Viongozi wengi tu wanafahamu lugha ya Kiingereza ikiwemo Gaddafi, Sarkozy, Putin, Kikwete n.k
Ila tofauti na Mh. J. K. Kikwete viongozi wengine hujisikia ni vizuri kuongea ktk lugha-mama zao kama Ki-Arabu, Ki-Faransa, KiRusi n.k kwa kuwa wametumwa na wananchi wao, hivyo ni haki wananchi wao waelewe kiongozi wao anaongea nini na 'wageni'.
Sisi Tanzania labda kwa kutaka siri / kujionyesha-'umekwenda shule' ndo maana viongozi wetu wanattumia lugha ya kigeni kuongea na 'wageni' wakati ni sisi ndiyo tumempeleka kwa kodi zetu hivyo si haki viongozi wetu wa Tanzania kutuacha solemba kwa kuongea kwa lugha za kigeni wakiwa ktk nyadhifa tulizowapa na kuwagharamia kwa kodi zetu.
Pia kwa kutumia mkalimani hutoa nafasi viongozi kuwa na muda wa sekunde/dakika kadhaa za kufikiria nini aongee, atamke. Lugha ni nyenzo muhimu ya kuonyesha uzalendo na mapenzi kwa nchi yako, hilo viongozi wetu wanatakiwa kulielewa.