Huu ni mwaka mbaya Tarime

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,462
4,364
Maafa Tarime!

2008-10-06 16:42:20
Na Waandishi wetu, Tarime

Kampeni za uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara zimelazimika kusitishwa kwa muda leo asubuhi baada ya maafa makubwa kutokea na kuwalazimu wagombea wa vyama vyote kwenda kwenye maombolezo.

Hadi tukienda mitamboni, mashuhuda wa maafa hayo wamesema kuwa tayari vichwa vya watu sita vimeonekana bila kiwiliwili huku watu wengine kibao waliosalimika katika tukio hilo la kusikitisha wakionekana wamejeruhiwa vibaya na wengine kufyekwa miguu, mikono na viungo vingine vya mwili.

Maafa hayo yametokana na ajali mbaya iliyotokea leo asubuhi iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace `kipanya` na lori moja la mafuta.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo mbaya imetokea katika kijiji cha Mika , baada ya lori la mafuta lililokuwa likitokea katika nchi jirani ya Kenya kuelekea Musoma, kugonga kipanya kilichojaa abiria.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema lori lililosababisha ajali hiyo ni lenye namba za usajili KAZ 821 Z, ambalo limekigonga kipanya chenye namba za usajili T 808 AHU.

Wakisimulia zaidi, wamedai mashuhuda kuwa baada ya kipanya hicho kilichojaa abiria kugongwa, kiliyumba na kwenda pembeni mwa barabara kunako mtaro, kisha kikageuka kuelekea kilikotoka na kisha kugongwa tena na lori hilo kwa namna ya ajabu.

Mwandishi wa Alasiri ameshuhudia matairi manne ya lori hilo la mafuta yakiwa yamekikandamiza kipanya hicho cha abiria kwa nyuma na kukiponda vibaya .

Pia mwandishi wa Alasiri amedai kushuhudia vichwa sita vya abiria vikiwa vimetenganishwa na viwiliwili vyao huku majeruhi wengine kibao wakichomolewa garini na wasamaria huku wakiwa hawana miguu, mikono na viungo vyao vingine baada ya kujeruhiwa vibaya.

Mara baada ya kusambaa kwa habari za tukio hilo la kusikitisha, viongozi kadhaa wa Serikali na wale wa vyama vya siasa walilazimika kukimbilia huko, miongoni mwao akiwemo Daktari Bingwa wa Mifupa, ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Rorya, Profesa Philemon Sarungi.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Dk. Sarungi aliondoka kuelekea Hospitali ya Wilaya ya Tarime walikopelekwa majeruhi wa ajali hiyo kwa ajili ya kusaidia namna ya kuwatibu wahanga.

Aidha, taarifa nyingine zikadai kuwa akribu wagombea wote wa ubunge na wapambe wa vyama vyao wamekimbilia katika eneo la ajali kwa nia ya kusaidia harakati za uokoaji, ambazo zilishaanza kufanywa na raia wema wakishirikiana na askari kadhaa wa jeshi la polisi.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Jeshi la Polisi likiwa chini ya uongozi wa Kamanda wa Operesheni Maalum wilayani humo, Kamishna Venance Tossi lilikuwa bize katika kuwaokoa wahanga hao.

Majeruhi majeruhi 18 walikuwa wameshaondolewa kwenye kipanya na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime kwa matibabu zaidi.

Pia polisi walikuwa wakiwazuia watu kusogelea katika eneo la ajali ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa hatari ya mafuta kuweza kulipuka katika eneo hilo.

Aidha, barabara ya Musoma kwenda Tarime ilikuwa imefungwa kutokana na ajali hiyo mbaya iliyoacha vilio vikubwa kwa wakazi wa jimboni humo.

Wiki iliyopita, ajali nyingine mbaya iliyowahusisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lebu wilayani Tarime iliwaacha watu kadhaa wakijeruhiwa huku wanafunzi wengine kadhaa wakifariki dunia baada ya kupata ajali wakati wakienda katika ziara ya kimichezo huko Nyamongo.

* SOURCE: Alasiri



Watanzania wanazidi kuteketea kwa ajali huko Tarime, baada ya Fusi ya wanafunzi sasa kipanya. Very sad, Mungu wafariji wafiwa.
 
Back
Top Bottom