MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Kama kuna watu ambao walihisi Prof Muhongo alionewa kuhusishwa na kashfa ya ESCROW na Mkuu wa kaya nae anaamini hivyo kuwa alionewa, na hii ndio maana alimrudisha tena kwenye wadhifa wake wa awali wakati huu wa ufalme wake.
Sasa wa kuifahamu ESCROW A-Z ni Rais Magufuli baada Tanzania kuamriwa kulipa billion 320, hapa ndiko atakapojua ni nani mhusika kweli wa Sakata la ESCROW, hapa ndipo atakapojua kuwa uteuzi wake kwa Prof. Muhongo una tija kwa taifa au laah! Nina uhakika mkuu hatakubali haraka haraka kulipa zigo hilo lote pasipokujua ni nani amelitia taifa hasara.
Je, akikuta ni kweli Prof Muhongo nae alikuwemo kwenye michongo hiyo atamwacha aemdelee kuchapa kazi kunako wizara?
Je, atakuta Prof aliingizwa tu mkenge pasipo kujua na waliokuwa wamazunguka?
Mimi sina jibu kamili lakini kwa wakati huu tu pekee mkuu ataitambua taswira halisi ya Prof. Muhongo.