huu ni utapeli au?

nyauvi

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
10
Reaction score
1
habari za siku wanajamii forum wenzangu,mimi ni mwanamke niliyedumu kwenye ndoa kwa muda wa miaka 9 mpaka sasa,imetokea kuona mesage kwenye simu ya mume wangu zikiwa zimeandikwa kwenda kwa mdada anayefanya nae kazi nyikngi ni za kumjulia hali na kumtakia mchana mwema.ila huwa akishachat na huyo dada huwa anadelete ili hata kwa bahati mbaya nisizione.bahati nzuri siku akasahau nikaziona kama tatu hivi.kumuuliza anasema alikuwa anafanya hivo kunirusha roho, je huu ni ukweli au ni wizi mtupu?tafadhali nifafanulieni?
 
Muulize mumeo, sasa unatuuliza sisindio tumekuoa??? Hahahahaaa just kidding
Ok ok ongea nae mmalizane, hawezi kukurusha roho kwa style hio bhana
 
Usipanic sasa! Hapo cha kufanya ni kuwa makini zaidi! Kuwa makini namatendo yako pia manake sometimes mtu anaweza tafuta demu sio kwa ajili ya kumgegeda ila kujihisi yuko sawa katika mahusiano hasa mahusiano yake ya wakati huo yakiwa mabaya!

So muhimu kuwa more alert na nyendo zake/zako! Manake anza kumkimbiza mwizi kimyakimya! yaani mpaka umkamate au la ajisalimishe polisi!
 
Unataka kunambia huna teknik kabisa zakike kufahamu kuwa mumeo anakutapeli au anakujaribu? Wake up woman!! Usiruhusu shetani nyumbani kwako!!
 
Ni mara ngapi ww huwa unamkumbuka mume anapokuwa kazini hata kumuuliza tu umekula mume wangu, umekula nini na kumtakia kazi njema au akitoka tu home kwako ndo nitolee hiyo kuonana usiku
 
Si ukweli ni wizi mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…