timamu utamuaminisha kuwa CUF haikupata mbunge hata mmoja katika uchaguzi mkuu uliopita hapa Tanzania ? Hila na njama ambazo ziliwagusa viongozi wakuu wa vyama vingine ambao walipiga kura na kujipigia kura ,hawakuziona hata ile kura ya mtu na mkewe zilipokwendea ,na hivyo ndivyo ilivyofanyiwa CUF kwa ujumla ni jambo ambalo lipo wazi kabisa ,kuwa mbinu za CCM ni kubwa sana juu ya kuona CUF haipati mbunge hata mmoja na wale wengine wanaopata huwa ni kama ruzuku inayotolewa ili kuwaziba macho wananchi. Ukweli ni kuwa matokeo ya uchaguzi mzima ni ya kupanga. Na kule ambako wananchi wamesimama kidete upangaji haukuwezekana.
  Nani anaweza kuamini kuwa Lipumba alishinda uchaguzi Mkuu uliopita hapa Tanzania ? Inakuwa ni vigumu ndivyo ilivyofanywa iwe na ionekane hivyo kuwa hakushinda na chama chake hakikupata hata mbunge mmoja hapa Tanzania Bara ,ni hujuma nzito sana iliyofanywa ambayo inaweza kuiweka nchi matatani kwa siku zijazo ,maana watu wakiwa na msimamo kama uliopo Pemba wa kupinga kudhulumiwa haki yao na kuburuzwa ,inakuwa ni hatari sana.

  Hivi sasa kuna mambo yanakuwa twisted ,kuna mambo ya muungano sijui mambo ya mafuta ,tunaona malumbano kati ya viongozi wa CCM bara na wenzao wa CCM visiwani ,hapa hamna lolote ni mchezo wanawachezea waTanzania ,ni lazima mulielewe hilo ,hawa watu kuwepo madarakani wanategemeana kwa asilimia mia moja ,hivyo hawawezi kuwa wapumbavu wagombanie au wagombane kwa mafuta au mambo ya Muungano ,hayo hayawezi kutokea na kutekelezeka ndani ya Chama kimoja cha CCM ni ulaghai mkubwa usiowahi kufanywa na kufanyiwa wananchi ,kwa lugha nyingine panafanywa usanii.

  Matokeo yake ni WaTanzania bara kuona WaZanzibari wanauchoyo na WaZanzibari kuona wajamaa wanataka kutumeza ,hapa hakuna kitu ila ni game played by CCM ,ukiangalia utaona CCM wanajipandisha chati kwa kujionyesha kuwa wataulinda muungano na pia mafuta na gesi yapo chini ya Muungano na serikali ya Mapinduzi haina ubavu sijui na hili na lile ,wakati wale wa zanzibari nao wanatingisha kuwa mali ya Zanzibar ni kwa Wazanzibari ,maigizo yote hayo bado Mtanzania unaona kweli sasa sio mchezo WaZanzibari hawatuchezei na wale wenzangu mie kule Zenji nao wanaona na kuambiana unasikia umeona Waziri alivyosema wabara hawayajui Mapinduizi waache watuchezee tu, jamii nzima inapindishwa na kuwekwa katika makundi mawili ambayo yote ni CCM ,hivi unategemea nini ?

  Ni lazima tuamke ili kuepuka siasa hizi anazotupeleka Sultani CCM ni lazima tuiunge mkono CUF ili turithi mapambano yalioanzshwa na WaPemba ,mapambano ambayo yanatakiwa kuungwa mkono na WaTanzania wote chini ya bendera moja ya CUF na si vinginevyo.

  Pemba kwa walipofikia ni pakupigiwa mfano na wamefanikiwa kutoa tension kwa maTaifa ya nje na hata kufikia kwa EAC kusema inaweza kuifukuza Tanzania katika umoja huo ikiwa itaonekana inavunja haki na misingi ya demokrasia na inaangaliwa namna mambo yanavyotokea Pemba ,kwa vyovyote vile naweza kusema Jakaya Mrisho Kikwete yupo matatani na huo ndio ukweli.
  Itakuwaje ikiwa WaTanzania wote watakuwa na msimamo kama waliokuwa nao watu wa Pemba ? Pemba mambo ni makubwa kulivyo yanavyoripotiwa tulisikia kuwa waandikishaji wa wapiga kura wameondoka kutokana na fujo ukweli ni kuwa WaPemba wamesusia kwenda kuandikisha baada ya kuona hila zinazofanywa ni mbaya na hazina mshiko zaidi ya ubabaishaji wa CCM,imebidi kambi za kuandikisha zifungwe na weshasema haendi kuandikisha mtu kama kila aliefikia umri wa kupiga kura amekubaliwa kuandikwa bila ya kipingamizi chochote kile.
  [​IMG]
   
 2. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kuna msururu wa vyama vya upinzani vya siasa nchini Tanzania, lakini hatuoni matun d a yake. Nimekuwa nikiwalaumu watanzania katika nyaraka nyingi sana na hata kujisahau kama mimi mwenyewe ni mtanzania vilevile.

  Licha ya kuwa na ufisadi wa kupindukia na nchi kutawaliwa na rushwa huku watanzani wenyewe ndio tunaoumia. Lakini cha ajabu bado watanzania tumeikumbatia CCM kama vile mtoto mdogo aliyefahamu kuwa chakula ni ziwa la mamake tu.

  Pemba wameshatuonyesha mfano ni vipi wananchi wasiozidi laki 4 wanaweza wakatoa ujumbe mkali kwa viongozi wa serikali (ccm) mpaka wakakubali kuketi chini na wapinzani wao. Lakini kwa vile wameona wafuasi wa vyama vingine hawajatoa ushirikiano wa kutisha katika kulilia haki zao za msingi basi wakapuuzia. Fikirini kama wakati huo tungejiunga na wanaPemba kuishinyikiza serikali ili ifanye chaguzi zote kwa haki na uhuru, basi leo si CUF peke yake ambayo ingefaidika bali ni vyanma vyote pinzani au vya kisiasa. Lakini upofu na ubinafsi wa watanzania ndio uliotufikishsa hapa tulipo.

  Pamoja na kwamba ndani ya CCM wabunge wake wameiga sakata dhidi ya wafuasi wao madhalimu na mafisadi, lakini bado haitoshi, kwani kinachohitajika ni mabadiliko ya chama na viongozi wawili watatu kuchez michezo ya kuigiza na kuwashutumu wenzo. Na hili haliwezekani mpaka pale watanzania wataposema HAPANA , HAPANA, HAPANA, HAPANA!!!!!!!!!!!!

  Tuige mfano wa CUF kama kweli tuko makini katka kupambana na ufisadi na rushwa. Lilokaribu zaidi ni kuiunga mkono CUF iingie madarakani, hii ikiwa kama , mbinu ya pamoja ya kuingoa CCM milele.
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  CUF kwa Bara ni kama wamekufa aisee,yaani wamefuliaa mbaya
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Una uhakika gani kama CUF wanapambana na ufisadi na rushwa? Au wana lao jambo!
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Sio wamekufa ni strategy ya CCM 2005 kutowapa kiti hata kimoja cha ubunge ili kuwafunga Spidi gavana. Ninakuambia kuwa 2010 zamu ya CHADEMA kupoteza wabunge wake. Haiingii akili Lipumba 2005 kupata 10% ya kura za urais na kushika nafasi ya pili wakati katika ubunge CUF wasipate kiti hata kimoja?. Sasa hii itatokea 2010 upande wa CHADEMA.

  Kila siku huwa nasema Tanzania hatuna demokrasia katika uchaguzi wa viongozi bali tuna michezo ya kuigiza. Ni mpaka hapo yatokee yaliyotokea sehemu nyingine katika kudai Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na vyombo vya usalama kuwa free na professional badala ya kuwa kama mbwa wanaosubiri amri ya kuuma toka kwa bwana zao.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Second step naamini kabisa Pemba itapambana na serikali ya Sultani CCM kudai KATIBA MPYA iwe ya Muungano au ya Zanzibar ,kusema kweli WaTanzania ni lazima ikifikia hapo basi kama hakuna wa kuwaunga mkono na kulipandisha chati dai hilo basi bora mkubali kuwapa kipande Chao au kwa upande mwingine itakuwa hakuna haja ya kuwepo na malalamiko ,kuwa Katiba inavurugwa ,uchaguzi ni wa uongo uliojaa maruerue na mauza uza ,vita vya ufisadi ni kiini macho au mazingahombwe ,kusema ukweli watu waPemba wanatuhitajia sana sana na njia wanayoionyesha ndio demokrasia halisi tunayoitafuta hapa Tanzania na ndio jambo kubwa ambalo limemfanya Sultani CCM kupeleka majeshi mapema huko ili kujaribu kuzima ,kinachohitajika hapa ni uungwaji mkono na WaTanzania wote kuwa kitu kimoja ili kupinga mbinu za Sultani CCM kutaka kuibana demokrasia na hapa ifahamike kuwa anaitumia Pemba kutaka kuwatisha WaTanzania wote ,tunasema kuwa ushirikiano na umoja ndio utakaowezesha mapolisi na majeshi kujitenga na na kukataa kufanywa watumwa na Chama Cha machinjachinja.
  Nasikiliza kwa hamu hatua ambayo CHADEMA wamefikia kuichukua ,je hatua hii itafuatiliwa na kuwashawishi WaTanzania nzima kuhusiana na ubakwaji wa demokrasia na hivyo kuamuru kuanzisha harakati za nchi nzima katika kuuunga mkono mapambano yalioanza Pemba katika kupambana na kupinga hila za CCM ambazo wanafikia kutangaza hadharani kuwa wana mbinu nyingi ,tunachokisema ni kuwa mbinu zao zinaonyesha kugonga ukuta mbele ya wananchi wa Pemba ,msimamo ambao unabidi uenee Tanzania nzima msimamo ambao utapelekea majeshi ,mapolisi na vyombo vya usalama kujitenga na siasa.

  Huu si wakati wa kuwabeza wananchi wa Pemba ikiwa Jumuia ya East Afrika na Jumuia za Ulaya zimeonyesha kwa uwazi kabisa mambo yanayofanywa Pemba na mtawala aliekuwepo madarakani si ya kuyapuuza au kuyafumbia macho ,mchana kweupe Sultani CCM amesomewa barua yake ,kinachohitajika ni kuionyesha dunia kuwa haya mambo hayafanwi Pemba tu bali uovu wa CCM umeenea Tanzania nzima ,hali hiyo itatokea ikiwa tu na WaTanzania wengine wataamka na kusimama kidete katika kulinda haki yao ya kidemokrasia hali ambayo itamtoa nduli pangoni na kuonyesha rangi zake halisi kama anavyozionyesha huko Pemba.
   
 7. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  This is delusional to say the least

  Tafadhali toa sababu kwa nini mpiga kura aunge mapambano chini ya bendera moja ya CUF pekee?

  ,

  You don't say
   
Loading...