Ni aina mpya ya utapeli. Nilipigiwa simu na mtu aliyedai ni mwalimu wa shule ya mwanangu akajitambulisha anaitwa Mwl. Fredrick,na kweli shule hiyo ina mwalimu mwenye hilo jina,akasema mwanangu amepata ajali amegongwa na pikipiki wamemkimbiza hospitali na anatakiwa kuongezewa damu haraka sana hivyo nitume elfu 50, nilipata mshtuko uliochanganyika na bumbuwazi,nikawaza kukimbia hosp lakini ni 30km kutoka hapa,nikapata wazo nitume kwanza hiyo pesa mtoto awekewe damu nisimpoteze mwanangu. Kabla sijatuma akili ikanijia, msaidizi wa mwalimu mkuu ni rafiki yangu,kwa nini hakunipa taarifa mpaka wampeleke hosp mbali hivyo wakati kuna hospitali kubwa private hapa jirani...nikasema ngoja nimpigie,nimemsalimia akaitikia kwa bashasha kuonesha yuko okay hakuna jambo la hatari,nikajiambia labda hata taarifa za ajali ya mwanangu,nikampa pole nikamuuliza imekuwaje wampeleke mtoto hospitali mbali badala ya kumpatia huduma za haraka hapa jirani akashangaa akaniuliza mtoto gani, nikamwambia taarifa niliyopewa kuhusu ajali ya mtoto, akacheka sana..daaah...akaniambia umeshaliwa,nikamwambia sijatuma ndio niko kwenye mchakato akaniambia wewe ni mazazi wa pili unapewa taarifa kama hii ila mwenzako ametapeliwa na pesa akatuma .
Nilichoka sana, baadae wananipigia wananiambia niharakishe nikawaambia simameni hapo hapo subirini pesa, wakanitukana mngese sana wewe wakakata simu.
Jamaa wanashtua sana hawa.