Huu ni Ugonjwa Gani?

itagata

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
209
71
Habari za leo wana JF Doctor!
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo ambalo bado sijapata ufumbuzi wake. Nikiwa na dalili za ugonjwa wa maralia, sehemu ya mwisho ya uti wa mgongo juu ya njia ya haja kubwa huwa inapasuka na kusababisha maumivu ambao mpasuko Huo huwa unadumu kwa siku mbili au tatu halaf unatoweka.

Nimejaribu kwenda hospital na nikaelezwa kuwa hali hiyo inaweza kuwa inasababishwa na ugonjwa wa maralia.

Je ni kweli hali hii inasababishwa na dalili za maralia? Na nifanye nini ili kuitibu?

Naomba ushauri wenu madaktari mliomo humu JF.
 
Nenda kawaone Ma Daktari wataalaam hapo Hospitali ya Rufaa Muhimbili wakupime kwa vipimo vyote ndio itajuliakana kama wewe kweli una Maralia au Maradhi mengine. Kisha uje hapa useme ni nin kinacho kusumbuwa au kama haupo Dar nenda katika mji unaoishi kwenye Hospitali kuu ya Mkowa unaoishi watakusaidia hayo matatizo yako pole sana.
 
Salam,
Hapa naona niungane na mchangiaji mada hapo juu, hili suala lako linajibika lakini inakuwa ni vigumu kuweza kukujibu moja kwa moja kwa vile hujajieleza vya kutosha, mfano jinsia yako, umri, mda wa hilo tatizo, unapopata dalili za malaria (unakusudia ukipata homa) siku nyengine jaribu kusherehesha dalili vya kutosha.
Lakini kwenda tu hospitali na kupimwa vipimo vyote ni usumbufu kutokana na mda na gharama, hivyo ushauri kama ni mwanamke ungeona kumuona Daktari wa mambo ya kike inawezekana sana una uambukizo kwenye njia ya uke ua kwenye kizazi, pengine mifupa bali kama ni mwanaume utamuona daktari wa Mifupa.
 
kupima ni muhimu zaidi sana kweli jaribu kufuata ushauri wa hao ndugu walio changia hapo juu. ninaimani utafanikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom