Huu ni Ujasiri wa kijinga

Huu ni Ujasiri wa kijinga

Tarehe 23 mwezi aprili mwaka huu majira ya saa mbili usiku nilipokea ujumbe wa maandishi katika simu yangu kutoka kwa jamaa yangu mmoja akinishtua niangalie habari katika chaneli ya ITV. Wakati huo mimi nilikuwa naangalia katika chaneli nyingine. Bahati mbaya sikuweza kukiona kipande cha habari hiyo.

Hamadi!! Nilifanikiwa kuiona habari hiyo, ingawa nilichokiona sikuamini macho yangu. Nilidhani naota. Siku ya pili yake ilinibidi niingie katika youtube ili kuthibitisha kile nilichokiona kama ni kweli au zilikuwa ni ndoto.

Habari niliyoiona iliniumiza sana kana kwamba ni mimi ndiyo nilitendewa kitendo kile. Nilishuhudia kijana mmoja anayeonekana kuwa na akili timamu kabisa akimkunja askari wa usalama barabarani aliyekuwa akitimiza wajibu wake na kumnyang'anya ufunguo wa gari.

Kitendo kilichofanywa na kijana Yule ambaye sijui nimuite kwa sifa ipi ili imfae ni cha udhalilishaji wa hali ya juu kwa binadamu na kwa jeshi la polisi kwa ujumla wake. Nilitafakari na sikupata jibu. Ni nani asiyejua umuhimu na unyeti wa jeshi la polisi katika uhai wa jamii yoyote ile. Ni nani anayeweza kushabikia pindi anapoona jeshi la polisi linagaragazwa?

Katika siku za hivi karibuni vitendo vya kuwadhalilisha polisi na jeshi la polisi vimekuwa vikiongezeka sana. Miaka michache iliyopita, mfanyakazi katika ubalozi wa nchi moja ya Ulaya alifikia hatua ya kumtemea mate askari wa usalama wa barabarani kwa kuwa tu askari huyo alimsimamisha baada ya raia huyo wa kigeni kwenda kinyume na sheria zinazoongoza matumizi ya barabara. Si hayo tu, bali pia mwaka 2010 tulishuhudia mgombea mmoja wa ubunge akimkata mtama mkuu wa polisi wa wilaya moja katika moja za wilaya hapa nchini.

Ni vigumu sana kupita mwezi mmoja kama hujasikia askari wa polisi ameshambuliwa na watu wakati akitimiza wajibu wake. Wapo wanaouawa na mbaya zaidi wananchi wanathubutu hata kuvamia vituo vya polisi na kuvichoma moto.
Tumeshuhudia kuchomwa moto kwa kituo cha Hedaru ambapo mali na nyaraka za serikali ziliteketezwa, lakini pia tumeshuhudia mauaji ya askari wakiwa wanatekeleza kazi zao. Wananchi pia walimuua askari mkoani Tabora mwaka 2011 wakati akiwa katika operesheni ya kuteketeza mashamba ya Bangi.

Huwa najiuliza, je ujasiri huu wa raia katika kuwadhalilisha polisi, unatoka wapi? Inakuwaje kila anayesaka umaarufu mbele ya watu basi hakuna pa kuupatia zaidi ya polisi? Ukienda katika mikutano ya wanasiasa, ni vigumu kukuta mkutano umemalizika bila kuwatupia madongo polisi. Wasanii hasa wa vichekesho (comedians) huwa hawaamini kama kazi yao imekamilika kama hawataweka kejeli kwa jeshi la polisi.

Udhalilishaji huu kwa sasa unachupa mipaka hadi sasa vibaka nao, wanadhani wanaweza kuwachezea polisi.
Tunaweza kutafakari kwa pamoja. Kama inatokea mtu mwenye akili timamu anaweza kumdhalilisha askari mwenye sare kwa kumkunja mchana kweupe mbele ya kadamnasi, atashindwa vipi kumpiga na hata kumchania sare au kumnyang'anya silaha pale atakapokutana nae vichochoroni?

Lakini pia, tunaweza kujiuliza! Kama anaweza kumkunja polisi namna ile, je ikitokea amekasirishwa na raia mwenzake atampa adhabu gani?

Cha ajabu ni kuwa, watu hawa wanaolidhalilisha jeshi la polisi, wanashindwa kufahamu kuwa ujasiri wote walionao unatokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi katika kuhakikisha kunakuwepo na amani na usalama katika nchi yetu.
Watu hawa wanadhani vitendo wanavyovifanya kwa askari wetu labda vitawajengea woga katika kutimiza majukumu yao. Wanasahau kuwa hizo ni changamoto katika kazi na kwamba vitendo hivyo ndo vinajenga na kuamsha ari ya askari katika kupambana na uhalifu wa aina yoyote katika jamii yetu.

Wanasahau kuwa kama usalama usingekuwepo, inawezekana hata huo muda wanaoutumia katika kuwadhalilisha askari na jeshi zima la polisi wasingeupata.

Baadhi yetu wananchi hatuelewi dhana ya polisi jamii na pia dhana nzima ya Utii wa sheria bila Shuruti. Tunadhani, Utii wa Sheria bila Shuruti kunatokana na polisi kushindwa kutumia maguvu. Uhuru tunaopewa na jeshi la polisi tunautafsiri kama uoga na kushindwa kutimiza majukumu kwa jeshi hilo.

Tunasahau kuwa lengo la utii wa sheria za nchi bila shuruti ni kupunguza uhalifu na matumizi ya shuruti katika usimamizi ya utiifu wa sheria za nchi. Lakini pia utaratibu huu pia unasaidia kupunguza gharama katika oparesheni za kupambana na uhalifu.
Watu hawa wanapendelea jeshi la polisi linalotumia maguvu kama polisi wa kikoloni, ambapo polisi na raia walikuwa na mahusiano ya kiuadui. Raia alipokuwa akimuona polisi hata kama hana kosa, alikuwa akitimua mbio.

Askari naye ni binadamu. Anatakiwa apewe haki zake zote na heshima yake kama binaadamu. Kumdhalilisha askari ni kuidhalilisha serikali.

Binafsi nimekuwa nikifuatilia sana ripoti za kituo cha Sheria na haki za binaadamu (LHRC). Katika taarifa zake za haki za binaadamu, sijawahi kukuta mahali walipoelezea ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na wananchi wakora kwa askari wetu. Swali za kujiuliza ni hili! Je, hawaoni ukiukwaji wa haki dhidi ya polisi? Au wanaona lakini wanafumbia macho ili polisi wachukue hatua katika kujihami na wao wapate cha kusema?

Wanaharakati ambao ninaamini kwa sauti waliyonayo wanaweza kukemea utovu wa nidhamu unaofanywa na raia dhidi ya askari. Watumie nafasi waliyonayo katika jamii katika kuhakikisha kuwa wananchi, wanaheshimu sheria kwa kuwaacha askari na watumishi wengine wafanye kazi zao walizokabidhiwa na umma.

Nimalizie makala haya kwa kuwaomba askari wasifadhaike kwa matukio yanayofanywa na raia wachache wasiothamini kazi nzuri ya polisi. Endeleeni katika kuilinda nchi yetu. Sisi raia wema tunathamini na kuijali kazi yenu. Zidisheni mapambano dhidi ya wahalifu popote pale walipo bila woga wala huruma. Pia niwapongeze askari wetu kwa uvumilivu mkubwa walionao, hii ni ishara kuwa wamefunzwa na wameiva. Na kwamba wapo tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayojitokeza kwao kwa sura yoyote ile.

Mkuu yawekana askari aliyefanyiwa vile nduguyo nini?.
Naona umepoteza muda wako mwingi kuandika ----- huu.Hivi unajua ulevi mkubwa wa mamlaka uliowakumba Askari wengi bila kujali ni Polisi au JWTZ.

Ebu chukulia mfano mdogo wa barabarani .Trafic anakusimamisha na unasimama lakini hata kabla kukueleza kosa yako anaanza kukimbilia ufunguo wa gari au Pikipiki ndiyo anaanza kuorodhesha makosa ya kutafuta.Katika mazingira kama haya unategemea nini?

Kama umojawao nakushauri upeleke elimu kuwa wanafaa kuwa heshimu waendesha magari au chombo chochote kilichopo barabarani na hao ndio wateja wao.Nenda vivijini kama utakuta Trafic kwanini? Tafuta jibu.
 
Ndugu mleta mada umekuza sana! Hadi nikadhani kuna mtu kachinjwa hadharani. Yule askari ni DHAIFU mno kiasi kwamba alionekana kuumia kwa kushikwa tu vile. Wala jamaa hakuwa na nia ya kumdhuru afande ila nguvu zake tu ndio zilimponza. Ila ndio hivyo, tuheshimu vyombo vya Dola
 
...kunatofauti kubwa sana kati ya utawala wa sheri na kutawala kwa sheria...
 
Mleta mada pole kwa kukwazwa na tukio hilo lakini kwangu mie wala sioni jambo la ajabu kwani nilisha nyanyaswa na hawa polisi uchwara ambao wao kitu logic ni kama msamiati. Nimeshuhudia rafiki yangu akichezea kichapo mpaka kuvunjwa taya bila sababu zozote za msingi na nikatoa ushahidi polisi jinsi ambavyo askari huyo alivyo kuwa amelewa na anatutishia kutulipua kwa bastola tusisogee. Report akifika mpaka kwa mkuu wa kituo na kilichotokea ni maajabu ya musa na filauni kwa polisi huyo bado yuko kazini na inavyosemekana mkuu aliwaweka chini wayamalize. Huwezi kunishawishi niwe na sympath ya aina yoyote juu ya watu hawa maana wao wanaamini kuwa wapo juu ya sheria na hawawezi kukukamata bila kukupa KICHAPO pia ndugu tambua 70% ya askari wetu IQ zao ni ndogo mnoo kufanya judgement ya kawaida katika shughuli zao maana elimu yao ndogo na wengi ni kamlete na hata walioko ni kwa sababu hamna ajira ila si kwa ajili ya kuitumikia jamii
 
Vipi unaweza kumtetea na huyu au na kwakuwa kafinywa ASKARI mwenzio basi kelele keleleee!
attachment.php

View attachment 92319
hii ndiyo the other side of ''polisi jamii''
‪Traffic Police akichapana makonde na dereva wa basi‬‏ - YouTube
 
silaumu sana raia wanapofikia hatua hiyo.pengne mleta hoja ULIDHAN HIYO NI HAKI YA POLICE KUTENDA HAYO,YAAN KUDHALILISHA RAIA,KUWABAMBIKIA KESI,KUWANYANYASA.watu wamechoka kuna kipind hata mimi huwaza hata kumgonga traffic ambaye kwa makusud kabisa anawaweka kwenye folen dakika 40 Kwa vile dereva taxi mbele alipiga horn.kwa hiyo mnapata adhab.anyway si jambo jema tujitahid kuvumiliana ila askar mtegemee meng sana kwa dunia ya sasa usipomweshimu mtu naye hakuheshimu.askar ni uniform tu tunawaheshimu kwa hlo lakin si kwa kuwa tunawaogopa.
 
Polisi wangefuata sheria hakuna ambaye angemkaba. Hebu tuangalie ni kifungu gani kinamruhusu Askari kuchomoa funguo ya chombo cha usafiri au kulazimisha polisi waachiwe funguo?. Wao ndio wamekuwa vyanzo vya fujo zote hizi unazoziona.
 
Anawatetea hawa?
 

Attachments

  • bom.jpg
    bom.jpg
    34.3 KB · Views: 42
  • polis.jpg
    polis.jpg
    64.3 KB · Views: 48
Huyu Jamaa aliyeandika makala hii sijui yupo Vatican ?!? Bila shaka hao unaojaribu kuwatetea wakafundishe kwanza haki za Kibinadamu...ni wanyama
 
Hahahahahahahahhaha,yule jamaa aliunyonga mkono wa traffik nikacheka sana kweli alipita ccp moshi yule polisi???
 
Waache kula rushwa na kuwabambikia watu kesi, pia waache kufanya upelelezi kwa kuwa kong'ota watu virungu vya mpingo bali wafanye upelelezi wa kisayansi. Wakiacha kutumiwa na watawala-wananchi watawaheshimu na kuwasaidia kazi zao! Yasipozingatiwa haya, polisi ataendelea kuwa adui wa raia mwema!
 
Mleta mada lazima atakuwa ni askari, kama ni raia wa kawaida basi mzazi wake au ndugu yake wa karibu ni askari. Ushauri wangu kwa mleta mada ajaribu kufanya research isiyo rasmi kuhusu namna polisi wanavyotekeleza majukumu yao sidhani kama atathubutu kuwaonea huruma.
Ndugu mtoa mada asilimia kubwa ya polisi hao unaowatetea ndio wanaongoza kwa vitendo vya rushwa, uonevu dhidi ya wasio na kipato, kubambikiza kesi ili wapate kitu kidogo n.k.
 
Nahakika mwandishi wa makala hii ni polisi, sielewi kwanini nae katumia nick name, imani kwa jeshi la polisi kwa wananchi wengi may be is only 20%, kama kuna hadi repoti za wao kuua raia, kubambikizia kesi, tena zingine kesi za mauaji n.k halafu eti mtu kufinywa kidogo tu unalalamika, hii ulipaswa kuipeleka pale polisi msimbazi na sio humu!
HAwajui polisi huyumleta uzi !nilimshitaki jamaa baada ya kunitapeli vijisenti kadhaa ,jamaa baada ya kukamatwa na kutiwa ndani wakamspice na mikwara fulani ikabidi aahidi kurudisha mpunga kesho yake.
Mke wa tapeli wangu akazileta asubuhi zikahesabiwa (it was 2m) askari akaniambia ni sign kuwa nimepokea kiasi hicho nikamwambia nitasaini vp wakati mpunga mnao nyie ?wakaendelea kusisitiza basi nikafuata maagizo yao,mtuhumiwa wangu akaachiwa -kivumbi kikaanza hapo kwenye kuchukua pesa zangu lilianza balaa hapo nikasamehe laki nzima tena huku wanalalamika kuwa kidogo haziwatoshi kugawana kwa 'kazi kubwa walionifanyia' !chezea vibaka uniform weye!
 
Huyo ndiyo kenyela bwana.................,mwepesi kusahau
 
Hiyo ndio dawa yenu ninyi policcm! , ukweli tumechoshwa nanya, rushwa nyinyi, kuua nyinyi, kubambikia kesi raia ninyi, kupora, hiyo ndio dawa yenu, p.u.m.b.a.v.u, hatauwezo wa kufikiri kwenu nimdogo, kwelikama umezaliwa na nyota ya mbwa, wewe utakuwa mlinzi maishani mwako.
 
Naomba niseme ya moyoni japo magumu kuyasema na machungu kuyasikia.

Hawa polisi wamezidi na wadhalilisha sana watu, wao hujifanya miungu watu. Ukweli wamechokwa na wananchi kwa jinsi hali ilivyo, na sasa wameamua kujitetea dhidi ya udhalimu huu. Hiyo ni mwanzo na cha mtoto kama utatazama mwelekeo wenyewe. Hivi sasa waTanzania hawajaanza kushambulia watu, hasira inaishia kwenye mali kama vituo, lakini siku wakianza kushambuliwa kama wao wanavyofanya sijui mwisho utakuwaje.

Polisi na serikali, Bunge Mahakama wanatakiwa watende haki. Hivi sasa hakuna haki, si muda mrefu watu wataanza kujitafutia haki.

UTAWALA si uongozi kwa sababu hatuna unatakiwa uchukue hatua ya kunusuru hali hii kwa KUANZA KUTENDA HAKI NA SI VINGENAVYO


 
Back
Top Bottom