Huu ndiyo utawala bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndiyo utawala bora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by antendembaga, Feb 25, 2012.

 1. a

  antendembaga New Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilishtuka na kuogopa sana juzi nilipopata taarifa kuwa askari polisi huko Songea wanauwa binaadamu tena watanzania wenzetu kwa risasi za moto. Ghafla nilijikuta napiga simu ovyo ovyo lengo nipate kujua kama ndugu waliopo kule wamesalimika na kadhia hiyo.

  Inashangaza polisi kuuwa raia tena wasio na kosa lolote eti kisa wanaandamana,sina hakika na aina ya mafunzo wanayopata huko Moshi labda ni ukakamavu pekee. Kote duniani polisi wamekuwa wasomi na wenye kufanya maamuzi sahihi,ingekuwa hivyo huko Syria raia wote wangekuwa wameshauliwa.

  Huu ni ubabe,unyanyasaji na udhalilishaji ambao kwa namna yoyote haukubaliki. Kikwete na vikaragosi wake wamekaa kimya hakuna wanalofanya, wananchi wafanye nini sasa.Wakichukua hatua wanalalamikiwa, wafanye nini ikiwa ndugu wanauwawa kama fisi.

  Huu ni utawala bora au uhuni na ubabe? Haiwezekani na haikubaliki ndugu zetu wauwawe wakati sisi tunachekelea tu,hatukubali. Tutapambana na kitaeleweka. Serikali makini huhakikisha raia wake wanalindwa kwa gharama yoyote ile.

  Nawataka wanasongea kutorudi nyuma na mapambano na uonevu huu,huku mkiona madhila ya serikali hii.Kosa lenu nini? Kukichagua CCM 2010 leo iwe kosa, mnalipwa kuuawa ndugu zenu! Pambaneni, tuko pamoja.
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe ulitaka wapigwe manati?
   
Loading...