tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 25,950
- 25,327
Tangu zamani waislamu na wakristo tumekuwa tukiishi kama ndugu huku tukishirikiana katika mambo mbali mbali ya kimaisha lakini kuna baadhi ya watu ambao wanataka kutugombanisha kwa maslahi yao binafsi.
Kuna waziri mwandamizi ambaye amesikika hivi karibuni akiwabagua waislamu akiwa ndani ya kanisa na amerudia uchochezi wake akiwa bungeni Dodoma.
Kitendo cha kudai kwamba wazanzibar wanataka kujitenga ili kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ikiwa serikali 3 zitapita, ni uchochezi unaolenga kuwadhalilisha, kuwachafua na kuwashushia hadhi waislamu mbele ya jamii. Aidha, kuwahusisha uamsho na chama cha siasa sio jambo la kulifumbia macho hata kidogo. Lengo lake ni kutaka kuwagombanisha waislamu na jamii. Na ni bahati mbaya maneno haya yametamkiwa ndani ya kanisa, kitendo ambacho kinalenga kujenga chuki kati ya waislamu na wakristo.
Jamani, tuwapuuze hawa wabaguzi kwani hawana nia njema na amani na mshikamano wetu tuliojijengea kwa muda mrefu sasa. Nawasihi pia viongozi wa dini waache kutumiwa vibaya.