Huu ndo ukweli.

tryvenak

tryvenak

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
245
500
TOFAUTI YA UCHANGIAJI WA MADA KTK SOCIAL NETWK KATI YA MAREKANI NA BONGO:

Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?
WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0772084823 Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..
MTUMISHI:

Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...


Sent using My bundle
 
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,473
2,000
Hiyo inaonesha how wabongo tusivyopenda mambo ya kijinga
 
Internal

Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,385
2,000
Kuna vitu vya kujadili na vingine sio vya kujadili. Wabongo tukiona sio la kujadili tunafunga mjadala mana kwenye kujadili unaweza kuzidiwa hoja na suala ni la kipumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom