Huu ni muda muafaka Rais Magufuli kuijua sura halisi ya Prof. Muhongo

Prof Muhongo ni mhusika namba moja. Alituambia hizo fedha si za umma lkn leo umma utatakiwa kulipa. Alipe yeye na familia yake. Inakera sana nchi hii kila siku tunapigwa na wajanja.
Hilo zigo linawahusu CCM wote waliojiapiza kua zile hazikua pesa za umma.
 
Mimi naamini professor sio fisadi naamini hivyo
Hiyo wizara ni moto tokea wakina Karamagi watoke
 
Hili suala Kafulila alishawahi kusema kua tusipokua makini tutalipa tu, lakini leo hii yametimia.
Na kuna watu walimbeza sana na kumkejeli na kumpiga vijembe lkn sasa matokeo yake leo hii wote tuna kabidhiwa kikombe hicho hicho
 
Hakuna mahala ambapo muhongo anahusika na hili sakata hili suala limeanza wakati wa mwinyi wewe unazungumza kiurahisi ukiwa kama mwanangezi wa haya mambo.

Kuna Siku utanifanya nipigwe ban, tunaongelea pesa za umma hapa sio za CCM, ulifuatilia hili sakata vizuri bungeni? Usijitoe ufaham kwenye mambo ya msingi. Haijalishi lilianza lini, tunatakiwa tulipe deni, pesa ilitolewa huyu waziri akiwa kwenye hiyo wizara husika na ulisikia kauli zake kuhusu escrow, huenda angeshauri vizuri maamuzi yake yakazingatiwa Leo hii pesa zingetolewa BoT na deni kulipwa.

OK kama lilianza awamu nyingine can you admit kwamba CCM messed up? You can't get away with this one, just like EPA, lugumi and the likes
 
Hakuna lolote!, deni tutalipa kwa mzigo huo kubebeshwa Watanzania wote kupitia kupandishwa kwa bili ya umeme na hakuna atakayeguswa kwa sababu kama ni Kutoa asante, ameanzia juu mpaka chini!, utamgusa nani, umuache nani?.

Kwani Richmond ilikuwaje? !. Mkataba ulivunjwa tukashitakiwa na kudaiwa tozo ya Dowans, watu bungeni wakajiapiza hatulipi na kuna wengine wakaapa kwa kiingereza "over my dead body!" (kuliko kulipa bora nife). Ukweli ni kuwa, deni lile limelipwa lote kimya kimya, gharama za umeme zimepanda kimya kimya na Watanzania wote tunalipia deni hili na hakuna yoyote aliyechukuliwa hatua zozote!, miongoni mwa wakajiapiza wengine ni mawaziri na wanaendelea kudunda!.
Pasco

Alaf bado tunajisifu nchi ya amani, ifike mahala tutofautishe ujinga na amani japo vina mahusiano lakini ni vitu viwili tofauti. Ukihoji utaambiwa mchochezi. Lugumi wapi?
 
Umaskimi wa watanzania wengi unasababishwa na mengi.
Utajiri wa wachache ni uonevu kwa hawa wanaoitwa Watanzania wa kawaida au watanzania wa kipato cha chini
 
Hakuna lolote!, deni tutalipa kwa mzigo huo kubebeshwa Watanzania wote kupitia kupandishwa kwa bili ya umeme na hakuna atakayeguswa kwa sababu kama ni Kutoa asante, ameanzia juu mpaka chini!, utamgusa nani, umuache nani?.

Kwani Richmond ilikuwaje? !. Mkataba ulivunjwa tukashitakiwa na kudaiwa tozo ya Dowans, watu bungeni wakajiapiza hatulipi na kuna wengine wakaapa kwa kiingereza "over my dead body!" (kuliko kulipa bora nife). Ukweli ni kuwa, deni lile limelipwa lote kimya kimya, gharama za umeme zimepanda kimya kimya na Watanzania wote tunalipia deni hili na hakuna yoyote aliyechukuliwa hatua zozote!, miongoni mwa wakajiapiza wengine ni mawaziri na wanaendelea kudunda!.
Pasco
Unapo changia hoja kama hii toa pia njia mbadala ya kutatua tatizo na kwakuwa hili limeshatokea basi angalau walio sababisha haya maumivu kwa watanzania tuwaone wakipewa adhabu na tuione
 
So far huna ushaidi kuwa Prof kahusika...
Ukiangalia maelezo yaliyopo ni utata mtupu...ni issue ya kisheria ambayo Muhongo sijui anahusika vipi? wale waliokuwa wanatafsiri sheria na kutoa amri jamaa walipwe ndio wakutueleza kinaga ubaga...yeye akatalie kutoa pesa na wakubwa zake wamebariki ni nani? yake?

Najiuliza kama walijua kuna utata na kesi kati ya hao wamiliki wa IPTL na Standard Chartered kwa nini waliharakisha kulipa badala ya kusubiri? Aliyetoa amri ya kutoa hizo pesa ndio ashughulikiwe? hii nchi bana...

Wakati mwingine unatamani TANESCO iuzwe...imekuwa mzigo kwa watanzania...tunalipa price ambayo si ya soko ili kunufaisha mafisadi...

Kama kungekuwa na shirika lingine shindani tusingesikia huu ufisadi...unaongeza bei umeme unatumia mwenyewe
 
Magufuli alisema alichelewa kuteua baraza la mawaziri kwa kuwa alikuwa anatafuta anae faa, ina maana huko ccm ya muhongo ni afadhali kuliko alio waacha itakuwa ya wengine wanayajua wenyewe sio wananchi, sasa akiamua kuatafuta anaefaa kuna hatari ya kukosa baraza la mawaziri wenyewe wana wimbo wao ccm ni ileile.
 
Hata sielewi yani...kama Standard Chartered walikuwa wanaidai IPTL why wanaishitaki Tz????!!!!
Si wamsitaki mdeni wao na kumfilisi???!!!
 
Nasikia Jimboni kwake ametoa Ambulance nyingi na jana kagawa vitabu vya milioni 500. Pia ana gari mpya kali sana. Hivi katoa wapi hela Prof au nae alilamba za Escrow?
Muhongo hajawai kuwa masikini hata kabla ya kuwa mwanasiasa...pale UD alikuwa ni mmoja wa watu wenye gari kali sana enzi hizo za mwalimu...anajipenda na ni muhimu kwenye field yake...anatumia ubongo wake kupata pesa...
 
CCM HAKUNA AFADHALI WOOOOTE NI POTELEA MBALIIII
Safi sana! Tutawajadili CCm hadi lini? Wenye kutumia akili zao vizuri walishajua kuwa ukoo wa wezi ni wezi wote tu. Wanaridhishana. Mawazo ya mwanadamu yakifika mwisho ndipo Mungu huanzia, sasa kwa hili la CCM kulindana tumesema tumechoka na tumefikia mwisho. Ukiwasema hivi wanatumia Polisi kukupiga, wanatumia vyombo vingine kukukandamiza. Sasa tufike hatua tumwachie Mungu hili tuone namna atakavyowahukumu.
Waadilifu tunateseka, wezi wanakula nchi? Escrow, Epa, IPTL, Lugumi, mTambo mengi sana hadi nashindwa kujua ni kwa nini watanzania wamepigwa upofu kutoona mabaya ya CCM kwa miaka mingi hivi!
 
Back
Top Bottom