Huu Ndo Ukweli kuhusu Mkoa wa Mara

Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
3,162
6,532
Imefika kipindi muache kutuangalia kwa jicho la chuki, haiwezekani kila kinachooneshwa kutoka mkoa wa Mara ni flani kakatwa, flani kachinjwa au yule kajeruhiwa na kadhalika.

Kama ipo hiyo ni tabia ya mtu tu sio sote, pia majanga yapo kila kona sio Mara Pekee, kuna mengi ya kufurahisha kuhusu Mara sio hayo tu yanayokuzwa na vyombo vya habari

Karibuni Mara chimbuko la muasisi wa taifa la Tanzania, amani Ipo na imetawala, Mje Kuoa, kuwekeza na kuishi

usisikie tu njoo ujionee mwenyewe kwani mengi yanayosikika ni uzushi tu, hakuna kitu kama hicho.

Kwani watu ni wakarimu na Amani imetawala, mengi yanayoenezwa ni propaganda za mitandao tu na chuki binafsi kwani Majanga Yapo kila sehemu. Wenyeji wake ni wakarimu na wapenda amani, ni Mkoa wenye Amani na Upendo.

Ukifikiria kuitembelea Kanda ya Ziwa, Usisite kuja Mara, Japo yanasemwa Mengi ni Uzushi tu.

Karibuni Sana.
 
Huwezi utuhadaa namna hii. wewe mwenyewe umeshindw kuelezea hayo mazuri unayoyaita. na kama hayo uliyoyataja ndiyo mazuripekee basi yanazidiwa na mengi mabaya tunayosikia kwenye vyombo vya habari. Hebu tushawishi zaidi basi
 
Imefika kipindi muache kutuangalia kwa jicho la chuki, haiwezekani kila kinachooneshwa mara flani kakatwa, flani kachinjwa hiyo ni tabia ya mtu sio sote pia majanga yapo kila kona sio Mara Pekee, kuna Mengi ya kufurahisha kuhusu Mara sio hayo tu yanayokuzwa na vyombo vya habari

Dont Try to Understand Women, Women Understand Women And they Hate Each Other!

NAOMBA UNIPE TOFAUTI YA ''GENERALIZATION'' kati ya Uzi wako na Signature yako..
 
Imefika kipindi muache kutuangalia kwa jicho la chuki, haiwezekani kila kinachooneshwa mara flani kakatwa, flani kachinjwa hiyo ni tabia ya mtu sio sote pia majanga yapo kila kona sio Mara Pekee, kuna Mengi ya kufurahisha kuhusu Mara sio hayo tu yanayokuzwa na vyombo vya habari, Karibuni Mara Amani Ipo Mje Kuoa kuwekeza na Kuishi, Usisikie tu Njoo Ujionee mwenyewe mengi mnayosikia Ni Uzushi Tu, Hakuna Kitu kama Hicho.

kwani watu ni wakarimu na Amani imetawala mengi yanayoenezwa ni propaganda za mitandao tu na chuki binafsi kwani Majanga Yapo kila sehemu. Wenyeji wake ni wakarimu na wapenda amani, Ni Mkoa wenye Amani na Upendo.

Ukifikiria kuitembelea Kanda ya Ziwa, Usisite kuja Mara, Japo yanasemwa Mengi ni Uzushi tu.

Karibuni Sana.

Mrudisheni Kaoge Musoma awe mkakamavu huku mlipomleta anaharibu sifa za Mara.
 
Njooni Mara bhana..acheni uoga wakuu.. Huku ni kazi na dawa tu.. Njoo Serengeti upate Nyama singisi, Njoo Musoma ufanye biashara, Tarime kuna arable land nzuri.. Ndizi, parachichi tamu haswaa hata za Moshi au Tukuyu hazifikii..tena bei chee Tarime mjini ndizi 10 buku tu..ha ha..Pia ipo Border ya sirari na imechngamka na utapata watoto moto akina Gati na Rhobi..Njooni na Rorya huku Muwekeze kwenye biashara za samaki wako wengi wa kutosha..

NB: Ukiwa unakuja hakikisha umetahiriwa; ndo stigma inapoanziaga.
 
Back
Top Bottom